kuitwa usaili TRA

Mkipata kaz msianze ku2zingua kitaa jamani mkumbuke hilo, maana cc wabongo 2kiwa nazo tunasahau ya zamani dah!
 
kama weye wamekupigia kwa nini wengine tusitumiwe hata sms tu jaman, je gharama ya kubox na kupiga simu ipi nafuu! au ndo wengine mshapata na ajira?
 
mi nimetoa taarifa tu ila watu wapo wengi tu wamepigiwa simu...km unam2 unaemjua muulize akupe habari
 
Mdau wewe uliomba nafac gani?kwani nakumbuka posts zilikuwa za aina nyingi.Asante mkuu kwa taarifa
 
hongera sana..na ukafanye mambo, vipi mnaenda kufanya paper au ni oral moja kwa moja..??? kama ni paper pole sana hapo mnasindikiza watu..hii ndi TZ yetu
 
mi niliomba tax officer na iyo itakiwa written interview...sina uhakika ila inawezekana safari hii hawakuita watu wengi sana
 
tax officer mkuu

mmh kijana huwezi ukaanza ukawa tax officer ni assistant tax officer alafu kuna bonge la mchujo so get prepared ili usije ukaregret lakini maisha si tra tu jaribu kuangalia sehemu kama NHIF wazuri sana
 
Daa jaman mbona wengine wametuchunia ili balaa sasa,anyway suburi nijiunge na chama cha kufa na kuzikana hapa kazini.
 
Mkubwa ahsante sana kwa taarifa mm pia niliomba zile nafasi lakini wamenikaushia, au mambo ya kichaga bado yapo? Nchi kweli imeuzwa hii.
 
Mimi niliomba nafasi ya Preventive Assistant TRA na sijapigiwa simu wala barua kutumiwa bado.Je inawezekana miongoni mwa walioitwa ndo hao mapreventive assistants nini!.Tujulishane jamani manake taarifa hizi hazimo hata ktk mtandao wa TRA hazipo.Sijui kwa nini ni mambo ya siri siri.
 
Mi ninachoshauri, waambieni wadogo zenu wasome sana ili wasiwe kama wahasibu niliowaona last week ofisini kwetu. Nakubari kuwa waliosoma uhasibu ni wengi lakini wanaoujua ni wachache! kwa hiyo msiogope tu wingi, wengine ni kama wamesoma hakuna!

Mi nafanya kazi na international org hapa tz, tangu mwezi jana tulikuwa tunaitaji wahasibu wawili, hatukutangaza gazetini, ila tulitangaza ndani humo. tulipokea application zaidi ya 400. tukaamua kuchuja, tukatafuta wenye GPA above 3.5 ili kuwapunguza, huwezi amini tulibaki na less than 30 application! Tukaongeza kigezo cha mtu awe angalau na full Module E, tulibaki na sita tu!

Kwa hiyo jamani msilahumu sana, kwanza GPA zinawaruhusu au mnairahumu tu serikali? eti mtu ana 3.0, naye anataka aitwe NAO! si utani huu! ni huu jamani.

kama hukuitwa uache visingizio, mara umangi sina mara nini, jipeleleze kwanza wewe mwenyewe kama unastahil. Mi ninachojua Huingii TRA kama huna angalau upperr!
 
Huo ni mtazamo hasi kabisa, ni ajabu unataka kutwambia kwamba mtu anayejua vitu ni yule mwenye GPA ya 3.5! hii ni ajabu mno.Nakumbuka mzee Nimrod Mkono pamoja na kuwa Advoket anayeheshimika kwa umahili wake aliwahi kuwaambia applikants wa kazi ktk firm yake kwama yeye haangalii GPA kwani hata yeye ana lower second.Lakini hata Jaji mkuu mstaafu Ramadhan aliwahi kuwaeleza wanafunzi aliokuwa anawafundisha pale chuo kikuu cha Zanzibar juu ya yeye kuwa na lower second class.Wanasheria wengi, madaktari na mainjinia hupata lower second kutokana na masomo haya kuwa magumu kidogo, lakini hii haiwazuii kufanya vizuri ktk kazi.Hii inanikumbusha upuuzi uliofanyika pale Udom eti wakati wanashortlist ktk baadhi ya posts walikinzana sana lilipokuja suala la nani apite kati yule wa Mlimani mwenye lower second na wa Makumira mwenye upper second.Hoja ikatoka ktk paneli hiyo ati mtu akasema heri ya C ya mlimani kuliko A ya vyuo vingine.nAKUBALI KWAMBA GPA ina msingi sana kuiangalia sana kwa malengo ya kupunguza watu kama ulivyosema kwamba mlifanya, ila hoja ya kwamba pasipo Upper second haajiriki, hiyo ni hoja hewa.Hata hivyo wapo wanaojua maksi wanazipataje.We fikiria ktk darasa langu la Tax lenye wanafunzi 180 ktk chuo nilichokuwa nasoma demu mmoja tu aliyekuwa anatoka na mwalimu ndiye pekee aliyepata A ya Tax Law, na mabinti wawili marafiki za yule demu ndo walipata B+ wengine tukaangukia B, C, na supplementary za kumwaga.
 
Mi ninachoshauri, waambieni wadogo zenu wasome sana ili wasiwe kama wahasibu niliowaona last week ofisini kwetu. Nakubari kuwa waliosoma uhasibu ni wengi lakini wanaoujua ni wachache! kwa hiyo msiogope tu wingi, wengine ni kama wamesoma hakuna!

Mi nafanya kazi na international org hapa tz, tangu mwezi jana tulikuwa tunaitaji wahasibu wawili, hatukutangaza gazetini, ila tulitangaza ndani humo. tulipokea application zaidi ya 400. tukaamua kuchuja, tukatafuta wenye GPA above 3.5 ili kuwapunguza, huwezi amini tulibaki na less than 30 application! Tukaongeza kigezo cha mtu awe angalau na full Module E, tulibaki na sita tu!

Kwa hiyo jamani msilahumu sana, kwanza GPA zinawaruhusu au mnairahumu tu serikali? eti mtu ana 3.0, naye anataka aitwe NAO! si utani huu! ni huu jamani.

kama hukuitwa uache visingizio, mara umangi sina mara nini, jipeleleze kwanza wewe mwenyewe kama unastahil. Mi ninachojua Huingii TRA kama huna angalau upperr!

acha uhaya wewe GPA siyo kujua kila kitu na siyo kigezo kizuri cha kuajiri
 
Back
Top Bottom