Kuhusu mgogoro huu wa CUF, Bunge limekosa busara na weledi

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,291
Bunge ni chombo kikubwa katika nchi na ni sehemu ambayo hutumika kanuni na busara katika kuamua mambo yake. Mabunge mengi duniani hutumika kama nyenzo ya kutuliza hali pale inapochafuka hata pale muhimili mmoja unapochafua hali. Tumeshuhuidia busara ikitumika kwa kuielekeza serikali kutekeleza baadhi ya mambo ili tu kuondowa sintofahamu kwenye jamii ama baina ya serikali na wafanyakazi ama serikali na kundi fulani katika jamii.

Hili la mgogoro wa CUF bunge limetumika kufanya ushabiki sana na kukoleza moto. Wanajuwa kuna MGOGORO pale na kesi iko mahakamani hili wanalijuwa. Busara ingetumika kuhusu nafasi ya mgombea wa EALA kutoka CUF basi walau wangeiacha nafasi wazi mpaka mgogoro uamuliwe mahakamani.

Ilichokifanya Bunge letu la JMT kupitia Job ndugai na Kashilila ni kutaka kulidhalilisha Bunge letu mbele ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na tuonekane watanzania kuwa ni mbumbumbu. Hapana.

Tokea Mwanzo dalili zilishaonekana kuwakamia upinzani na kufanya siasa zisizo tija. Tunashindwa kujuwa wakati gani maslahi ya Taifa yatangulizwe mbele na wakati gani tufanye siasa. Ikiwa hapa Bunge linafanya zile siasa za kukomoana kwa wapinzani , wamesahau kuwa vyama hivi vina wanasheria weledi na yumkini suala litafika mahakama ya EAC. Itategemea maamuzi ya kisheria lakini naona tunaweeza kuadhirika kama taifa.

CUF inajulikana ilishamfukuza uanachama Habib Mnyaa tena kwa katiba ya CUF mamlaka hayo yako katika tawi lake huko mkanyageni Pemba. Na wala si CUF Taifa. Ikumbukwe pia kuwa Mnyaa alikuwa mwanaCHAMA WA KAWAIDA TU HAKUWA KIONGOZI AMBAYE TUNGESEMA YUKO KWENYE MGOGORO ULE ULIOPO WA KIUONGOZI. Hivi hili bunge letu hili wanalijuwa?

Kukimbilia kuwatambuwa eti wagombea wote wa CUF bila kusubiri kujuwa hatma ya maamuzi ya Mahakama ni kupoteza rasilimali na muda bure. Ikitokea kesi ya msingi ya mgogoro wa CUF ikaamua vyenginevyo dhidi ya Lipumba na genge lake bunge letu litasemaje kuhusu utoto huu waliofanya wa kukosa busara tena za kawaida?

Hawakumbuki kuwa ni juzi tu Mahakama imemzuiya Msajili kuwapa ruzuku CUF mpaka kesi ya msingi itakapoamuliwa iweje leo bunge lije likoleze mgogoro na kushindwa kutumia busara?

Tunawatakia kila la heri wateuliwa.

Kishada.
 
Bunge lenye wabunge chekechea !!!!!! Usitegemeee akili wala busara pale ndugu yangu nadhan ndio maana hata JPM amesha wadharau hawa viumbe
 
Tukose Uwakilishi Mpaka huo Mgogoro usiojulika utaisha lini ndio busara?

Na ingefanyika hivyo pia mngeuliza Bunge limetumia kanuni gani?
 
Yaani wewe unajifanya huelewi. Kesi iko mahakamani. Hili ni jambo kubwa litazame kwa makini. Mahakama ipewe nafasi hio ndio busara.
 
Hakuna Kesi ya uanachama wa Habib Mnyaa Mahakamani usiwe Mzushi!
 
Bunge ni chombo kikubwa katika nchi na ni sehemu ambayo hutumika kanuni na busara katika kuamua mambo yake. Mabunge mengi duniani hutumika kama nyenzo ya kutuliza hali pale inapochafuka hata pale muhimili mmoja unapochafua hali. Tumeshuhuidia busara ikitumika kwa kuielekeza serikali kutekeleza baadhi ya mambo ili tu kuondowa sintofahamu kwenye jamii ama baina ya serikali na wafanyakazi ama serikali na kundi fulani katika jamii.

Hili la mgogoro wa CUF bunge limetumika kufanya ushabiki sana na kukoleza moto. Wanajuwa kuna MGOGORO pale na kesi iko mahakamani hili wanalijuwa. Busara ingetumika kuhusu nafasi ya mgombea wa EALA kutoka CUF basi walau wangeiacha nafasi wazi mpaka mgogoro uamuliwe mahakamani.

Ilichokifanya Bunge letu la JMT kupitia Job ndugai na Kashilila ni kutaka kulidhalilisha Bunge letu mbele ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na tuonekane watanzania kuwa ni mbumbumbu. Hapana.

Tokea Mwanzo dalili zilishaonekana kuwakamia upinzani na kufanya siasa zisizo tija. Tunashindwa kujuwa wakati gani maslahi ya Taifa yatangulizwe mbele na wakati gani tufanye siasa. Ikiwa hapa Bunge linafanya zile siasa za kukomoana kwa wapinzani , wamesahau kuwa vyama hivi vina wanasheria weledi na yumkini suala litafika mahakama ya EAC. Itategemea maamuzi ya kisheria lakini naona tunaweeza kuadhirika kama taifa.

CUF inajulikana ilishamfukuza uanachama Habib Mnyaa tena kwa katiba ya CUF mamlaka hayo yako katika tawi lake huko mkanyageni Pemba. Na wala si CUF Taifa. Ikumbukwe pia kuwa Mnyaa alikuwa mwanaCHAMA WA KAWAIDA TU HAKUWA KIONGOZI AMBAYE TUNGESEMA YUKO KWENYE MGOGORO ULE ULIOPO WA KIUONGOZI. Hivi hili bunge letu hili wanalijuwa?

Kukimbilia kuwatambuwa eti wagombea wote wa CUF bila kusubiri kujuwa hatma ya maamuzi ya Mahakama ni kupoteza rasilimali na muda bure. Ikitokea kesi ya msingi ya mgogoro wa CUF ikaamua vyenginevyo dhidi ya Lipumba na genge lake bunge letu litasemaje kuhusu utoto huu waliofanya wa kukosa busara tena za kawaida?

Hawakumbuki kuwa ni juzi tu Mahakama imemzuiya Msajili kuwapa ruzuku CUF mpaka kesi ya msingi itakapoamuliwa iweje leo bunge lije likoleze mgogoro na kushindwa kutumia busara?

Tunawatakia kila la heri wateuliwa.

Kishada.

Acha kulialia mwanasheria wenuanajua mmeharibu sasa mkajipange na uchaguz 2022
 
Aliandika mkuu barafu jana mapema kabisaaa,kuwa kwa fitna hizi za CCM basi CUF ya Lipumba lazima ishinde

Kwenye mgogoro huu wa CUF kila aliyejificha atafichuka, taratibu mihimili miwili imedumbwikia (Serikali na Bunge)

tunaisubiri Mahakama ingawa Jaji Kihiyo na yeye ameshajidhihirisha. Nyuma ya mgogoro huu tutaona mengi.
 
Hakuna Kesi ya uanachama wa Habib Mnyaa Mahakamani usiwe Mzushi!

Pitia mada vizuri. Habib mnyaa ameshafukuzwa uanachama tawini kwake sio mwanachama huyo. Kupendekezwa na Lipumba na timu yake hakumfanyi awe mwanachama na tayari pingamizi lilishapelekwa BUNGE likakataa bila kujiridhisha.
 
Bunge na serikali wako bega kwa bega na lipumba lakini wananchi tunaona
 
sasa nimeanza kuamini Lipumba ni mwenyekiti halali ya CUF

Ungesubiri kwanza maamuzi ya mahakama. CUF kama taasisi ina KATIBA yake .tafsiri ya katiba ya CUF na uhalali wa lipumba utapatikana baada ya mahkama kutafsiri katiba hio. Hizi ni hilba za siasa.

Kwa mfano huoni tatizo msajili kumtambuwa Lipumba kama mwenyekiti lakini bodi ya wadhamini ya CUf na Baraza kuu la uongozi halimtambui. Nani mwenye haki kwa mujibu ya KATIBA YA CUF? Msajili au Bodi ?

tafakari.
 
Mkuu kwa mfumo wa Mahama zetu hiz lipumba lazima atahalalishwa tu

CUF ya Lipumba ipo pale kimkakati tu ni pandikzi
 
Nyie cuf tumieni akili. Mmemuabudu seif vya kutosha sana sasa mbadilike. Seif ameangamiza wanasiasa wengi sana wazuri kimizengwe kwa kulinda tumbo lake. Sasa ni zamu yake
 
Angalieni maslahi ya nchi sio maslahi ya seif. Cuf ni chama kizuri sana ila njaa zenu ndio zinaiua
 
Hakuna Kesi ya uanachama wa Habib Mnyaa Mahakamani usiwe Mzushi!
Ndugu yangu Pohamba, kama hakuna kesi ya uanachama wa Habi Mnyaa basi alishakubariana na maamuzi ya chama ya kuvuliwa uanachama, maana kama angalikuwa amepinga basi angeenda mahakamani.
 
Back
Top Bottom