Habari wana Jf?
Kuna professionals wanafanya kazi kwenye private sectors ambazo ni "Profit seekers" na ni taasisi au makampuni makubwa tu. Lakini waajiriwa wao ambao si vibarua bali ni professionals hawana mikataba ya kazi. Yaani ukimuuliza mtu mkataba wako unasemaje hana la kusema.
Pia pamoja na kwamba taasisi au makampuni hayo ni makubwa, wafanyakazi wake hawana bima za afya. Ukiugua au hata kupata ajali utajijua mwenyewe.
Sasa naomba kufahamishwa, je?
1. Hitaji la bima za afya kwa wafanyakazi ni takwa la kisheria au ni huruma ya mwajiri?
2. Hitaji la mikataba (writen ) ni hitaji la kisheria pia au mwajiri anaruhusiwa kufanya lolote analojiskia?
3. Kama hitaji la mkataba ni juu mwajiri kuamua kumpa au kumyima mfanyakazi, anawezaje kumwajibisha mfanyakazi kwamba hajafanya wajibu wake?. Maana kadiri ya ufahamu wangu ni kwamba majukumu ya mfanyakazi uainishwa katika mkataba.
Asanteni,, karibuni tupeane ujuzi na maarifa.
~JODEO~