Kwa dhati nampongeza Rais Dk. Magufuli kwa uamuzi wa Serikali yake kutimiza ndoto ya Taifa kuhamishia makao makuu Dodoma. Pamoja na pongezi hizi, kuna jambo moja nimeshtukia linakinzana na kaulimbiu na jitihada za Rais kupunguza matumizi ya taaasisi za umma hasa kwenye mambo kama posho za safari na malazi.
Lililonishtua ni kwamba kama hakutachukuliwa tahadhari ya haraka, Serikali hii itaingia ghalama kubwa mno katika kulipa posho za safari na kujikimu kwa Mawaziri na watendaji wengine wa Serikali ambao kiitifaki tayari wamehamia Dodoma. Kwa mfano Waziri Mkuu alikuwa kiongozi mkubwa wa kwanza kuhamia Dodoma Septemba mwaka jana. Lakini toka ahamie, kwa wastani asilimia 20 yupo Dodoma, 30% ziara mikoa mingine na 50% yupo Dar es Salaam. Wiki hii Waziri na wizara ya Utumishi wa Umma nayo iliuaga mji kwa mbwembwe kuwa inaelekea Dodoma. Lakini kumbe kilichoondoka ni magari ya mizigo Waziri bado yuko Dar! Mifano iko lukuki.
Kiitifaki hawa watumishi wanapohesabika kuhamia Dodoma, Dar na mikoa mingine inahesabika kama kazi nje ya kituo. Hivyo watumishi hao hutakiwa kulipwa posho ya malazi na ya kujikimu.
Ikiwa waliojitangaza kuhamia Dodoma muda wao mwingi wanautumia Dar maana yake ni kuwa ghalama za kuendesha Serikali zitaongezeka katika kulipa posho. Na kwa wale wasio waadilifu watatumia mwanya huo huo kuongeza mapato. Hivyo ni muhimu suala la viongzo na ofisi zilizokwishajitangaza kuhamia Dodoma zidhiitiwe kwa kuwekewa utaratibu juu ya posho za ugenini hasa Dar es Salaam. Ikumbukwe wengi wa wanaohama wanaacha familia na vitega uchumi vyao Dar. Kwa hiyo kuna kila kichocheo cha wao kupenda kurudi au kutumia muda mwingi Dar.
[HASHTAG]#TutafakariDodoma[/HASHTAG]