Kuhusu China, Correct Me If Am Wrong

Bandari hii ni muhimu kwa mstakali wa nchi yetu.Cha msingi mikataba isimamiwe vizuri ili vizazi vijavyo visije kutulaumu.Bandari zingine ndogo ndogo nazo ziendelezwe kuweza kusaidiaana na bandari kubwa katika kuleta ufanisi.
Nasisitiza watanzania wasomeshwe kwenye fani zinazohusiana na uwekezaji mkubwa tusije kuishia kuwa vibarua na kutoa mwanya kwa wageni kukamata ajira nyingi.
Kwa kuanzia Serikali ianze kutoa mikopo ya elimu kwa baadhi ya vyuo vya nje kwa vijana wa Kitanzania ili wajiandae kukamata ajira na kuwa wakufunzi kwa vyuo vya hapa nchini ili elimu hiyo ipatikane hapa nchini kwa urahisi na vijana wengi wapate taaluma muhimu kwa ajira zitakazo kuwepo.
 
 
Simply namuunga JK mkono kwa hili la kushirikiana na wachina! Tulipotoka hapo nyuma, hasa Mkapa aliamua kuegemea upande wa magharibi! uchafu mwingi unaomtesa JK uliasisiwa na Mkapa... Kenya wamepiga hatua ya haraka baada ya Kibaki kuwatamkia "no more west! we are turning east now!" ndo maana wanahaha kuhakikisha Raila anaingia madarakani...Wazungu ni wanyonyaji in the name of Demokracy...Bora wachina ambao siku zote wako kwenye win win ...
 
Jamani Mbona tunadanganywa na misaada ya US/UK na UE yenye kudharirisha utu wetu na masharti ya mashoga! leo hii tunajiuliza kwanini CHINA waisimamie mradi huu kwa kuleta menejiment yao ebu tujiulize menejiment za MIGODINI ni wazungu wa TZ ndo wanaoongoza au? Hivi tujiulize mikataba ya madini tena yanayochimbwa na kuisha ni ya miaka mingap 99 au 100? Bandari its a big deal huwezi compare na mikataba ya madini hata chembe! Tusidanganywe na US/Uk/UE the new world order is coming soon
 
Jamani, hivi baada ya hiyo miaka hamsini bandari itakuwa bado iko imara kwa maana ya miundo mbinu yake (majengo na magati)?
Naamini kwa umuhimu kwa nchi saba zinazoitegemea na ukubwa wa hiyo bandari, miaka 20 inatosha kabisa kwa Wachina kurejesha mtaji na faida ili tupate angalau miaka 20 ya sisi kupata faida ya moja kwa moja kabla span life ya majengo na magati haijaisha.
 
1) Naona wachina wanapigwa madongo juu ya hii mikataba, kwani ni Tanzania au China ndio wameinitiate ujenzi wa hiyo bandari?
2) Wachina wanajua udhaifu wetu katika kusimamia miradi, wametupa TAZARA- imetushinda, Kiwira-imetushinda, Urafiki-imetushinda, Mang'ula machine tools-imetushinda, magari ya nyumbu-imetushinda, Uwanja wa taifa-SIJUI...sasa bado unataka mtu akujengee port kwa mabilioni then alale mbele, ili umlete TASCAN na mikataba yake. Kwanza akiwapa tu after 2yrs utasikia tu matatizo harafu hiyo hela yake mturudisha vipi?....also know that, there is no free lunch nowadays.....kama unamashaka na mtu jenga mwenyewe.
 

mimi si mjuzi wa mambo ya mikataba ila hapo penye red kidogo pamenitia moyo, ila maelezo yaliyofuatia yananikumbusha machungu ya mkataba wa Buzwagi, baada ya kusaini walikuja na mlolongo wa faida zitakazopatikana na loyalty etc lakini mpaka leo ni maumivu tu.
 
Haya na mikataba mingine iliyosainiwa ni ipi? maana wengine tunasikia tu mikaba mingi imesainiwa...
nchi hii!!!!
 
Serikali ingeiweka mikataba hii wazi ingekua vyema sana kuisoma.
 
Ingawa sijafika mwisho wa uzi wako hapa kwa mkataba huu wa miaka 50 sijui kuendesha bandari itakuwa kama migodi wanachimba masaa 24 ila mwisho wa siku wanasema hakuna faida hii bandar kwa upande wa china kuiendesha mwisho wa siku wataichukua yote kabisa mana lazima deni wanalo dai litakuwa lipo juu tushindwe kulipa waombe bandar tuwaachie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…