Kuharibika kwa Mimba: Fahamu Sababu, Kinga na Tiba za tatizo hili

Una uhakika ulikuwa na mimba? Ulifanya vipimo kuthibitisha? Pole sana.
 
Reactions: BAK
Pole mwaya.

Sababu ziko nyingi, kwanzia stress mpaka kua na matatizo ya uzazi!! Kwa uhakika zaidi ni vizuri ukamuona gynecologist.
 
Reactions: BAK
Pole mwaya.
Sababu ziko nyingi, kwanzia stress mpaka kua na matatizo ya uzazi!! Kwa uhakika zaidi ni vizuri ukamuona gynecologist. . . .

Kama alivyosema Lizzy kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha ujauzito kuharibika. Wataalamu wa mambo ya ujauzito mara nyingi wanaweza kukwambia sababu baada ya kufanya uchunguzi lakini wakati mwingine wanaweza wasijue kabisa kipi kilisababisha ujauzito kuharibika. Pole sana.
 
Ni vyema ukamwona daktari kwa uchunguzi na ushauri zaid mana huenda labda ni maambukizi ya fangaz kwenye kizazi, au labda mimba haikukaa vizuri kwenye mfuko wake, au kazi nzito unazofanya, au stress yn sbb ziko nyingi sana ila nakushauri MWONE DAKTARI KABLA HUJAPATA UJAUZITO NA BAADA TU YAKUJIGUNDUA U MJAMZITO. POLE SANA MPENDWA
 
Kaz nzito nzito, utumiaj wa madawa,kufanya ngono wakat ukiwa mjamzito, matatizo ya kurith, utapiamlo, maradh wakat wa mimba, kisukari na presha.
 
kaz nzito nzito,utumiaj wa madawa,kufanya ngono wakat ukiwa mjamzito, matatizo ya kurith, utapiamlo, maradh wakat wa mimba,kisukar na presha

Rais Kivuli, mambo yote uliyo yataja hapo sio sababu kubwa zinazosababisha kuharibika mimba! Ni vema ukajua kwamba wanawake wengi hupata ujauzito, na mimba hutoka bila wao kujua kama walikuwa ni wajawazito. Sababu ya mimba kuharibika zikiwa changa kwenye umri wa hadi wiki 12 ni matatizo ya kimaumbile (chromosomal abnormalities).

Na hii ni natural selection tu hutokea kwani nature huona kwamba kiumbe atakaye zaliwa hata weza kuishi kwenye mazingira ya kawaida (compatible with environment) na hivyo hutolewa mapema. Na hapa defect huwa zaidi kwenye cell division wakati wa organogenesis. Issue ya kizazi kulegea (cevical incompetency), matatizo ya mfuko wa kizazi (uterine abnormality),magonjwa (infection), na magonjwa ya mama mjamzito hufuata baadaye.

Ni vizuri ukawaona wataalamu pindi utakapo jihisi kuwa mjamzito ili upate huduma mapema. Lakini ni muhimu pia kupata pre conception care ambayo ni uchunguzi na huduma kabla ya kubeba mimba kwa takriban miezi mitatu kabla ili kuhakikisha unaondoa hatari zozote ambazo zingeweza kujitokeza kwa baadaye.
 
JF Doctors
naombeni ushauri kwani nina MYOMA inanisumbua sana,baada ya kupima nikakuta zipo 5 zenye size tofauti na kila nikipachikwa mimba hutokea miscarriage na nimeelezwa kuwa miscarriage hizo husabishwa na MYOMA zinagombania nafasi na mtoto na mwisho wa siku zenyewe hushinda

nacho omba kama kuna dawa ya kuziondoa kabisa ama ni lazima nifanyiwe operation?

nawasilisha.



 

Waweza fanyiwa procedure iitwayo "Magnetic resonance-guided focused ultrasound surgery"
yenyewe haitaji upasuaji,lakini sina hakika kama Tz wanafanya hiyo procedure.
 
Huwa tunasikia Wachungaji wanaponya, viwete, vipofu, ukoma, wazimu, au huwa ile ni "wajinga ndio waliwao""?

Nakumbuka Nyerere aliwapiga marufuku pale mnazi mmoja akawaambia kama wakweli nendeni Muhimbili na Oshen rodi, wagonjwa wamejaa huko.

Nenda India.
 
Mimba iliyoharibika wiki sita hivi baada ya kutungwa, yaani wiki nane hivi baada yahedhi ya mwisho.


Shamba la Mungu kwa watoto wasiozaliwa.

Mimba kuharibika ni tukio linalopatikana mara nyingi katika wanawake na mamalia wa kike kutokana na shida mbalimbali katika ukuaji wamimba tumboni mwa mama.

Ni tukio tofauti na utoaji mimba ambalo linasababishwa na binadamu kwa makusudi.
Matukio yote mawili kwa kawaida yanaleta matatizo mbalimbali kwa mama.

Kuharibika kwa kijusi au kiinitete pengine kunatokana na mfadhaiko wa kiajali au sababu za kimaumbile. Mimba nyingi huharibika kutokana na kutonakiliwa kisahihi kwa kromosomu; pia huweza kuharibika kutokana na mazingira.

Mimba inayotamatika kabla ya wiki ya 37 katika kipindi cha ujauzito husababisha uzaaji wa mtoto hai na hujulikana kama kuzaliwa mapema.

Kijusi akifa akiwa ndani ya chupa ya uzazi baada ya wiki 22, au wakati wa kujifungua, kwa kawaida hujulikana kama mzaliwa-mfu au siriziki. Kuzaa mapema na uzazimfu kwa jumla hauchukuliwi kama kuharibika mimba ingawa matumizi ya maneno haya wakati mwingine yakaingiliana.

Kati ya 10% na 50% ya mimba hutamatishwa kwa njia zinazoweza kubainishwa kimatibabu, kutegemea umri na afya ya mwanamke mjamzito.

Mimba nyingi huharibika katika hatua za mapema sana za ujauzito, kiasi kwamba mwanamke hafahamu kwamba alikuwa mjamzito. Utafiti mmoja uliofanywa kupima homoni za kutoa yai na ujauzito uligundua kuwa 61.9% ya uhamili ulipotezwa kabla

ya wiki 12, na 91.7% ya kuhabirika huko kulitokea bila ya dalili, na bila ya fahamu ya mwanamke aliyekuwa mjamzito.
Hatari ya kutoka mimba ghafla hupungua kwa kiasi kikubwa baada ya wiki 10 kutoka kipindi cha mwisho cha hedhi.

Kisababishi kikuu cha mimba kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza huwa matatizo ya kromosomu ya kiinitete / kijusi, hali ambayo husababisha angalau 50% ya kutoka kwa mimba mapema.

Sababu nyingine ni pamoja na magonjwa ya mishipa (kama lupus), kisukari, matatizo mengine ya homoni, maambukizi, na matatizo ya chupa ya uzazi.

Umri mkubwa na historia ya mimba zilizotangulia kuharibika ni sababu mbili kuu zinazohusishwa kwa pakubwa na mimba kuharibika ghafla.

Hiyo inaweza pia kusababishwa na kiwewe kinachotokana na ajali.
 
Mke wangu alikuwa na mimba ya miezi 2, alipata homa mimba ikaharibika. Mpaka sasa ni siku ya kumi toka aanze kupata damu baada ya mimba kuharibika. Huku nilipo ni kijijini sana na daktari wa zahanati kasema damu itakata yenyewe. Je, ni dawa gani anatumia mwanamke aliyeharibu mimba kama antbiotic? Je, ni dawa gani inasaidia kukata damu? Msaada jamani. Huku nilipo ni zaidi ya kijijini.
 
Anatoka damu kiasi gani? Kama anajaza pedi moja ndani ya lisaa limoja anapoteza damu nyingi sana!
Kwa kawaida huwa anaenda hedhi siku ngapi? Mara nyingine baada ya kupoteza mimba mtu anaweza kwenda hedhi siku nyingi kuliko kawaida.

Either way, I suggest uende hospitali kubwa kidogo! Maisha ya mkeo yaweza kuwa hatarini hapa!
Poleni sana. Mungu atawaponya!
 
Mkuu pole sana,hapo hata kama ni kijijini sana mpeleke mkeo hospitali kwaajili ya kunusuru maisha.
 
Mkimbize hospital haraka. usiulize mkuu. Kimbiza hospitali fasta kabla hata madoctor hawajagoma tena.
 
Pole sana, mpeleke hospitali ya wilayani kwako aua mkoa kusiwe na ngoja ngoja tena.
 
Mkuu pole sana. kwa kawaida baada ya mimba kutoka mwanamke hutoka damu week 3 -5 wengine hadi week 8. Zingatia yafuatayo ili kuokoa maisha ya mkeo 1. Mpeleka hospitali kubwa referal hosp 2. Hakikisha anakunywa maji na juice ya kutosha 3. Hakikisha anatumia matunda ili kupata vitamin kama machungwa,nanasi,embe, papai etc 4. Hauruhusiwi kusex na mkeo mpaka atakapopona 5. Haruhusiwi kuingizi kitu chochote kwenye uke 6. Haruhusiwi kufanya kazi yoyote mpaka apone 7. Haruhusiwi kufanya mazozi yoyote 8.apatiwe vitamin c and k supprement 9. Iron sulphate apewe kwa ajili kuzuia anemia 10. Antibiotic hapa mpaka vipimo ili kujua kama anainfection . 11. Usifanya uzembe kumbuka kutoka kwa damu ni hatari sana anapote maji, minerals, mpeleke hospita fasta kama huna hela kopa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…