Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,243
- 12,769
Moja ya mambo yaliyowaingiza wanadamu wengi matatizoni ni kutafuta pongezi na sifa. Moja ya mambo yaliyopelekea watu kutapeliwa, kudhuriwa, kupta hasara na kuwa-taken advantage of ni kusifiwa na kupongezwa.
Asilimia kubwa ya pongezi na sifa unazopewa ni za kinafiki, ni za watu wanaotaka kitu kutoka kwako. Pongezi na sifa huwa ni katika kukulainisha. Epuka sana kufuatilia pongezi na sifa.
Jenga ukuta kuzuia pongezi na sifa. Jenga akili yako isijali pongezi na sifa. Njia moja ni kukumbuka kutoshukuru mtu akikupongeza au akikusifia, hilo litamdiscourage asiendelee na mpango wake wa kukulainisha.
Njia ya pili ni kuacha kutafutiza kupongezwa na kusifiwa, kwa jinsi gani? Acha kuelezea mafanikio na mipango yako kwa watu. Acha habari za mwanangu hivi, kazi yangu vile, biashara yangu hivi, mke wangu vile, mume wangu kalikwenda kakarudi nk nk.
Ukiacha kujali na kufuatilia kusifiwa na pongezi utaishi maisha huru sana.