kujisifu hatua nzuri ya kumkaribia shetani...

kujisifu hatua nzuri ya kumkaribia shetani...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,419
Reaction score
17,765
katika ulimwengu wa waamini Mungu, utajifunza kuwa sifa zoote za mazuri mtu afanyayo ni KWA MUNGU.

Mungu pekee ndiye anayestahili sifa,kutukuzwa,kuabudiwa,kuenziwa.

kwa upofu wa ukweli huu katika jamii ya waaminio Mungu wafuasi tumejikuta tukimiminia sifa,tukiwatukuza, tukiwaenzi na kuwasujudia viongozi na vinara walio mstari wa mbele ktk imani.

shambulio hili, shetani amefanikiwa kujikusanyia maelfu na kuleta mgogoro mkubwa kati ya waamini Mungu na Mungu wao.

SIFA, UTUKUFU,UWEZA na enzi ni kwa Mungu tu. Kamwe usiruhusu mwanadamu akachota hata punje za sifa zilizomstahili Mungu. au wewe kujirundikia masifa yaliyomstahili Mungu anayekuwezesha.
kwa kufanya hivyo (kujisifu) tunakuwa tumepiga hatua nzuri gizani kuuchuchumilia ufalme wa giza.
 
Back
Top Bottom