Mbishi 4 real
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 640
- 655
Kwanza napenda kuipongeza sekretarieti ya ajira kwa kuwasaidia vijana ( watoto wa wakulima ) kupata ajira serikalini sababu bila ya nyinyi hali ingekua ngumu sana kwa sisi walalahoi kupata ajira serikalini.Nasema hivyo kwasababu taasisi nyingi za serikalini zimejaa undugu kiasi kwamba huwezi kupata kazi bila ya kuwa na mtu unaemfahamu katika taasisi unayotaka kuomba kazi.
Sekretarieti ya ajira imekua na utaratibu wa kuendesha usaili kwa kada mbalimbali na wanaofaulu hupangiwa vituo vya kazi.Kwakua nafasi zinakua finyu wale ambao wamefaulu lakini hawakupangiwa vituo vya kazi majina yao huifadhiwa kwenye kanzidata (database) kama majina ya reserves(akiba).
Kitu ambacho nadhani wanachotakiwa kufanya ni kuweka hadharani majina ya waliopangiwa vituo vya kazi na vilevile waweke wazi majina ya wale ambao wameingia kwenye database ili nao wawe na matumaini flani hata kama ikitokea sio wote watakaopata nafasi lakini angalau wajue kwamba ni wangapi wameingia kwenye database.
Kwakumalizia napenda kuwapongeza kwa kuwasaidia watoto wa wakulima ambao hawana wa kuwashika mkono katika mchakato mzima wa kupata ajira serikalini.
Asante.