kuhusu vyandarua vyenye dawa

kuhusu vyandarua vyenye dawa

Complicator

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2013
Posts
2,208
Reaction score
3,609
Jana usiku nilisikia sauti ya mbu akiranaranda nje ya chandarua changu,ukichangia na ugumu wa maisha mwenzi huu January nikawaza jambo moja la kijinga hivi..

hivi vyandarua ambavyo serikali inagawa kwa wanafamilia walidai vina dawa,dawa yake haswa inafanya kazi gani..

inaua mbu?!!
mbona sijawahi amka asubuhi na kukuta maiti kadhaa za mbu waliokwishaaga dunia kisa dawa ya chandarua.

inawafukuza mbu!?
mbona wanakuweko nje wanapambana kuingia ndani wakunyonye damu!??,tena usiombe akukute mbu aliyehangaika kukupata.

tusaidiane jamani tutoane tongotongo.

dawa inafanya kazi gani!?
 
DAWA inakwisha. tatizo ukipewa HAWASEMI mana utakuta tayari imeisha nguvu
 
Dawa ina muda wake ikiisha inabidi iwekwe tena
 
Mbu wenzao huwa wanawabeba kwenda kuwazika kabla hakujakucha ndo mana huwaoni asubuhi.
Pia ukiona wanalia sana usiku jua wanaomboleza vifo vya wenzao......!!
 
then kuna mtu keshawahi kuiweka na kesho asubuhi akashihudia mbu wamekufa?!
 
Back
Top Bottom