Kuhusu CV na PhD ya Dr. Slaa

Status
Not open for further replies.
Wanajamii forum.

Napenda kuwafahamisha kuwa jana nimepokea simu nyingi sana kwani kwa kula hali inaonekana mtpoa hoja/thread ameandika kwa nia ya kutaka kunivunjia mahusiano yangu na jamaa zangu huko Tanzania.

Hakika mimi niliweka hii CV kwa nia njema kabisa kama ambavyo ningeweka ya JK au hata Prof Lipumba au hata yangu mwenyewe kwa nia ya kuijadili na kutathimi mambo mbalimbali kama kiongozi wenu.

Kwa kukataa kuvunja mahusiano yangu na watu huko Tanzania na kuona thread hii haina tija kwangu wala kwa maslahi yoyote kwa jamii yoyote zaidi ya kujikita katika umbeye na uzandiki.

Naomba kusita hapa.

Adios
 
Nikupe pole wewe kwa imani yako ya ukanda na ukatoliki lkn nikwambie mimi kama mshabiki wa upinzani, mtu mwenye uelewa wa mambo yanayoendelea nchi ya Tz na hapendi ufisadi (sio mkiristo wala mkaskazini) basi atapenda Chadema. Madesa mliosoma kwa kificho kule mlimani kwenye nyumba ya ibada imewaharibu hata mlielimika mkabaki na inferior complex.
 

Sio lazima mtu mwenye Pd kuwa na masters.....nchi nyingi za continental europe kuna hata maprofesor wenye masters tu.....hivyo inategemea na mfumo wa elimu wa eneo husika.
 
Mwenye wasi wasi na elimu ya Dr. Slaa afuatilie kwa karibu wale vijana wanaotoka Seminari za kikatoliki (maana siku hizi seminary ziko nyingi) na kujiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Sheria. Wengi wao wanaishia kupata first class au second class upper. Na wengi ninaowajua mimi wamebaki pake kuwa waalimu au wamekuwa mawakili na majaji wazuri sana huko mitaani. Ni kwa sababu ya elimu yao wanayopata kule seminary. Inawapa foundation nzuri. Hata elimu ya kawaida ya sekondary bado tunaona Seminary za kikatoliki ndiyo kinara wa wanafunzi wanaofaulu vizuri. Seminary hizi nyingi zinaongozwa na kuhudumiwa na watu wenye elimu aliyopata Dr. Slaa. Hakuna cha ajabu wala cha kushangaza. Dr. Slaa ana uwezo mkubwa na elimu yake haina walakini. PhD yake siyo ya kuokota kama baadhi ya PhD tunazozijua humo kwenye system ya wanasiasa wa Kitanzania. Wengine tumewaandikia thesis zao waka-submit vyuo uchwara vya nje waambiwa wamepata PhD. Sitaki kuwataja majina lakini list yao ni ndefu!!
 

Mimi nilimfanyia interview wakati ule wa kampeni za uchaguzi 2010. Kwa kweli Dr Slaa ni encyclopedia. Mwulize swali lolote atakujibu kwa ufasaha bila kubabaika na hahitaji kujiandaa ili akujibu. Kama halina logic, atasema swali lako linajichanganya na ataonesha kujichanganya kwenyewe. Hata hivyo atakujibu tu kwa kile ulichouliza. Dr Slaa ni kichwa! Actually, graduates wa St Urban University au Louvain University si mchezo. Na ili uchaguliwe kuwa Katibu Mkuu TEC lazima ziwe zinacharge kwelikweli na Dr Slaa ni mmojawapo!
 
Why ar u discusing a people hu ar enjoyng lfe wakati wewe unapigika? Uar ol out of ua brains!dscu abt uar future u people hu dnt focus away!
 

Wewe ndio hufahamu hicho unachokiandika, ngoja nikupe shule kidogo.

Kabla ya Bologna process (Bologna declaration) ambayo ilikubaliwa tarehe 19 June 1999, nchi nyingi za ulaya zilikuwa zinatumia mfumo wa 2-cycle system. Yaani unaenda chuo kikuu kusoma unahitimu kwa kupata shahada ya uzamili (Masters degree0 moja kwa moja. Program za aina hii zilikuwepo huko ujerumani, Poland, Itally, Hungary, n.k.


Mfumo huo wa elimu sio kwamba ulikuwa inferior, la. ila ulikuwa una unganisha masomo katika level zote na unagraduate with master (Muda wa masomo ilikuwa miaka 5 hadi 7 kutegemeana na aina ya course). Mfumo huu ulikuwa na tatizo moja, kila nchi ilikuwa na mfumo wake wa grading, hivyo kutathmini na kuhamisha credit kutoka chuo kimoja au nchi na nchi ikwa ni kugumu sana.

Hivyo ikaamuliwa na kukubalika kuwe na mfumo mmoja wa elimu kwa nchi wanachama wa jumuia ya ulaya (euro zone). Hadi sasa nchi 47 zimejiunga na mfumo huu unaoitwa European Credit Transfer System, na unafuata mfumo mpya wa 3 - cycle (BSc./MA -->MSc./MA-->PhD)

Kwa mfumo wa zamani usishangae mtu wa masters aliyesoma ujeruman alipewa Master Diploma Certificate. Hivyo ndivyo ilikuwa inajulikana kwa mfumo wa elimu yao.

Wewe usilinganishe mfumo huo wa elimu ya wakati huo ukadhani ni diploma kama za tanzania.

Baada ya Bologna process kuanzia 1999, nchi nyingi karibia 47 za ulaya zilianza kufanya mabadilko ya mfumo wa elimu kwa kufuata mfumo wa 3-cycle yaani Undergraduate|Masters|PhD (3-5 years|1-2years|3years.

Na pia kuanzisha program nyingi kwa lugha ya kiingereza ili kuvutia wanafunzi wengi kutoka nje ya ulaya hasa wanaotumia lugha ya kiingereza katika elimu ya chuo kikuu.

Unachoshangaa ni kwa kuwa hukuwa na uelewa huu.

Think again.
 

Hapo kwenye bluu, kwa mtazamo wa watu wanaodhihaki PhD ya kusomea ya Dr. Slaa ni kwamba U-profesa na u-Dr. wa Prof. Juma Mikidadi au Ibrahim Juma waliobodea katika sheria za Kiislamu U-profesa na U-Dr. wao ni feki au nusu, siyo?
 

Hapo kwenye nyekundu, hisia siyo hali halisi. Lengo la threadi hii ilikuwa na itakuwa kueleweshana. Sijui ni kitu gani kinafichwa katika kutoa majibu ya maswali yaliyoulizwa katika threadi hii.

Pia sifahamu ni kwa namna gani kujibu maswali 1. na 2. au yote manne ni tatizo, kwanza Slaa ni kati ya wanajamii wa Tanzania. Nlidhani njia sahihi ya kupata suluhisho kwa dhihaka ya PhD ya kusomea ya Dr. Slaa ni kupata majibu ya maswali hayo. Kama hakuna majibu sijui ni kwa nini dhihaka hiyo iendelee.
 

Kwa baadhi ya wachangiaji humu, ninaona kabisa kile ninachokiita 'intellectual masturbation'. Mtu anpoleta hoja bila kujua ni kitu gani anataka kijadiliwe au kwa kuhisi "kama wangekuwa Wakristo au Wakatoliki wangesemaje?" Unaona kabisa yuko offpoint. Kwani Wakristo au Wakatoliki siyo Watanzania? Je, mtu aliyewahi kuwa sheikh, pastor, traditional priest, guru...nk

Kama ana sifa za kuwa kiongozi na anakidhi vigezo vya kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa mujibu wa Katiba, asiweze kugombea on grounds za kuwahi kuwa sheikh, pastor, traditional priest, guru? Mimi naona ndani ya mijadala kama hii kumejificha JINI baya sana la UDINI.

Na ndiyo maana wakati wa kampeni kulizuka madai "Dr Slaa kapora mke wa mtu" na baada ya uchaguzi hilo jini pia limetoka. Sasa limekuja hili la PhD ya Dr Slaa. This is pure intellectual masturbation!
 

Hakuna point yoyote hapa! Mwalimu Nyerere alisema: "Huwezi kuniua kwa nia njema halafu useme hujaniua. Umeniua!" Hata wewe huwezi kuweka post ya kueneza udini na useme umeiweka kwa nia njema. Ulijua na bado unajua lengo lako lilikuwa nini na umefanikiwa kupandikiza ulichokitaka kwenye 'mindset' ya baadhi ya Watanzania wenye mlengo kama wako. Jifunze: "Mchuma janga hula na wakwao." The sin you've created will start eating you!
 

You are in a cage! Tembea vyuo vya nje ndio utaona kinachoongelewa hapa. Kuna mifumo mingi ya elimu duniani. Nikupe mfano mdogo: Elimu ya msingi Malawi ni miaka 8. Elimu ya sekondari miaka 4 (Form I-IV). Kutoka hapo mtu anajiunga chuo Kikuu. Elimu ya msingi Tanzania ni miaka 7, ya sekondari ni miaka 6 (Form i-VI). Na kutoka hapo mtu anajiunga Chuo Kikuu.

Mimi nilisoma kwenye chuo ambacho kilikuwa kinachukua wanafunzi kutoka Malawi (Form IV), Tanzania (Form VI), Kenya (Form VI), Uganda (Form VI) na Zambia (Form IV). Ukiangalia wale wenye Form IV, utadhani unawazidi kwa vile mfumo wao wa elimu ni miaka 4 lakini content ya mfumo wao wa elimu ni kwamba kwa baadhi ya masomo tunayojifunza sekondari wao wanajifunza shule ya msingi na vilevile mkianza chuo kwa pamoja utakuta kuwa hakuna tofauti kati ya mwenye Form IV na VI.

Sasa kwa kuwa na mfumo tofauti wa elimu huwezi kusema mfumo wako ndio bora zaidi kuliko mifumo mingine. Jamani tuelemike! Hoja zetu nyingi hapa zinaonesha hamna shule kwa baadhi ya wachangiaji ingawa watu wana elimu ya chuo!
 
Mwisho sasa mtasema waliosoma shule za seminari hawana elimu ya sekondari, wakati kila siku ndio wanaoongoza kwa ufaulu.
 
Wana Jf tunamaliza time kudiscuss thread kama hizi posted by EDUCATED BARBARIAN' sijui rubaruba shame on u.!
 

Kitu ambacho wachangiaji wengi hawajui ni kwamba, wanadhani mtu akimaliza falsafa au teolojia anakuwa tu amejifunza Biblia au sheria za Kanisa wakati mfumo wa elimu ya Kanisa Katoliki ni kumfanya mhitimu wa masomo hayo awe 'competent' katika kukabiliana na mahitaji ya jamii. Ndiyo maana mfumo wao wa elimu basically unahusu maisha ya jamii katika ukamilifu wake kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

Kwa hiyo, padre anakuwa amesomea mambo yote yanayomhusu mwanadamu katika ukamilifu wake. pengine, mfumo huu ni tofauti na ule unaofundishwa katika dini ya Kiislamu.

Theology imeganwanyika katika nyanja mbalimbali - kuna political theology (studying theology in line with policitcs), environmental (eco) theology (studying theology in line with the einvironment), economic theology (studying theology in line with economic trends), moral theology (studying theology in line moral principles + dilemmas) etc.
 
Ni vizuri watu wakaongea kwa kufanya utafiti,kwa waliosoma FTC ie Full Technician Certifictate miaka ya nyuma au waliosoma ufundi katika vyuo kama dar tech kwa sasa kinaitwa DIT.

Arusha Techincal na Mbeya Technical hili si suala la kushangaza, kuna VICHWA vya maana ambavyo vimeweza kufanya mambo ya maana sana blia kusoma first degree mfano Dr Richard Masika,ambaye aliwahi kuwa Director of Studies wa DIT ie Dar Tech na sasa ni Principal wa Arusha Technical College.

Masika alisoma Msc baada ya kumaliza FTC,na amefanya vitu vizuri sana. Kwa tuliosoma ufundi ie FTC hili si jambo la kushangaza hasa kwa wateule kama Masika na walimu wengine wa *Ufundi.

Pia naomba watu waelewe,klia taasisi ina mfumo wake wa elimu,Leo hii ukistoka KIDATO CHA SITA UKITAKA KUSOMA DEGREE YA UHANDISI DIT LAZIMA USOME MIAKA MINNE,WAKATI MTU ALIYESOMA DIPLOMA AU FTC ANASOMA MIAKA MITATU. Hivyo inategemea na wwe mwenyewe unataka kusoma wapi!

 

Hiyo Kijiproma kwenye red maana yake nini? Yaani credibility ya mchango wako haipo na unaonyesha ni jinsi gani hata wewe ulivo mchakachuaji.
 
Wana Jf tunamaliza time kudiscuss thread kama hizi posted by EDUCATED BARBARIAN' sijui rubaruba shame on u.!

Alexism, unajua suala la PhD ya Dr. Slaa nimekuwa linarudiwa sana. Ndiyo maana ilikuwa ni muhimu kuuliza maswali yale manne. Inaonekana wanaotoa dhihaka wameamua kukacha kutoa majibu kwa sababu wanazozijua wao wenyewe. Kwa hiyo wale wanaohoji kisomo chake watasaidie kupata majibu manne yaliyoulizwa hapo juu. Tulia mwananchi usijali.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…