NCHAGWA JOSEPH
JF-Expert Member
- Sep 15, 2014
- 802
- 226
Ni aibu kuonataifa la kidemokrasia kama Tanzania kuanza Kuhujumu watanzania kupata habari za wale waliowatuma kuwawakilisha. Matangazo ya bunge ni kioo cha kutuonesha kama kweli wanatimiza wajibu wao au wameenda kulala ili kufanya maaumzi tena ya kuwachagua au la. Ajabu ninaiona ni kwa wabunge wa ccm kudhana kuwa kuruhusu matangazo ni kuwajenga wapinzani na kuwapa umaarufu. Swali ni hili, je ninyi wanaccm ninani aliyewazuia kutafuta ummarufu kwa mambo mema?. Kama huhitaji umaarufu kwa mema wewe ni wakala wa yule mwovu. Leo kunawachezaji wazuri wa mpira tunawajua kwa uhodari wao wa kucheza mpira, iweje leo ninyi kuficha mema yanayotendeka bungeni?.
Kumbuka mema yote mnayoweza kuyatenda kwa mwaka mmoja yaweza kufutika ndani ya siku moja. Gadafi alitenda mema lakini wanadamu walimgeuka kwa dakika na sekunde kana kwamba hajatenda mema. Kosa lake kubwa lilikuwa ni kuhujumu haki ya waliowachache bila kujua kuwa wao pia walistahili heshima na haki.
Ogopa sana Mtu kama nape anayefanya maamuzi yasiyo na maslahi kwa taifa. Lazima ajue kuwa ni kupitia bunge watanzania waliweza kujua uovu wa watu wachache walioliibia Taifa letu. Leo hata mtoto mdogo anajua kuwa kulikuwa na ufisadi wa mali za umma.
Nape anapaswa kujua kuwa utawala wake ni wa miaka mitano tu na baadae watanzania watafanya maamuzi tena.Kama hukuwatendea haki watakuhukumu tu. Na ndipo huja majuto kwa kiburi cha madaraka kilichokosa maamuzi sahihi na busara kwa masilahi ya Taifa la Tanzania.