Kuinyoisha hii nchi ni wapi palipopinda

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,011
2,165
Wafuasi na wanachama wa CCM unajua Mungu wetu muumba mbingu na nchi anawaona kwa huu unafiki wenu;

2005-2015 wapinzani wa CCM na wananchi wengine walikuwa wakipiga kelele za kusema kuna ufisadi, ubadhirifu, rushwa chini ya serikali ya CCM, lakini hawa wanachama, wafuasi wa CCM walisema siyo kweli, na wakasema hii ndiyo serikali bora kuwahi kutokea katika nchi ya Tanzania, yaani utawala wa awamu ya 4.., wakaenda mbali na kusema 'wapinzani' wanawaonea wivu!

2015/2016/2017 - wanachama wale wale wa CCM wanasahau yale ya 2005-2015 na kusema sasa hii ndiyo serikali bora kuliko zote kuwahi kutokea nchini.., wanasema sasa 'wanainyoosha nchi'.., nashindwa kuwaelewa hawa wakazi wa mtaa wa Lumumba.., Je, hii nchi nani aliipindisha, kwani imewahi kuongozwa/kutawaliwa na watu wengine zaidi yenu!? kwanini mnataka kuinyoosha wakati awali mlisema iko salama!?

..., nimeishia kukumbuka ile kauli ya Albert Einstein; "We can't solve problems by using the same kind of thinking we used when we created them."

TUENDELEE KUINYOOSHA NCHI....., SIJUI ILIPINDISHWA NA WAKOLONI KUTOKA JAMAICA..,
 
Back
Top Bottom