Fredinho
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 971
- 1,161
Jina kwa maana nyepesi ni neno au maneno yanayomtambulisha mtu au watu, mnyama,kitu au hata mahali,kila jina lina maana yake ambayo inatokana na asili ya lugha fulani.Yapo baadhi ya majina ambayo watoto wanapewa yana maana tata mfano mtoto anaitwa Mtumwa au Jalala.Haya ni majina pengine hayawapendezi watoto lakini wazazi wao wameamua waitwe hivyo.Majina ya namna hiyo yanaweza kusababisha mtoto anapokuwa darasani kwa mfano, apate usumbufu wa kutaniwa na wenzake na hata kujihisi vibaya anapokuwa shule.Hali hiyo inaweza kupelekea mtoto kuwa mnyonge pindi mwalimu akifundisha na kusababisha ashindwe kuelewa somo.Ni vizuri wazazi mkaliona hili na kujaribu kuwapa watoto majina yenye maana nzuri,hata watoto wakiitwa wajisikie fahari mbele ya wenzao.