Kuishi pasipo na matarajio yoyote ni aina nyingine ya kupoteza mwelekeo wa akili

Kuishi pasipo na matarajio yoyote ni aina nyingine ya kupoteza mwelekeo wa akili

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
7,289
Reaction score
11,787
Kuna hali ambayo haizungumzwi sana-ya mtu kuishi bila matarajio yoyote, bila malengo, na bila hata shauku ya kubadilisha maisha yake.

Hii sio tu hali ya kawaida, bali ni ishara ya kupoteza mwelekeo.

Ikiwa unaishi pasipo kutarajia chochote, tafsiri yake ni moja tu- hujajaribu chochote.

Kwa sababu matarajio hujengwa na hatua.
Yanatokana na jitihada, majaribio, na uthubutu wa kuanza.

Mtu asiyejaribu:

•Hana kitu cha kutegemea
•Hana dira ya maisha
•Hana sababu ya kujisukuma mbele

Na hapo ndipo anapoanza kuishi chini ya uwezo wake halisi.

Kwa lugha rahisi, anakuwa mtazamaji wa maisha ya wengine, badala ya kuwa mshiriki.

Wakati wengine wanajaribu, wanashindwa, wanajifunza na kusonga mbele-yeye anabaki pale pale, akisubiri siku zipite.

Kijana aliyepo katika prime age yake hapaswi kuwa katika hali hii.

Hiki ni kipindi cha:

•Kujaribu fursa mbalimbali
•Kujifunza ujuzi tofauti
•Kukutana na changamoto na kuzitatua
•Kujenga uthubutu na kuzoea hatari za maisha

Kwa sababu ukweli ni huu - uwezo hauji kwa kufikiri tu, unajengwa kwa kufanya.

Mfano:

•Kijana anayejitosa kwenye biashara, hata ndogo, anajifunza thamani ya pesa na nidhamu ya soko
•Anayeanza kazi za mikono anapata ujuzi wa vitendo unaompa uhuru wa kujitegemea
•Anayejifunza skill mtandaoni na kuanza kuitumia, anajijengea thamani inayolipika

Lakini kijana asiye na matarajio:

•Anaahirisha kila kitu
•Anaogopa kuanza
•Anaishi maisha ya mazoea yasiyo na changamoto

Matokeo yake?
Miaka inapita - lakini hakuna kinachobadilika.

Ni muhimu kuelewa kwamba:
Kutokujaribu si utulivu - ni kupoteza muda kimya kimya.

Hata hivyo, kuna mstari muhimu sana:

Jaribu, lakini usipoteze utu wako
.
•Usijihusishe na mambo yasiyo halali
•Usishushe heshima yako kwa tamaa ya matokeo ya haraka
•Epuka njia za mkato zinazoweza kukuathiri baadaye

Mafanikio ya kweli yanajengwa juu ya nidhamu, uvumilivu, na maamuzi sahihi.

Kwa kifupi:

•Mwenye matarajio anachukua hatua
•Asiwe na matarajio, mara nyingi hajawahi hata kuanza

Na mwisho wa siku, maisha hayataangalia ulikuwa na uwezo kiasi ganiyataangalia- ulichofanya na huo uwezo.

Jiulize leo - una kitu chochote unachotarajia, au ni “yote kheri” tu? 😀
 
Huwezi kuwa na expectations kama huna actions unazochukua.

Matarajio ni zao la uwekezaji wa nguvu au akili, huwezi kutegemea kuvuna mahali ambapo hukupanda.

Success is not an accident it's a result of deliberate efforts, kuishi kwa mazoea ni adui wa maendeleo, lazima uwe na kitu kinachokufanya uamke asubuhi ukiwa na shauku.
 
Je, mtu anaweza kuwa na amani bila matarajio?, au lazima mateso ndiyo yamsukume kuwa na malengo?
Mtu anaweza kuwa na amani hata bila matarajio, lakini amani ya kweli huwa haitokani na kutokuwepo kwa malengo, bali na kuwa na mwelekeo wa ndani unaoeleweka. Matarajio yenye afya hayaleti mateso -yanampa mtu sababu ya kusonga mbele na maana ya maisha. Ukikosa malengo, unaweza kuwa “poa” kwa muda, lakini ukosefu wa mwelekeo huanza kukula taratibu.
 
Mwelekeo wa ndani unaweza kuwepo bila kuchukua hatua yoyote?
 
Huwezi kuwa na expectations kama huna actions unazochukua.

Matarajio ni zao la uwekezaji wa nguvu au akili, huwezi kutegemea kuvuna mahali ambapo hukupanda.

Success is not an accident it's a result of deliberate efforts, kuishi kwa mazoea ni adui wa maendeleo, lazima uwe na kitu kinachokufanya uamke asubuhi ukiwa na shauku.
Wengi wanakubali hali zao mapema ndo maana inakua ngumu kupiga hatua, kuna muda inabidi ujikane
 
Kila kitu kinaanza na kujaribu, haijalishi utaanguka mara ngapi lakini kama ujafanya majaribio - uko katika mwelekeo sahihi
Mtu anaweza kujaribu tu bila hata kujua lengo lake linampeleka kwenye muelekeo sahihi?
 
Mtu anaweza kujaribu tu bila hata kujua lengo lake linampeleka kwenye muelekeo sahihi?
Takwimu zinaonyesha wapo walio wahi kujaribu bila kujua muelekeo na bado watatusua

Hujawahi kuona watu wanazamia kwenye meli lengo ni kufika nchi flani na huko anakofikia hana mwenyeji
Hata hapa Tanzania kuna watu wanatoka mkoa kuja kujaribu maisha hapa DSM na hawana ndugu, na kuna wengine Mungu anawafungulia milango ya baraka na wanafanikiwa
Ukisubiri muelekeo ndo uanze kujaribu basi ujue na wewe huna tofauti na mtu anayesubiri mazingira yaliyo tayari

Kusubiri muelekeo = Kupoteza muelekeo
 
Strategic or randomness?
 
Vipi kama tarajio ni kuishi bila ya matarajio? Hapo kutakuwa ni kupoteza mwelekeo wa akili?

Monks wanaishi maisha yasio na matarajio yoyote, na wengine huacha kabisa kuongea. Vipi, nao wamepoteza mwelekeo wa akili?
 
Back
Top Bottom