Goodluck Mshana
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 1,271
- 1,119
Kuendelea kuijadili CCM na matokeo yaliyompa Dr. Shein kuwa Raisi wa Zanzibar ni kuvunja katiba ya nchi. CCM walishakiuka misingi ya katiba ya nchi hii kwa kitendo kilichofanywa na Jecha. CCM walikibariki na hivyo uchaguzi ukarudiwa hiyo jana na kumtawaza mgombea wao mshindi.
CUF na UKAWA hawakushiriki wakiamini mgombea wao Maalim Seif alishinda uchaguzi wa 2015. Tafsiri ya haraka ni kwamba CUF hawakushiriki uchaguzi ulioitwa wa marudio wakiamini haki haikutendendeka. Na mimi naamini hivyo. Demokrasia ilibakwa na kuwekwa fungate. Lakini msingi wa hoja ni uvunjaji wa katiba na sheria ya uchaguzi wa nchi. Hivyo CUF hawakutaka kushiriki dhambi hiyo. Kiungwana kabisa wakajiweka pembeni kumpisha mwenye timu, kiwanja, filimbi, washangiliaji na mtoa kombe. Na amejitangaza. Ni Rais wa Zanzibar!
Sasa kuwaona watu wakiendelea kujadili uhuni huo mnakuwa washiriki na washirika wa kuvunja katiba ya nchi kama walivyofanya CCM. Wanachokivuna CCM ni kile walichokipanda cha kuvunja katiba na sheria ya uchaguzi. Wanavuna maamuzi ya Jecha. Wanavuna ukimya, upole ustaarabu na heshima kubwa iliyooneshwa na Maalim Seif. Wanavuna ukimya, upole na uvumilivu wa wazanzibari. Wanavuna busara za viongozi wa CUF na UKAWA.
Wote hao kama wangeamua wadai haki yao kwa utaratibu ule ule wa kuvunja katiba ya nchi na sheria za uchaguzi basi leo hii fukwe za bahari zingekuwa zimejaa miili ya watu. Miili ya kina mama, watoto, wazee huku mingi ikiwa ya vijana wenzangu ingekuwa ikielea kama magugu maji baharini. Tungepata kusikia idadi kubwa ya waandishi wa Habari waliotekwa na kupotea kabisa. Tungesikia matamko makali kutoka USA, EU, ASIA na machache kutoka EAC na SADC. Maana hawa wa mwisho ni washirika pia wa ubakaji wa demokrasia.
Sasa basi, tuwaache CCM wavune matunda yao kwa kumtawaza mwali wao. Tusiwe sehemu ya wavunja katiba. Tusitarajie fair play kutoka kwao. Tusitarajie huruma ya kupewa makamu wa kwanza wa Rais (M1R). Bali tuwapongeze wote walioisaidia Zanzibar kuwa na utulivu( sio amani) tunao ushuhudia sasa. Jeshi la polisi limechangia kwa kiasi flani utulivu huo. Maana nina hakika hakuna Jeshi liloweza nguvu ya umma pale umma unaposema IMETOSHA.
Waacheni CCM wale uzao na matunda waliyopanda. Msiwe sehemu ya matunda yao. Kwani kwa kufanya hivyo mnabariki uwovu na kuwa sehemu ya waovu. Hivyo kuwajadili tunakuwa sehemu ya wavunja katiba. Asanteni.
Na Goodluck Mshana