Kuhusu Makamba, watanzania tutulie ukweli utajulikana

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,605
12,229
Nikiwa kama mtanzania mwenye haki yakuchangia mawazo yangu pasipo kumtukana mtu au kumkashifu, ningependa watanzania wote tulio na mapenzi mema na taifa hili tutulie na tusubiri maamuzi mazito ya serikali na chama cha mapinduzi ktk kushughulikia kashifa nzito inayo iliyomkumba Makamba.

Ukweli ni kwamba kile kimekuwa kinasemekana amekifanya Makamba hata viongozi wengine kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakikifanya japo tu hawajaamuliwa kuwekwa wazi ktk vyombo vya habari sema serikali kupiti idara zake imekuwa ikiwashughulikia kimya kimya.

Tuseme ukweli familia ya makamba sio mara ya kwanza kumulikwa kwa wale mnakumbuka hapo kipindi cha nyuma ilishawahi tokea skendo kaa hii ila ikazimwa kimya kimya kunusuru ofisi ya rais.

Ndugu zanguni, kwa wale wamekuwa wakifuwatilia maisha ya mwanasiasa huyu kijana sio kificho hana yale maadili ya kiuongozi na vyombo vyetu vya usalama vimekuwa vikimuanika mambo yake ya siri katika namna ambayo sio rahisi kwa mtu wa kawaida kujuwa nini serikali inakifanya.

Labda niwakumbushe ipo michoro aliweka wakati fulani kwenye profile zake ambayo ilizua maswali mengi ktk taifa. Je, nani aliwahi kujiuliza alikuwa anamanisha nini?

Ukweli ni kwamba kipo kitu Makamba alitegemea kukipata kwa namna moja au nyingine lakini hakukipata na hili limemfanya kuwa waziri amabaye mimi na wewe hatumuelewi.

Kwa mfano anakuwa akiongea kama msemaji wa chama tena issue ambazo yeye sidhani angepaswa kuziongea labada wazee wake na kwa kufanya hivyo amezua utata mkubwa ndani ya chama, mfano tu ile kauli ya siku za karibuni eti serikali iliopiata ilikuwa na mchezo wa kuleana.

Jamani nani ilikuwa inamlea kama sio yeye na team yake ya kudalali taifa letu.

Kauli hii naimani haikumfurahisha mtu kuanzaia state na vyombo vya usalama wa taifa.

Pia siku amabayo Rais alisema watu wapeleke form zao za maadili kabala ya saa kumi na mbili kesho yake kwenye gazeti la mwananchi Makamba alionekana kwenye ukurasa wa ndani yupo na balozi wa Kuweit, kwa wenye kutafsiri mambo hii inamanisha nini?

Ndugu watanzania na wanaccm embu tutulie tuone mwisho wa hii picha ambayo mchezeshaji ameamua kuicheza pamoja na anayechezeshwa.

Ukweli utajuikna pasipo chenga na kwa sisi tunaomuomba Mungu tuna imani mwisho wa kuitukana na kuzibeza serikali kwa vijana tunaoibukia unakuja.

Mwisho ushauri kwa vijana wote wa Tanzania tulio na mapenzi mema na taifa hili, ni wakati sasa wa kukaa na wazee wenu na kujifunza namna ya kuliongoza taifa na sio kuwatukana na kuwabeza watawala wakati tunaitaji kujifunza kutoka kwao.

Hili linanikumbusha jambo moja, kila uteuzi wa rais tunambeza huyo mteule ni mzee ni lazima tujuwe kuongoza taifa ni kazi inayohitaji hekima kubwa na sio umri wa mtu.

Leo Janaury angekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania tungejifunika usoni kwa shuka gani?

Ni wakati wa vijana kujifunza kutoka kwa wazee na Mungu siku moja atawapa kufika pale mnaitaji kufika.

Mungu ibariki Tanzania na viongozi wake wote.
 
Nimesoma kwa makini lakini sijaelewa kabisa, labda kwa sababu sijui mambo mengi kuhusu makama na tawala hizi mbili (awamu ya 4 & 5). Ume-assume kuwa kila mtu anaujua uovu/utata wa makamba, anyway...., asante kwa ushauri wako kwenye paragraph ya mwisho..

Kuhusu vile vikatuni havikuwa na maana mbaya...., in-fact vilikuwa na tafsiri nyingi sana
 
Shida unaitaja CCM sana... chama chako kimelinda sana wahuni wa kisiasa... everything in this world is about time, and i guess that time is now.
 
Ukweli umeshajulikana...all makambas wamekiri kupokea pesa kutoka kwa mwitaliano ili apewe dili na baadae wakamgeuka pamoja...walidhani ule uroda aliogawa dada mtu unatosha kutuliza mzuka wa muitaliano kumbe jamaa ni mzoefu wa michezo kama hii.
 
Acheni puuzi, baada ya makamba kusema serikali iliyopita ilijaa kulindana ndo anaanza kushughulikiwa kwa kashafsa ambazo hata kuzithibitisha Bado ni vigumu. Muacheni dogo janja apige kazi
 
Acheni puuzi, baada ya makamba kusema serikali iliyopita ilijaa kulindana ndo anaanza kushughulikiwa kwa kashafsa ambazo hata kuzithibitisha Bado ni vigumu. Muacheni dogo janja apige kazi
Ni kweli kabisa serikali iliyopita ilijaa kulindana... nae ni mmoja wapo aliyelindwa na JK
 
Back
Top Bottom