Umenena vizuri mkuu, alimwambia mama yake amtafutie shule ya private alizozoea, lakini kutokana na uchumi wa mama Huyo kuyumba Hana uwezo tena.
Kama mtoto wa rafiki nilianza kumkemea kuhusu kuwa na Huyo binti hata kabla ya kwenda shule muhula wa kwanza. Hata yule binti alijenga chuki na Mimi. Alipopewa fedha kwa ajili ya shule alibadilisha matumizi na kuondoka na Huyo binti na kumpangia nyumba mjini karibu na shule, huo ni mrejesho wa wanafunzi wenzake.
MY TAKE
Tuwe makini na shule tunazopeleka watoto wetu, kijana sass hivi makundi sanaaa, bange mbele maisha ya kibongo movie, yasiyoendana na maisha Halisi ya kipato cha wazazi wake
Kinachosikitisha zaidi Hana uelewa Kama yeye ni kidato cha tano kweli.
Kama wewe huwezi hurumia wazazi wako ambao wamekusomesha kwa kukopa na kujibana, nini uwezo wako wa kufikiri Kama kidato cha tano?
Miongoni wa washauri ukiachilia babake ni Mimi peke yake ndo Me, wengine wote ni KE marafiki wa mama yake.