Kuhusu Tanzania: Vitu 11 ambavyo vinaweza kukuacha mdomo wazi

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Karibuni wadau tuichambue hii TANZANIA yaani TANGANYIKA (TANGA (kitambaa kinachotumika kama Engine ya jahazi) + NYIKA yaani JAHAZI NYIKANI) na ZANZIBAR (Zengi(mtu mweusi) + Barr (pwani) yaani Mtu mweusi maeneo ya pwani)

ONGEZEA CHOCHOTE KATIKA LIST HII

1506_sisal3.jpg

1.Zao la katani/MKONGE(white gold) lilipandwa kwa mara ya kwanza Afrika nchini Tanzania. Lililetwa baada ya mjerumani researcher kuiba (alichukua kinyume na sheria) miche 1000 Mexico kuja TZ kupitia Hamburg ujerumani. Ilifika bandari ya tanga miche 63 tu mingine ilikufa njiani. Ndio chanzo cha katani afrika na kuifanya TZ duniani kuwa nchi ya pili nyuma ya Brazil kwa kuzalisha katani.
Google Books (history of sisal in Tanzania)
Cut-African-blackwood.jpg

2.Mti ghali na wenye thamani kabisa kuliko yote duniani MPIGO unapatikana Tanzania.
Tanzania-Flag.jpg

3. Wimbo wa taifa "Mungu ibariki afrika" ulikuwa ni wimbo wa Kizulu ".Nkosi sikelel' Afrika ". mwaka 1873 mwalimu Enock santonga wa africa kusini aliutunga. Lengo ilikuwa ni kutunga wimbo wa Shule aliyokuwa anafundisha. Leo hii tunauimba sio sisi tu bali S/Africa, Zimbabwe.
Coconut-crab.jpg

4.Kaa/Crab (coconut crab) mkubwa na mtamu kuliko wote (kwa mujibu wa walaji) dunia nzima anapatikana Tanzania maeneo ya Chumbe kisiwani zanzibar.
9754054.jpg
Chaga.jpg


5: Katika list ya makabila 10 Maarufu Afrika nzima, Wamasai ni wa pili na wachaga wanashikilia nafasi ya 10.
philipsk70.jpg

6: Zanzibar ndio ilikuwa ya sehemu ya kwanza kwanza bara lote la Africa kutumia TV zenye rangi kuanzia mwaka 1974.TV zote nilikuwa zinaonekana ktk Monitor/screen kwa black and white bila rangi nyingine.Pia mwaka huo Zanzibar TV station ilianzishwa na karume na inasadikiwa kwa gharama zaidi ya 24M, wakati Television station ya kwanza kwa bara ilianza mwaka 1994 sababu ya kucheleweshwa inasemekana ilikuwa ni kupingwa na mwalimu Nyerere na sera zake ujamaa.
barbaig.jpg

Wasandawe
1024px-Hadzabe_Hunters.jpg

Waadzabe
7:Kama ilivyo Marekani Wahindi wekundu, Makabila mawili Waadzabe na Wasandawe ndio wakazi halisi wa Tanzania. Wengine wote tulihamia miaka zaidi ya 2000 iliyopita. kuna tuliotoka Africa Magharibi (wabantu), Africa kusini, Kaskazini Sudan, Ethiopia na sehemu nyingine mbalimbali africa. Mfano Wadatoga na wengine Waarusha waliingia kutoka mipakani mwa Ethiopia na sudan kati ya miaka 2900 hadi 2400 iliyopita kutokana na ushahidi wa kiachiolojia. Tusibaguane tuwaheshimu hawa wadau wawili.
800px-Ngorongoro_Crater.jpg

8:Tofauti na nchi kama Israel au Libya ambapo jangwa ni asilimia kubwa sana nchi yetu tanzania ni ya 31 kwa ukubwa duniani. lakini 38% ya nchi au ardhi imetengwa kama hifadhi na haitumiki kwa uzalishaji isipokuwa utalii.
Kilimanjaro570Big.jpg

9:Tanzania ina sehemu mbili za muhimu katika jiografia ya africa. Point ndefu kabisa afrika ni mlima kimanjaro kileleni (yaani kama tukiiminya afrika na ukasimama kilimanjaro utaiona Afrika yote) na point ya chini kabisa ipo katikati ya ziwa Tanganyika. Mlima kilimanjaro mchakato wa kuanza kwake ulisababisha uwepo wa Ziwa Tanganyika, Edward na kivu.
800px-FIB-training-22_%289311333487%29.jpg

10:Kikosi maalumu cha wanajeshi wa tanzania kilichopo CONGO, kiliingizwa katika list ya SPECAIL FORCES bora kabisa (most elite) 35 duniani . list hii iliongozwa na US NAVY SEAL, Brittish SAS, HUNTMEN CORPS danish special forces.
irrigation-farmland.jpg

11: Kulingana na National Illigation MASTER plan ya 2002, eneo la kilimo hapa kwetu linalofaa kwa umwagiliaji ni HECTA MILLIONI 29.4, lakini eneo ambalo hadi june mwaka 2011 limekuwa likitumika kwa kilimo HIKI ni HECTA LAKI TATU ELFU KUMI NA MIASABA AROBAINI NA TANO sawa na asilimia 1.06.


UPDATES
stunted_photo_800x680.jpg

1:Zaidi ya 40% ya watanzania walidumaa utotoni. Mfano mtoto wa miaka 13 ana urefu na wa mtoto wa miaka 7. Hii haiathili Urefu tu na Uwezo wa ubongo unakuwa duni sana. sio kwa kukosa chakula bali kukosa virutubisho tangu mama zao walipokuwa na mimba hadi siku alipozaliwa mtoto mwingine.utafiti unaonyesha kudumaa huku kuko sambamba na udumaaji wa maendeleo ya taifa.
source:WHO children growth standards 2014.

tanzanites.jpg
tanzanite-rough.jpg

02:Tanzanite iligundulika TZ mwaka 1967. Dunia nzima inapatikana TZ tu. Mwaka 2002 American Germ Trade association waliingiza Tanzanite officially kwenye list ya Vito (birthstone) kwenye biashara zao.Ilivumbuliwa na mmsai mmoja mfugaji baada ya radi kusababisha moto porini, na kuona rangi ya zambarau ikingaa. Japo cha ajabu kwa kutaka kuficha ukweli duniani kuwa inatoka tanzania inatambulishwa kuwa inapatikana Afrika Mashariki.
Tanzanite - Facts, Lore, History, Myths and Pictures
676x380

3:Ni nchi ya tatu afrika kuwa na ngombe wengi, wapo karibu millioni 25 Na ni ya pili nyuma ya ethiopia kwa Mifugo barani afrika. Lakini kwa mwaka tunazalisha lita Billioni 2 za maziwa wakati majirani zetu kenya wenye ng'ombe chache sana wanazalisha lita Bilioni 2.4. pia Kiafya mtu mmoja inatakiwa kutumia lita 200 kwa mwaka lkn sisi tunatumia lita 43 wastani. Pia bado kwa mwaka mamilioni ya lita za maziwa huingia nchini kwa mwezi(kihalali).
source:Sekta ya maziwa na fursa chekwa za kiuchumi kwa Watanzania
Huge milk imports cause concern
 
halaf tunakimbilia mabasi yaendayo kasi bomba la gesi maghorofa posta daraja la kigamboni. Halaf nasikia wanataka kujenga daraja lingine kutoka selender hadi coco beach lingine eti kutoka Dar hadi zenji.

Sisi ni waajabu sana. Shame on us!
Nimeipenda sana comment yako Copenhagen. Nchi imekosa vipaumbele na inatenda kwa kujilinganisha na jirani anaishi vipi. Lakini mbaya zaidi,watanzania kwa ujumla wetu tumeamini kuwa Tanzania ni dar es salaam pekee ndio maana tunashabikia kujenga flyovers dar nzima bila kujali mkoa jirani hauna maji safi na salama.
 
Back
Top Bottom