Je uhitaji wako katika maisha hukuweka katika hali gani?.
Siku baada siku zimepita, ni wiki kadhaa zimeisha, kama si 2 basi 3 zimepita, mambo nilivyotarajia hayajatimia, hivyo basi moyo wangu ukaugua, akili yangu ikanipa ufahamu, nikakumbuka Mithali 13:12 Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima., ubongo ukanikumbusha kuwa uone michongo inapofeli, huyo ni dizasta vina katika wimbo wa karibu duniani.
Katika wiki, moja ya siku, jana yake nilitafutwa nikawa sipatikani, maana nilitalajia kuanzima pesa hivyo sikuwa na bahati, uaminifu, ukweli, upole bado havina nafasi, vipi kukopa kukopeshwa kwako vina nafasi, moyo huugua unapokosa hitaji, nagundua moyo haupo katika nafasi, rejea katika kitabu cha mathayo 13:7-9-22... Mathayo 13:7, 9, 22
7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;
9 Mwenye masikio na asikie.
22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
pia rejea katika mathayo 9:13...Mathayo 9:13 Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
Masaa yakasonga hatimaye nuru ikatoka azimio nikatimiza, miminiko la furaha likamwagika, ni nini hiko basi, ni> freezer, pesa nilizotarajiwa kuanzimwa nikapata, asante ni wakati wa kuzirudisha sasa.
Kuna kitu nimejifunza katika safari hii ya kununua freezer, maana nilikuwa nalipia kidogo kidogo, lakini nilijijenga kimchakato wa kifedha hatua hiyo ilinipa utayari wa kwenda kuanza kulipia kidogo kidogo hadi kumaliza. hata kama nimeanzima pesa basi ni kiasi kidogo ambacho naweza kulipa ndani ya muda mfupi.
Moja ya malengo yangu ya mwaka huu yalikuwa ni kuwa na freezer, kwa maana naona linakwenda kuongeza kipato changu na kupiga hatua nyingine ya kimaisha.