Kuhusu Katiba Mpya, JK Atoe Tamko! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu Katiba Mpya, JK Atoe Tamko!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Buchanan, Dec 28, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tumeshuhudia kauli mbali mbali toka kwa viongozi wa Serikali kuhusu Katiba Mpya!

  1. Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani: "Hakuna umuhimu wa kuwapo katiba mpya na kwamba Serikali inaridhika na utaratibu uliopo wa kuifanyia katiba hiyo marekebisho ya mara kwa mara pindi umuhimu wa kufanya hivyo unapokuwapo. Alisema kuwa Serikali haiko tayari kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya kwa sababu wanaodai kuwapo kwa katiba hiyo hawajapeleka maombi yao serikalini kwa maandishi.

  Waziri Kombani alisema maombi hayo lazima yaainishe vifungu vya katiba ambavyo wanaona vina utata na wapendekeze vifungu mbadala, lakini alionya kwamba suala hilo lina gharama na sio kipaumbele cha Serikali wala wananchi."


  2. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda: "Isije watu wakadhani serikali ina kigugumizi; hapana. Sasa mjadala umeiva na ni vizuri lizungumzwe kwa utaratibu. Nipo tayari kuzungumza na rais. Nitamshauri mzee (rais) na nitaweka nguvu zangu huko... hilo halitawezekana tusipoweka ‘initiative' (juhudi)," alisema Pinda.

  "Watu wasifikiri wala kuona kuwa serikali haioni kama madai ya katiba mpya kuwa si ya msingi.
  "La pili, tunataka kuzungumza machache, lakini kubwa ni hili la katiba mpya. Kumekuwa na maelezo mengi, marefu, mjadala mkali;
  sasa hili nataka niseme tusione kama madai ya katiba si ya msingi sana; hapana. Ni ya msingi. Kwa serikali mabadiliko ya katiba ni utaratibu wa kawaida kwani ni jambo lililo ndani ya katiba," alisema Pinda.

  "'All along' Watanzania wameendelea kuibuka na kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Tulipofikia tunaulizana 'kuna ugumu gani kukaa na kuandika katiba mpya?"
  Aliongeza kusema: "Mimi binafsi sioni tatizo kwa hilo kufanyika, lakini kama serikali zipo namna mbili za kulishughulikia. Moja ni kutafuta utaratibu wa kumshauri rais aunde kamati ya watu wangalie maeneo gani ya kuingiza katika katiba hata ikibidi wananchi waulizwe yatoke ya kuwekwa mezani kwa kuhusisha vyama vya siasa na wanazuoni."
  Pinda aliitaja njia ya pili kuwa ni rais kuunda timu yake ya kiserikali itakayoangalia mapendekezo ya tume zilizoundwa awalikuangalia marekebisho ya katiba na kuchukua mapendekezo yaliyojirudia yatakayoonekana kufaa kuingia katika katiba.

  "Tume zote zina viporo vya kuanzia na kuchukua kuliko hali ilivyo sasa ambayo kila mmoja anasema lake kuhusu katiba," alisema Pinda.


  3. Mwanasheria Mkuu, Jaji Fredrich Werema: "Kuandika katiba mpya hapana, lakini kufanya marekebisho kwa kuondoa au kuongeza mambo fulani kwenye katiba ruksa," alisema Jaji Werema.

  "Suala la kubadilisha ibara zinazoonekana kutokidhi haja na kuingiza mambo mapya kwenye katiba, linakubalika na kwamba hayo yamekuwa yakifanyika," alisisitiza Jaji Werema na kutolea mfano mabadiliko ya katiba yaliyoruhusu kuingizwa kwa haki za binadamu.

  Hata hivyo, alisema maoni ya watu yanayotolewa kuhusu katiba mpya ni sahihi kwani kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa katiba iliyopo.

  "Raha yangu ni kuona Watanzania tunajadili suala hili maana kila mtu ana haki ya kusema na ni sahihi, lakini tunatofautiana tu kama kila maoni ni sawa," alisema Jaji Werema na kuongeza:

  "Lakini si kila mtu analolisema lifuatwe. Tukisema kila mtu anachokisema tukifuate haitakuwa sawa. Kwa mfano mimi kule kwetu wafugaji nao watataka mambo ya ng'ombe wao yaingizwe kwenye katiba, na Wahaya pia wanaweza kusema tuingize kwenye katiba ndizi zao, hii si sawa;" alisisitiza Jaji Werema.


  4. Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan: JAJI Mkuu anayemaliza muda wake, Agustino Ramadhan amezungumzia tena umuhimu wa kuandikwa kwa katiba mpya, safari hii akitaka uundwaji wake uharakishwe ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili nchi.

  Ramadhan alishawahi kukaririwa akisema kuwa suala la katiba mpya linazungumzika, akiungana na wanasiasa wa kada mbalimbali, wanasheria na wanaharakati ambao walieleza kuwa suala hilo sasa haliepukiki.

  Jana, Jaji Ramadhan, ambaye ameshamaliza muda wake, alikiambia Kituo cha Televisheni cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na katiba mpya. "Kuna umuhimu wa kubadilisha katiba ya nchi yetu ili kuondoa upungufu uliopo katika katiba ya sasa ambayo inalalamikiwa na wengi,|" alisema jaji Ramadhan.


  5........................

  Kombani na Werema wameongea kama watu wenye mandate ya mwisho ya kuzuia au kuruhusu Hatima ya Katiba Mpya Tanzania!

  Pamoja na hayo tumeona CUF wakitaka kuwasilisha Rasimu ya Katiba Mpya kwa maandamano na Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) kuwasilisha Hoja Binafsi kuhusu Mjadala wa Katiba Mpya Bungeni kwa mujibu wa Kanuni ya 55 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007.

  Mimi naona tu kwamba Rais Kikwete atoe tamko kwamba anakubali Katiba Mpya au la badala ya kuacha mambo yaende kama yalivyo huku Mawaziri wake wakitoa matamko ya kupinga suala hilo. Kama amewatuma yeye ieleweke wazi badala ya kukaa kimya kiasi hicho!
   
 2. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Katiba mpya haiepukiki....it's now or worse
   
Loading...