Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,981
- 45,903
Watanzania tumekua tukiishi kwa muda mrefu sana kwa mazoea tu na kuziweka sheria na taratibu pembeni.
Maisha ya mazoea yanatokana na namna tulivyokuzwa toka utotoni katika hali ya kuishi kindugu na kirafiki, hili sana sana linatokana na aina ya maisha ambayo tulianza nayo ya " Ujamaa" ujamaa umetusogeza karibu sana kiasi kwamba, tumeamua kuwa ndugu mmoja, undugu huo umetufanya hata pale sheria inapotaka kuchukuliwa basi watu huamua kuiweka pembeni na kufuata taratibu nyingine ambazo zitachukuliwa.
Ujamaa huo ulirithishwa vibaya, nataka kusema ni vibaya kwa kua umepelekea kuzaliwa kwa uzembe, na sasa ufisadi.
Nchi nyingine kama China ambayo tulikopi siasa za kijamaa, wao wamerithi ujamaa katika mtazamo chanya kwani kila mali ya uma ina lindwa kizalendo, wananchi wamekua katika dhana kwamba mali ya uma ni mali yetu sote.
Uzembe uliozaa ufisadi kutokana na kutokufuata sheria, umeua kabisa uzalendo, na kuzaa ubinafsi.
Sasa awamu hii ya Tano imeamua kujikita katika kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa. Matamko ya Rais na watendaji wengine walioteuliwa naye yanalenga katika kuhakikisha kua sheria zilizopo zinafuatwa. Hakuna hata tamko moja lililotolewa mpaka sasa ambalo halitokani na sheria tulizojiwekea wenyewe.
Lakini matamko hayo yanaonekana kua ni kinyume cha utaratibu kwakua hatukuwahii kuamua kuzitumia sheria zetu, u ajabu wa hayo matamko unakuja kutokana na ugeni wetu katika kufuata taratibu kwani tulizoea tu kuishi kindugu, na kuamua kuacha kufuata sheria.
Tukikubali kufuata sheria, basi ni dhahiri kwamba uzembe utapungua, ufisadi utakosa nafasi na uzalendo utachukua nafasi yake.