Kuhusu hili Please enlighten me.,

Kuhusu hili Please enlighten me.,

Character X

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
331
Reaction score
382
Ndugu zangu wa JF, Amani kwenu

nina andika hapa kwakua nina fahamu kabisa kwamba hapa nimahali palipo sheheni watu wenye nafasi nyingi kubwa katika taifa letu hili, lakini pia watu wenye experiences kubwa na ninazoweza kujifunza kwazo.,

ndugu zangu,
liko jambo katika tasnia ya siasa linalo nisumbua sana hasa ninapo pata majibu yanayo vunja moyo kidogo kutoka kwa watu wanje (wasio wanasiasa waowenyewe) nahivyo kunifanya nililete hapa nikiwa na mategemeo kwamba wale walio hasa wanasiasa waliopo humu watanipa First hand information katika hili katika ukweli na haki yote wakitumia mifano yao wenyewe au ya wanasiasa wanao fahamika kwa ukaribu kwao.

ndugu zangu,
yapo mengi tume sikia,. yapo mengi tume soma hata kutoka hapa hapa JF, matamko ya wanasiasa flani flani ya wazi., yaliyo onyesha kujihusisha moja kwa moja na practise ya USHIRIKINA. singependa kuongelea matamko hayo wala si nia yangu kuyazungumzia hayo per se

ila katika hali hii ya kiu yakutafuta kujua, Nimesoma vitabu vichache vya wana siasa wachache africa na duniani kwa ujumla, zikiwemo historia za maisha ya wachache kati yao (biographies), na katika mengi ambayo naendelea kujifunza katika nyanja zote kuanzia uongozi kwamaana ya leadership as a discipline kwenda kwenye maisha yao ya kawaida kabisa i.e traits and character zao, lipo jambo lilikamata attention yangu,

ofcourse, hii sio kwa wote!
nasio tu kutoka kwenye vitabu hivyo lakini pia kutokana na maneno ya kila siku yanayo zungumzwa na jamii yetu hapa, na watu wanao sema wanaijua siasa.

-USHIRIKINA!

neno hili linaweza kuwa na tafsiri nyepesi na tafsiri kali kuligana tu na msimamo wako. namaanisha, mtu mmoja anaweza kutafsiri suala kama kutambika katika makaburi ya wazee wake wazamani kama ushirikina na mwingine akasema lah, huo sio ushirikina ila ni mila tu ya kawaida.,

lakini hapa, na kwa madhumuni ya mjadala huu ninaomba tutumie msimamo uleninaoweza kuuita mkali., yani kwamba chochote kinachofanyika kwakutafuta kujiongezea nguvu kwakutafuta kujiunganisha na nguvu flani isiyo ya kawaida., (supernatural) ukiachilia mbali maombi ya kawaida kwa Mungu anae aminiwa na watu wote.
practise kama hiyo tuiite ushirikina. (kwa makusudi ya mjadala huu)

SWALI HASA,
ndugu zangu, swali langu hasa hapa ni je? ni kweli kwamba Ushirikina ni sehemu kubwa sana ya Siasa? na je? Mtu hawezi kuwa Mwanasiasa bila kuwa mshirikina?
je? ni kweli kwamba hakuna mwanasiasa yeyote anaye endelea kulipatia taifa lake mafanikio kwa michango yake bila kuwa MSHIRIKINA?

hapa, niombe tu majibu kutoka kwa watu wanaofanya siasa wao wenyewe au kwa wale wanaowafahamu wanasiasa kwa ukaribu sana (personal level). pia majibu haya ya unyeshe ukweli wote kwa kadri ya uelewa wa mchangiaji,

tafadhali, ninategemea majibu yenye kubeba hoja za nguvu, niwashukuru sana.,

comrades,
ni hayo,
 
Nakupa second hand info.

Katima maisha yoyote lazima uwe na drive zinazokupa nguvu
Mambo ya kiimani ni mojawapo ya drive kubwa sana sababu inamwezesha mtu kuvuka hata pale alipokuwa amekata a tamaa.

Sijui kwa nini umeondoa nafasi ya dini kujadiliwa hapa, lakini mie naona hata yenyewe ilifaa iwe hapa maana na yenyewe ni imani kama zilivyo zingine.

Nikirudi kwenye mada yako, kama katika maisha ya kawaida ya shuleni, kazini na kwingineko. Watu tunetoka kwenye backgroung tofauti, na pale unapopatwa na tatizo unajua wapi pa kupata msaada.

Siwezi kuongelea % za ushirikina katika siasa sababu sijui, lakini ushirikina kwenye siasa upo kama ulivyo mahali pengine, na sio wanasiasa wote wanashiriki ushirikina.
 
Nakupa second hand info.

Katima maisha yoyote lazima uwe na drive zinazokupa nguvu
Mambo ya kiimani ni mojawapo ya drive kubwa sana sababu inamwezesha mtu kuvuka hata pale alipokuwa amekata a tamaa.

Sijui kwa nini umeondoa nafasi ya dini kujadiliwa hapa, lakini mie naona hata yenyewe ilifaa iwe hapa maana na yenyewe ni imani kama zilivyo zingine.

Nikirudi kwenye mada yako, kama katika maisha ya kawaida ya shuleni, kazini na kwingineko. Watu tunetoka kwenye backgroung tofauti, na pale unapopatwa na tatizo unajua wapi pa kupata msaada.

Siwezi kuongelea % za ushirikina katika siasa sababu sijui, lakini ushirikina kwenye siasa upo kama ulivyo mahali pengine, na sio wanasiasa wote wanashiriki ushirikina.

POWERFUL,.!
Nashukuru sana., nadhani umefanikiwa kuni tazamisha kitu ambacho sikua nimekiona bado., asante nadhani hii inatoa base ya hoja kawujumla wake., na inatoa matumaini i must say ha ha.,
 
Back
Top Bottom