Helicobacter pylori
JF-Expert Member
- Feb 15, 2013
- 430
- 287
Habari zenu wadau, Samahani sana wadau wa elimu, Nina mdogo wangu kachaguliwa kujiunga na Astashahada (Certificate) ya Sheria katika Chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDSM) Kupitia NACTE, Kwenye anwani (Account) Ya NACTE wamemuandikia, Uteuzi wake unategemea udhibitisho kutoka chuoni(UDSM), Ila mpaka sasa bado hawajamtumia kiambatanisho chochote cha kujiunga na tayari wameshatoa siku ya wanafunzi wapya kufika chuoni (08/10/2016) , Pia wametoa tangazo katika tovuti yao(UDSM) kua barua za kujiunga zitatolewa kuanzia tarehe hiyo kwa wanafunzi wa mikoani na huyu kijana ni moja ya wanafunzi hao, yupo Mwanza. Nimepekua katika tovuti yao sijaona majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na mafunzo kwa ngazi ya Astashahada na Stashada bali tu wa Shahada waliochaguliwa kupitia mfumo wa TCU na pia hawajaonysha katika tovuti yao Mafunzo (Program) katika ngazi hizo tajwa. kwa wale wanaofahamu utaratibu wa chuoni hapo jinsi ya kujiunga na kuhakiki uteuzi wa mwanafunzi husika naombeni msaada wenu kwa maana siku zinajongea na tunatakiwa kujua ni kiasi gani cha pesa kinachoitajika kabla kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya chuoni hapo.