Rosh Hashannah
JF-Expert Member
- Sep 13, 2017
- 3,415
- 2,043
(sehemu I)
Ni vitu gani hivi? Hivi si vitu bali virusi vya ajabu vinavyoupelekesha Ukristo katika karne hii na mwongo huu. Usihangaike nitakueleza nawe utavitambua kwa wepesi wa macho ya nyama. Wala hakutahitajika darubini kali kuvibaini. Punde tu utavielewa kikamilifu kabisa. Kama unavyo mwenyewe utatambua dalili ulizonazo, matatizo yatabaki mawili tu, dawa ya kujiponyea na kinga ya kuwakingia waamini wanaochipukia. Zaidi ya hayo, virusi hivyo vitabainika vyema kwa vile unawafahamu sana wahusika wa Kibiblia: Haruni, Gehazi, Yuda Iskariote, Simoni mcheza mazingaombwe na malkia Yezebeli. Kwa mada hii napenda kukusomesheni na kukutafakarisheni Kut 32:1-35, 2Fal 5:1-27, Lk 22:1-6, Mdo 8:9-25 na 1Fal 21:1-29 mtawalia.
Kut 32:1-35 ni kisa cha uasi wa Israeli kwa ndama wa dhahabu. 2Fal 5:1-27 ni kisa cha Naamani na zawadi zake nono. Luka 22:1-6 ni kisa cha usaliti wa Yuda Iskariote. Mdo 8:9-25 ni kisa cha Simoni mcheza mazingaombwe. 1Fal 21:1-29 ni kisa cha malkia Yezebeli kumuua Nabothi kwa ajili ya shamba lake dogo la mizabibu.
Nivumilie. Makosa waliyotenda watu hao ndio nitakayoyaongelea kama virusi vinavyoupelekesha Ukristo leo. Si jambo la bure mifano ya kushangaza kuripotiwa kwenye Biblia. Kila kitu ndani ya Biblia kimekusudiwa kisomwe kwa nia maalum. Mungu wetu si chizi eti afanye kitu kisicho na lengo takatifu. Makosa ya watu wa kale yaliandikwa yawe masomo kwetu kusudi tusitumbukie katika makosa ya aina hiyo hiyo (1Kor 10:8). Kumbe, tufumbuane macho ili tusiangamie kiholela. Kama tumepatwa na virusi hivyo, tujisahihishe haraka. Nawaombeni sana katika mambo ya dhambi tuitangulize alahaula. Basi, twende hatua kwa hatua.
Kuharunika
Katika simulizi la ndama wa dhababu, mhusika mkuu ni Haruni aliyeshikilia ukubwa pale Musa alipokwenda kuonana na Mungu mlimani. Jambo hili limeelezwa vizuri katika Kut 32:1-35. Tunasimuliwa, Waisraeli walipoona Musa anakawia kurudi walimshawishi Haruni awatengenezee Mungu wa kumwabudu. Pasipo kupima mambo na kusali, Haruni akakubali kichwa kichwa tu. Akaitisha vikuku vya akina mama akaviyeyusha na kuwatengenezea watu ndama wa dhahabu na kuwaruhusu waiserebukie na kuiabudu kama Mungu wao. Mkasa huu wa mtu mkubwa kufanyizwa kosa kutokana na kuelekezwa na anaowaongoza ndiyo kirusi ninachokiita kuharunika.
Haruni alipaswa kuangalia akili ya kuambiwa angechanganya na yake, yaani alipaswa apime vizuri alichopendekezewa na anaowaongoza. Yeye hakufanya hivyo, badala ya kuongoza aliongozwa. Kama kiongozi wa kiroho alipaswa kumuuliza Mungu afanye nini hapo kwa sababu alitanzika. Ilimpasa asali kusudi awajibu na kuwaelekeza watu inavyotakiwa. Kinyume chake, hakufikiri kwa kujitegemea, hakumuuliza Mungu wala hakusali akakurupuka kufuata matakwa ya watu waliompa pendekezo la nini afanye. Narudia. Kutokupima mambo hivyo na kukubali kufanya alichopendekezewa tu ndiko ninakokuita kuharunika. Haruni aliharunika.
Musa aliporudi kutoka mlimani na kumkuta Haruni ameharibu mambo alishangaa mno. Kweli aliyakuta mambo yameharibika kwa watu kumwacha Mungu wa kweli na kuserebukia na kuiabudu ndama wa dhahabu alimuuliza Haruni swali gumu: “Watu hawa wamekufanya nini hata ukaleta dhambi kuu hii juu yao?” Kwa maneno mengine swali hili lilikuwa, “Kaka Haruni watu hawa wamefauluje kukudanganya wewe kiongozi mzima hata wewe kufanya walivyotaka wao badala ya wewe kusali na kujipatia jawabu zuri la kiroho hata kuwasaidia kubaki na imani ya kweli? Wamekulisha nini au wamekupa nini hata ukasahau nafasi yako ya uongozi?
Kifupi, kwa swali hilo Haruni hakuwa na jibu lenye mashiko bali alijikanyagakanyaga tu. Jibu lake lilionesha utoto wake mwenyewe. Alisema, “Hasira ya bwana wangu isiwake: wewe unawajua watu hawa, ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya. Maana waliniambia, ‘Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.’ Nikawaambia, ‘Mtu yeyote aliye na dhahabu na aivunje,’ basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu.” Kwa jibu hili, Haruni hakusema lolote isipokuwa kujisema kwamba alikuwa mpumbavu mkubwa. Alizungukazunguka tu akiona aibu kukiri ujinga wake mwenyewe.
Tusemeje sasa? Tuseme ifuatavyo: Leo hii WAKLERI KADHAA wameharunika. Walei wanasema hivi nao wanafanya tu. Akili ya kuambiwa hawachanganyi na yao. Ndipo wanachukua vikuku vya wanawake, ndiyo pesa, na kutengeneza ndama wa dhahabu wanaoabudiwa na watu siku hizi.
Walei wamewaambia, “Tuna laana tufanyieni ibada za kuvunja miti ya ukoo na kutuondolea laana,” wakleri wamekubali wanafanya kama walivyoambiwa. Wameharunika na kusahau kabisa kwamba habari za kulaaniwa kwa watu si mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Walei wamewaambia, “Tuna maradhi mengi tufanyieni makongamano ya maombezi na uponyaji, tupone kwa njia za mkato na fasta,” wakleri wamekubali wanafanya kama walivyoambiwa. Wameharunika na kusahau kabisa kwamba uponyaji haufanyiki kwa matamasha. Yesu, Bwana wetu, hakufanya hivyo na wala sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa haiendi kwa namna hiyo. Wamesahau kwamba kufanya miujiza kwa matamasha si mafundisho ya Kanisa Katoliki isipokuwa uongo wa makanisa “private” wanayopiga pesa za wajinga ndio walio kwa kuwafanyia miujiza ya kisanii.
Wamesahau wamisionari walipotukuta na maradhi walikazana kujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali, kinyume chao, wakleri Waafrika wanakazana kufanya makongamano ya uponyaji kwa maombezi. Kifupi, Kanisa letu limeshuka chini. Inasikitisha, yaani Kanisa Katoliki pamoja na zahanati, vituo vya afya, hospitali na wataalamu wake linakopi ujinga wa makanisa yasiyo hata na kisanduku cha dawa za huduma ya kwanza (first aid kit).
Walei wamewaambia, “Tuna matatizo ya ufukara tufanyieni ibada za kutupatia mafanikio kwa njia nyepesi ya kukemea umaskini na kuamuru kwa maneno watu tupate ajira, magari, nyumba na kadhalika kwa kusali tu,” wakleri wamekubali wanafanya kama walivyoambiwa. Wameharunika na kusahau kabisa kwamba “injili ya mafanikio pasipo kufanya kazi” si mafundisho ya Kanisa Katoliki. Wameharunika hata kukubali akili nyepesi ya Kinjikitile ya kutatua tatizo gumu kwa maneno matupu. Kinjikitile aliwaaminisha watu kwamba risasi zingegeuka maji kwa kuzitamkia tu, “MAJI, MAJI, MAJI, MAJI!”
Maskini! Wamesahau wamisionari walipotukuta na ufukara wa kunuka walikazana kutufundisha kilimo na ufugaji, kinyume chao, wakleri Waafrika wanakazana kufanya makongamano ya kuondoa umaskini wa watu kwa maombezi na makemeo ya “UMASKINI ONDOKA!” “UMASKINI ONDOKA!” “ROHO YA UMASKINI ACHILIA!” “ROHO YA UMASKINI ACHILIA!” Kifupi, Kanisa letu limeshuka chini. Tunajilisha ujinga na akili ya Kinjikitile. Inasikitisha, yaani Kanisa Katoliki pamoja na shule, vyuo na wataalamu wake linakopi ujinga wa makanisa ya “private.”
Walei wamewaambia, “Tuna matatizo ya ajira, ujane, kutopata watoto, kutoolewa na kadhalika tufanyieni ibada kali matatizo hayo yayeyuke kwa miujiza,” wakleri wamekubali wanafanya kama walivyoambiwa. Wameharunika na kusahau kabisa kwamba miujiza kumbakumba haikuamriwa na Yesu na hayo wanayong’ang’ania walei yafanywe si mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Walei wamewaambia, “Kuna walozi na wachawi angani, hewani na katika mitaa yetu tuzindikieni anga na turuhusuni tuwe tunasali usiku wa manane tuzuie ndege za wachawi zisiruke,” wakleri wamekubali wanafanya kama walivyoambiwa. Wameharunika na kusahau kabisa kwamba miujiza kumbakumba haikuamriwa na Yesu na hayo wanayong’ang’ania walei yafanywe si mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Katika yote, kinachosikitisha zaidi katika kuharunika ni kwamba hakuna “Musa” wa kuwashtusha walioharunika. Hakuna “anayemusika.” Hakuna mwenye uwezo wa kuwauliza walioharunika, “Watu hawa wamewafanya nini hata mkaleta dhambi kuu hii juu yao?” Kwa maneno mengine hakuna anayewauliza, “Enyi akina Haruni watu hawa wamefauluje kuwadanganyeni ninyi viongozi wazima hata ninyi kufanya walivyotaka wao badala ya ninyi kusali na kujipatia majawabu mazuri ya kiroho hata kuwasaidia kubaki katika imani ya kweli ya Kanisa Katoliki? Wamekulisheni nini au wamekupeni nini hata mkasahau nafasi zenu za uongozi?
Masomo ya miaka saba Seminarini, na wengine kupewa fursa ya kupata masomo ya juu katika vyuo vikuu bora, yalikusudiwa wakleri wasiharunike. Lakini loh, wanavyoharunika inatufanya watu tusione maana ya kuwa na Seminari Kuu wala maana ya mkleri kupelekwa ng’ambo kwa masomo ya juu. Lakini balaa, baba lao, ni kule kushindwa kwa baadhi yao kufundisha wenyewe hata kuwakaribisha viongozi wa “makanisa ya private” wawafundishie kondoo wao! Ha! Haiingii akilini! Hata kufundisha kunabinafsishwa!
Nimalizie kwa mfano bayana zaidi. Kuharunika ndiko kunakofanya Karismatiki wasikemewe na yeyote hata kama wanafanyiza mambo kinyume kabisa na maagizo ya Yesu Kristo, Bwana wetu (rej. Mt 6:5-8) na kinyume kabisa na Maandiko Mtakatifu (rej. 1Kor 14:26-40). Hii maana yake nini? Maana yake ni kwamba wakleri wanashindwa kujua kwamba kwa vitendo vyao Karismatiki ni wapinga Kristo na wapinga Maandiko Matakatifu kwa viwango vipi. Kushindwa huko ndiko kunakowafanya siyo tu wasiwakemee bali hata wao wenyewe wawemo ndani. Lakini “poa”, nitalijadili jambo hili katika makala rasmi, makala itakayokwenda kwa kichwa cha “MAKONGOMANO YA AIBU NA MAKONGAMANO YA HAIBA.” Humo nitaeleza jinsi sisi viongozi tulioharunika tunavyoachilia au kushadidia “makongamano ya kulofazana” huku tunamsingizia Roho Mtakatifu kuyadhamini.
Ndipo sisi tunapiga kelele, kutoana mapepo na eti kufunguliana kutoka kwenye laana na uchawi wakati wenzetu Ulaya, Marekani na Asia wanafanya makongamano haiba, makongamano ya kiuchumi kupanga mikakati mikubwa ya kibiashara na kiuchumi. Nadhani katika mwezi huu wa Juni tumeshasikia habari ya makongamano ya kiuchumi ya Shagri-La, ya St. Petersburg, ya Qatar na kadhalika. Sasa linganisha makongamano hayo na yetu ya kulofazana katika majimbo, dekania au parokia na kadhalika yanayofanyika katika miezi ya Mei, Juni na Julai kila mwaka. Makongomano yetu na yao ni tofauti kama ya kati ya kaniki na kanga au kati ya usiku na mchana. Katika makongamano yetu, eti akina baba na wake zao na watoto wao na wajukuu zao, makleri na watawa na walei wao wanakusanyika kumlilia Mungu awajalie ajira, awaondolee ujane, awapatie wachumba, awaondolee umaskini, awafungue kwenye vifungo vya nuksi, “awatoe mapepo”, “awatoe majini”, awaondolee madeni na kadhalika. Ha! Aibu! Yaani hatufanyi mikakati ya pamoja ya kutumia akili na rasilimali zetu! Kwa namna hii hatuendi mbele bali tunapiga mbio kurudi nyuma. Matokeo yake Waafrika hatutaamka kamwe (ng’o) na kwa namna hiyo tutakae mkao wa kutawaliwa na kuombaomba milele.
Kugehazika
Nabii Elisha alikuwa na kijana wake aliyekuwa akimsaidia kazi. Baada ya Naamani kuponywa ukoma wake, Naamani alitaka kumzawadia nabii Elisha pesa vipande elfu tatu na mavazi mawili ya sikukuu. Elisha alikataa akisema aliyemponya ukoma ni Mungu na si yeye nabii. Alibaini vitu vile vingelingana na malipo ya huduma aliyoitoa. Kinyume chake, kijana Gehazi aliona kukataa vitu vile vizuri ulikuwa ujinga wa hali ya juu. Moyoni mwake aliona nabii angelipokea vitu vile kama malipo ya kufanikisha muujiza. Basi, akanuia yeye kuvichukua vitu vile alivyokataa nabii.
Basi, Gehazi alimtoroka Elisha, akamfukuzia Naamani njiani na kumdanganya kwamba nabii Elisha alighairi na hivyo alikuwa anavitaka vitu vile kwa vile huko nyuma amefikiwa na manabii wenzake wawili. Naamani akatoa vipande elfu sita na mavazi yale ya sikukuu wakati ilikuwa uongo mtupu. Gehazi akajipatia mali kwa ulaghai. Kutamani na kujipatia mali katika huduma za Mungu ndiko ninakokuita kugehazika. Gehazi alitaka huduma ya kinabii ilipiwe na siyo kutolewa bure. Kisa hiki kimesimuliwa vizuri katika 2Fal 5:1-27.
Tusemeje sasa? Tuseme ifuatavyo:
Siku hizi wakleri wengi wanatoa huduma za kiroho wakidai namna ya malipo. Wamegehazika. Wakitoa sakramenti ya Ubatizo, lazima aliyehudumiwa atoe asante. Wakitoa sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa, lazima aliyehudumiwa atoe asante. Wakitoa sakramenti ya Ndoa, lazima waliohudumiwa watoe asante. Wakiadhimisha misa, lazima waliohudumiwa watoe asante. Kifupi, hakuna tena kufanana na Elisha, yaani kutoa huduma bure kama alivyopendekeza Yesu (Mt 10:8). Kanuni inayojengeka sasa ni “Sakramenti au huduma ya kiroho kwa mshiko.” Inakuwa kana kwamba tunaishi falsafa ya “Hapendwi mtu, ila pochi.”
Nimepata habari ya ziada ya kusikitisha, eti kwamba mapadre na maaskofu wengine wakitembelea parokia au taasisi fulani, lazima “washikwe mkono” kwa bahasha nono. Jambo hili linawakera sana waamini. Kwa nini? Kwa sababu limeongeza michango katika Kanisa Katoliki. Lakini hapo hapo pamefungulia mlango uovu mwingine. Karismatiki wameona fursa ya kujipenyeza na mafundisho yao ya kizushi. Wamepatiwa uwezekano wa “kununua njia” ya kuingilia mahali na kupandikiza uovu wao. Ni hivi, kwa kuwa Maaskofu na mapadre wanapenda sasa wakitoa huduma “washikwe mkono kwa bahasha nono”, huwa wanaandaa bahasha hizo nono na kuwakabidhi na hivyo kuwafunga macho na midomo waweze kujieneza jimboni au parokiani pasipo kusahihishwa wala kukemewa na mtu yeyote. Alahaula, ni kanuni ile ile ya “Penye udhia penyeza rupia.” Kumbe, ni kugehazika kunakosababisha viongozi wanunulike na vinywa vyao vifumbike. Asalaleh!
Kuyudaika
Hapa tuwaache akina Yuda kedekede waliosimuliwa katika Biblia Takatifu, tumchukue Yuda mmoja tu, Yuda Iskariote. Kwa kituko alichokifanya ninajenga msamiati wa kuyudaika. Kisa hiki kimesimuliwa vizuri katika Lk 22:1-6. Yuda Iskariote aliishi na Yesu kinafiki tu. Yeye alikuwa anawinda kutengeneza pesa tu. Mkoba aliopewa autunze kama mhasibu akawa anadokoa vilivyokuwa vikitiwa ndani yake. Kila jambo alililotazama alilitazama kwa macho ya kutengeneza pesa ajinufaishe yeye. Ndiyo kisa Yesu alipokuwa anapakwa mafuta ya gharama kubwa, akatafsiri kama hasara kwani yangeuzwa kungelipatikana pesa nyingi za kuwasaidia maskini. Lakini mwinjili anasema hilo alilisema kiunafiki tu, wala hakuwa anawawazia maskini kwa dhati isipokuwa kinyume chake alikuwa akitamani mafuta yangeuzwa zikapatikana pesa nyingi ambazo zingeliingizwa kwenye mfuko yeye akapata nafasi ya kuiba pakubwa (Yn 13:4-8).
Kutokana na uchu wa kipato binafsi, mwishoni mwa mambo, Yuda Iskariote aliona hata akimuuza Yesu mwenyewe atapata kitu ndipo akamuuza kweli. Ndugu zanguni, huko kuishi kanisani na kutenda kazi kwa kuwinda pesa ili mtu ajinufaishe, unafiki na uroho unaomfikisha pahala pa mtu kumwona Yesu kama bidhaa ya kuuzwa ndiyo ninayoiita kuyudaika.
Tusemeje sasa? Tuseme ifuatavyo: Siku hizi, si wakleri haba walioyudaika. Wanaweza kuwekwa katika nafasi kubwa au pengine hata ndogo ambapo watakuwa wanafanya kazi wakipiga hesabu za jinsi ya kujipatia kitu tu. Mali wanazokadhiwa wanaweza kudokoa na jambo lenye kuuzika wanaweza kuuza. Aghalabu, wanakuwa na jicho la kunyemelea fursa za kutengeneza pesa katika hayo hayo wanayosema wanayatumikia bure. Jambo hili linawafanya walioyudaika wawe katika fikra endelevu za kutafuta jinsi gani ya kumuuza Yesu au Ukristo na wao kujitajirisha binafsi. Ndipo hapo wanapoishia “kuibiadhisha” au “kubiasharisha” injili kwa uongo na ulaghai mwingi.
Hata hoja ya kuipokea karismatiki mahali husema kwamba kiongozi mhusika ameyudaika maana utasikia, “karismatiki wanafaa kwa sababu wanapokuwapo wanaongeza utoaji wa sadaka na zaka”. Ebo! kuyudaika huko! Tangu lini Yesu alisema, “Nendeni dunia kote kwa kipaumbele cha kuchangisha watu sadaka na zaka?” Kumbe, ndugu zanguni, kuyudaika ndiko kunakoibusha kashfa nyingi katika ofisi kubwa kubwa kanisani ikiwa pamoja na benki ya Kanisa huko Vatikano.
Mzee wenu Pd. Titus Amigu