Kama kuna mtu anaelewa hili naomba anijulishe:
Mimi ni mkazi wa Dar, kadi yangu ya kupiga kura imepotea. Awali nilijiandikisha kituo cha Kimara Stop-over (wilaya ya Kinondoni), lakini sasa naishi Tabata (wilaya ya Ilala). Kwenda Kimara ku-renew ambako ndio kituo changu cha awali naona taabu kwa ajili ya foleni na muda mwingi utapotea. Je, naweza kujiandikisha hapa hapa Tabata?
Nikikumbuka mheshimiwa JK naye alihamia Msoga badala ya Chalinze alipopiga kura awali.