Kujenga nyumba kwa Tshs. milioni 7 inawezekana?

Jana mmoja aliuliza tzs 10m inatosha kujenga? Leo wewe unauliza tzs 7m inatosha kujenga? Kesho mwingine atakuja kuuliza tzs 4m inatosha kujenga? Ngoja tusubiri wataalam wa ujenzi waje watuambie maanake mimi nitakwambia hio inatosha madirisha na kuezeka nyumba ya vyumba viwili tu.
 
Jana mmoja aliuliza tzs 10m inatosha kujenga? Leo wewe unauliza tzs 7m inatosha kujenga? Kesho mwingine atakuja kuuliza tzs 4m inatosha kujenga? Ngoja tusubiri wataalam wa ujenzi waje watuambie maanake mimi nitakwambia hio inatosha madirisha na kuezeka nyumba ya vyumba viwili tu.
Eee sawa si kila mtu anauliza pale alipo? Sasa aulize mil. 200 ambazo hana.
 
Mkoani yaeza tosha kwa sebule vyumba viwili maana huko tofali za udongo zmechomwa...... Kwa daslaam mzee ni za tofali na bati tu
 
jaribu kupiga hesabu ya tofali na gharama za vitu vingine walau approximate uone kama inatosha anza na chumba na sebule ikitosha ongeza chumba cha pili walau upate rough approximation....wengi tutakaokudis hatuna kiwanja, nyumba wengi tumepanga na tunamiliki smartphone, au laptop na wachache gari ....so ushauri wetu usikukatishe tamaa
 
Jenga ya miti halafu unakandika kwa udongo wa mfinyanzi halafu unai-skim! Ezeka kwa mabati ya migongo midogo lakini ya rangi! Weka Dari ya fito na ukandike udongo wa mfinyanzi na ui-skim!
Iwe Nyumba ndogo ya vyumba viwili kimoja master na jiko na public toilet! Weka tiles!
MTU akikutembelea atadhani imegharimu 30m! Kwa kifupi gharama kubwa iwe kwenye finishing!
Ina uwezo wa kudumu kwa zaidi ya miaka 50 bila nyufa!
 
Hahahaha
Kuna jamaa yangu kwa nyumba chumba 1 na sebule kwa 8 millions aliishia kwenye mkanda wa juu tu

Inawezekana hata msingi usiishe kama eneo ni bondeni na kunatakiwa leveling ya kutosha ili uanze kunyanyua ukuta
 
Nyumba ya kisasa ni ipi?

Gharama ya nyumba kuwa kubwa au ndogo inategemea vitu vingi, mfano upatikanaji wa maji, mchanga na usimamizi.

Ushauri; Ramani yako iwe hivi sehemu ya kulia chakula na jiko viunganishe(2.5m kwa 4m) hiyo iwe ndani kwa ndani,sebule iwe 3m kwa 3.5m, vyumba vya kulala weka viwili tu chako 3m kwa 3m cha watoto 2.8m kwa 3m ,pia weka na cho cha wote kimoja.
Usitumie mawe kwenye msingi, msingi zungushia nondo tatu tatu kuzunguka nyumba. Pandisha matofali usawa wa linta weka tofali 8 kutoka kwenye msingi, halafu zungusha linta nondo tatu tatu kuzunguka nyumba na usawa wa vyumba hata linta ya nondo 2 itafaa. Ukifika hapa simama uniambie umebakiwa na kiasi gani.

Tofali fatua mwenyewe mifuko 50 kila mfuko tofali 45, hapo utapata tofali 2250,kumwagilia ufanye mwenyewe au mkeo ili okoa gharama za umwagiliaji.

Kama eneo lako linatoa mchanga chimba mchanga hapo hapo, hapo utapata na shimo la choo na mashimo mengine utayafukia taratibu taratibu na taka za majumbani.

Ili hela itoshe usimamizi ni wa hali ya juu, usipoteze hapo hata mfuko mmoja wa semeti, mafundi wana tabia ya kufukia mifuko arithini usiku wanairudia.

Hadi hapa unaweza kutumia 4,500,000 fundi utakae mpa kazi mwambie una laki 8 mpaka tofali mbil za juu ya linta, mafundi ni wengi kazi hakuna atajua atakavojipanga hela itoshe.

Ukishapigiwa mahesabu ya mbao nenda mwenyewe buguruni, siku ya kwanza zunguka maduka yote ya mbao ulizia bei, wakikuona unazunguka sana kutafuta bei ya chini ,atatokea mmoja wao atakutajia bei halali kwa mita akijua kua atakuibia, ukishakubaliana nae chukua mawasiliano yake kesho yake nenda na futi kamba yako kwenye begi, waache wakuchagulie mbao wao kwa futi kamba yao,idadi ikifika wakati wa kupakia pakia mbao kwa kutumia futi yako. Hapo watakuibia kwenye uandishi andika mwenyewe, hapo muwe watatu wewe fundi wako na ndugu yako mmoja. Wawili wanapima wewe unaandika ndio mbao inapakiwa kwenye gari. Hapo watakubali iwe hivo mana wanajua watakuibia kwenye kujumlisha mita za mbao. Hapo ili uwapatia wakijumlisha jibu andika pembeni, halafu mpe mwingine ajumlishe jibu andika pembeni na mwishowe jumlisha wewe kwa umakini walipe ondoka zako, nakuhakikishia utaikoa zaidi robo ya gharama za mbao.

Weka mabdrisha, milango miwili jikoni na sebuleni, usipige ripu, flow wala usiweke wiringi ya umeme ,weka mapazia hamia,tengeneza choo cha nje hamia, vilivyobakia vyote utamalizia kidogodogo ukiwa humo humo ndani.

FANYA HIVI TUPE MREJESHO
 
Back
Top Bottom