Kujifunza kutokana na makosa

Kujifunza kutokana na makosa

outsider

New Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
4
Reaction score
0
katika maisha yetu ya kila siku ni rahisi sana kuona madhaifu ya wenzetu,huku tukiamini kuwa sisi tuko salama.ubaya unakuja pale tu mabaya yetu yanapoanikwa live kwa wengine.tunajiona kama tumedhalilishwa na hivyo ili kujifariji tunajaribu kujisafisha kwa kila namna ili kuupinga ukweli,badala ya kuchukua jitihada za kujifunza kuishi vizuri na watu, tunapoteza muda mwingi kulumbana na watu na kuendekeza chuki kwa vile tu fulani kaweka mambo yangu hadharani.hakuna mkamilifu,ila wajanja wa maisha ni wale walio tayari kujifunza kila siku ili kwamba wawe kielelezo kwa wengine wanaomtazama.hatutakiwi kuwa waoga wa kufanya makosa au kukosolewa bali tunapaswa kuwa jasiri wa kukubali ukweli na kuanza na pale tulipo haribu.
 
Kakangu alinifundisha kitu kimoja nikiwa mdogo bado. Ukiambiwa kitu kuhusu wewe una step kadhaa za kuchukua.
1. Elewa unachoambiwa na kwa nini unakosolewa. Yaani mtazamo wa wengine ukoje juu ya suala husika.

2. Fanya self evaluation kama ni kweli ama hawakuelewi tu. Manake misinterpretation zipo tu. Huhitaji kufanya clatification kwa yeyote unless you want to.

3. Amua. Kama ni kitu utakachotaka kubadilisha ama kama umeamua kwa dhati hivyo ndivyo unavyotaka kuishi maisha yako.

4. Chukua hatua. Kama ndo hutaki kubadilika yaani ongeza kasi. Kama unataka kubadilika look out for your options.

Mtoa mada, haijalishi huyo anaekuambia ama kukukosoa kaambiwa na nani ama imekuwaje. Inajalisha kama info ni za kweli, bhaaaaas! Na ukijikosoa unajiongeza. Unaingia kwenye ngazi nyingine.
 
Back
Top Bottom