Kuhama kwa Patrobas kuwafungue Macho WanaCHADEMA watiifu

Kuhama kwa Patrobas kuwafungue Macho WanaCHADEMA watiifu

Benson Mramba

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
766
Reaction score
1,884
Nimeshtushwa na taarifa za kuhama kwa Patrobas Katambi kutoka CHADEMA na kwenda CCM sikuwahi kuwaza jambo hilo.

Simlaumu Patrobas kwani mazingira yake ya kiutendaji tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa kwa kiasi fulani niliyafahamu kwasababu mimi nilikuwa ni Afisa Utawala kwa miaka miwili tangu achaguliwe.

Patrobas hakuwa treated in the way he deserved. Hakuheshimiwa alivyostahili na kwa hadhi yake. Sio yeye tu. Namna Mbowe anavyoiendesha Chadema ni kimtandao kama nilivyowahi kusema awali.

Mbowe anaongoza chama akishirikiana na watu watatu tu ambao ni John Mrema, Reginald Munis na Godbless Lema. Viongozi wengine katika mfumo wa Chama ni alama tu ya kuwaonyesha wananchi wa Tanzania na after all wamependekezwa na hiki kikundi cha watu watatu.

Kikundi hiki hakiguswi wala hakikosei na ni mfano wa genge ndani ya Chadema. Mahawara wao na vijana wanaowaheshimu hawa ndio wenye fursa kwasasa ndani ya chama na ndio ambao wanatarajia kupata fursa endapo zitajitokeza.

Kwa aina hii ya uongozi ndio inayomfanya Freeman Mbowe kutengwa au kuwatenga viongozi wenzake kwani huwa hawashirikishi jambo lolote wanakaa hawajui nini kinaendelea wala hawawezi kumshauri kwa lolote.

Kwa utaratibu huu Makamu wenyeviti wote wa Mbowe na manaibu Makatibu wakuu wake wamekuwa wakishindwa kufanya nae Kazi.

Marehemu Chacha Wangwe alishindwa, Said Arfi alishindwa, Zitto Kabwe alishindwa, Dr Slaa kashindwa na hata sasa Prof Abdallah Safari kashashindwa na John Mnyika anajikaza kisabuni.

Inasemekana Prof Safari ameshajiuzulu Mara kadhaa lakini wanampigia magoti asitangaze. Mbowe amejitahidi kuwalipa mshahara mikubwa wasaidizi wake hao lakini hawapangii kazi yoyote jambo ambalo ni ufujaji wa Mali za Chama na matumizi mabaya ya madaraka.

Kamati Kuu ya chama kwasasa imejaa wasaka fursa, watu waoga na walamba nyayo na hawa wote ni matunda ya Kikundi hiki.

Baraza kuu la chama limejaa watu waliokata tamaa na wasioheshimiwa kwasababu wengi wameteuliwa na kikundi hiki katika programu inayoitwa CHADEMA NI MSINGI.

Mathalani katika kikao cha baraza kuu lililofanyika Mwanza John Mrema, Reginald Munis na Salum Mwalimu walituhumiwa kula rushwa ya ngono na fedha na ushahidi ukatolewa na Msigwa na Sugu maazimio yakafikiwa. Ila Mbowe amewalinda watu wake akawateua kuwa wakurugenzi akawaongeza na mishahara mikubwa sana Mara 2 ya awali. Kutoka mil 1.5 mpaka mil 3. Msigwa na Sugu nao wakapozwa kwa kupewa ujumbe wa kamati Kuu wametulia mpaka leo.

Kwasasa kikundi hiki cha watu wanne kinafanya kazi Maalum ya kumdhibiti Lissu na Lowassa na wenzake kutoka CCM wasipate fursa yoyote ndani ya Chama kwasababu kuu mbili:- 1. Mbowe bado anataka kuwa Mwenyekiti wa Chama 2. Mbowe anataka kugombea Urais 2020

Katika muktadha huo huo Masha ameshtuka mapema wengine watamfuata soon. Mbowe amerejista deni LA bilioni saba na
Mali nyingine za chama kama hatua za kujiandaa na mbio za Urais 2020.

Reginald Munis pia alikuwa ndio Meneja wa Billicanas kabla haijafungwa na wakati huo huo mpaka sasa ni Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Uchaguzi na Wanachama

John Mrema ni Mkurugenzi wa Uenezi,Itikadi na Mambo ya Nje .

Lema ni Mbunge ila pia yuko kwenye ulinzi na intelijensia.

Kwa wanaojua siasa idara za wanakikundi hao ndio zimeshika Chama chochote cha siasa. Mashinji he is just a signatory hana analoweza kufanya wala kupanga.

WanaChadema hangaikeni na mambo ya ndani ya Chama kwasasa huku Nje kwenye maswala ya nchi Magufuli anafanya yanayotakiwa na watanzania walio wengi wakiwemo wanachadema.
 
Kwasasa kikundi hiki cha watu wanne kinafanya kazi Maalum ya kumdhibiti Lissu na Lowassa na wenzake kutoka CCM wasipate fursa yoyote ndani ya Chama kwasababu kuu mbili:- 1. Mbowe bado anataka kuwa Mwenyekiti wa Chama 2. Mbowe anataka kugombea Urais 2020
Nyee watu mnashangaza sana na inaelekea kuna kikundi kingine kimeibuka kimeshavuta mkwanja kwa ajili ya kuichafua CHADEMA kama kikundi kile cha akina Mwampamba na akina Shonza.

Mara mseme Mbowe alimuuzia chama Lowassa kwa bilioni 10,mara mseme CHADEMA ni mali ya Lowassa.

Sasa sijui Mbowe anawezaje kutafuta kumdhibiti Lowassa mwenye chama ambacho alikipata kwa kununua kwa gharama kubwa,na ni Mbowe huyohuyo aliyemkaribisha Lowassa kwenye chama kugombea nafasi ya urais baada ya kumuona kuwa Lowassa ana nguvu kubwa ya kukisaidia chama kutokana na nguvu yake aliyonayo pengine hata kumzidi Mbowe mwenyewe.

Na baada ya Lowassa kujiunga CHADEMA na kugombea urais kupitia CHADEMA chini ya UKAWA chama kimepata mafanikio makubwa sana kuliko wakati wowote ule ikiwa ni pamoja na kupata kura nyingi za urais pamoja na kupata wabunge wengi sambamba na kuongezeka ruzuku ya chama.

Mbowe ataonekana ni mtu wa ajabu sana kama ni kweli atataka kumdhibiti mtu ambaye alimkaribisha mwenyewe akijua kuwa mtu huyo ni mtu mwenye nguvu za kiushawishi kwa wananchi pengine hata kumpita Mbowe mwenyewe.

Mbowe ataonekana ni mtu wa ajabu sana kufanya mipango ya kumdhibiti mtu ambaye amekiletea chama mafanikio makubwa kupita wakati wowote na atakuwa hajui alitendalo katika harakati zake za kuiondoa CCM madarakani.

Kama ni suala la baadhi ya watu kuonekana tofauti na wengine hilo ni jambo la kawaida katika mambo ya utawala hata CCM yapo,ACT yapo hata katika kuiongoza nchi lazima mambo hayo yawepo.

Ambapo kiongozi anaweza akawa karibu na watu fulanifulani kutokana na sababu zake mwenyewe anazozifahamu mwenyewe na anaweza asiwe karibu na baadhi watu wengine kutokana na sababu zake kama vile Magufuli na Bashite.

Mtasema wee na kusema mabaya yote aliyonayo lakini mwenye mtu atainuka na kusema wewe chapa kazi niliyekuteua ni mimi na akina Nape wanafukuzwa kazi wakati wote wameteuliwa na mtu yuleyule lakini anawachukulia kwa uzito tofauti.
 
Chama kinatakiwa kifahamu viongozi wake wake, kiwawezeshe, kiwapime utendaji kazi, kipokee maoni na kuyaheshimu kama kuna kasoro pande zote zirekebishwe.

Hizi blah blah tunazosikia sasa sijui alikua galasa, hajui kazi, alikua mamluki ni non sense. Ni upumbavu wa hali ya juu kuanza kusema hayo leo wakati muda muafaka ambao uliwekuwepo kuweza kurekebisha kasoro hizo hilo halikufanyika. Niwasihi vijana tuache kauli hizo tutoe michango yetu na maoni yetu kurekebisha kasoro.

Bwana Katambi ilishasemwa haiwezi Bavicha baada ya kushindwa kwenda na kasi ya siasa za harakati, siasa za tit for tat lakini hatua hazikuchukuliwa ili kumfanya aendane na hali ya sasa au hata kumuondoa aingie mwingine.

Funzo lingine viongozi waache siasa za haki zichukue nafasi watu wapimwe kwa mchango wao katika harakati Chadema ina vijana wengi wazuri kisiasa, wasomi, wenye kuweza kujenga hoja mara mia ya Patrobas na hata kwenye uchaguzi huyu jamaa asingeshinda kama sio mbeleko za wakubwa fulani wanaoamini kwamba maono yao ni sahihi bila kujua kwamba wanakosea.

Iwe funzo kwenye chaguzi na teuzi ndani ya chama viongozi watazame vizuri maamuzi yao sitaki kuzungumzia ilivyokua viti Maalumu tulishapiga kelele hilo, tulishapiga kelele hadi rafu za huko majimboni.

Sitasahu kukatwa kwa 'man of the people' Peter Lijuakali ili nafasi iende kwa Peter Kibatala japo natambua mchango wa kibatala kwa chama lakini yale yalikua maamuzi ya hovyo nakumbuka nilimtext Lijuakali kumtia moyo.
Mungu bariki kilio kilisikika wakarekebisha.

Pia sitazungumzia uchaguzi wa Eala kwa wajumbe kumpitisha 'wakuja' bwn Masha ambaye leo hii katimkia Ccm na kumuacha binti jasiri wa chadema Nusrat Hanje.

SIASA NA KIPATO.
Inadaiwa kwamba Patrobas muda mrefu alikua akilalamika njaa kwamba ilifikia wakati anakumbuka kazi yake ya uandishi aliyoacha pale radio free Africa. Najiuliza Je chadema alikua halipwi??

Nashindwa kuamini kwamba mwenyekiti Bavicha taifa hana mshahara, au hana usafiri wa kazini au hana nyumba ya kuishi anayolipiwa na chama.

Kama haya ni kweli ni maajabu.
Ajabu namba 1.
Unawezaje kumpa mtu majukumu makubwa ya kitaifa ya full time huku ukiwa humuwezeshi kimaisha je unategemea aishi vipi? Ni vipi atimize mahitaji yake yeye mwenzi wake, familia yake n.k huyu ni kijana lazima atakua na mke kama si mbeebz sasa ishu ya njaa na stress za kukosa pesa huku Mbeebz anakuazama ni wazi uvumilivu umemshinda.

Ajabu namba 2.
Chama kinapokea ruzuku. Sasa kama Patrobas kwa nafasi yake ya Mwenyekiti Bavicha analia njaa Ruzuku ya chama inatumika matumizi gani?

Japo tunafahamu kwamba siasa za upinzani sio za kusaka pesa ulaji lakini yapo mahitaji ya msingi lazima mtu atimiziwe na kutimiziwa huko ni kumlipa mshahara na hiyo ndio kazi ya ruzuku siasa haiwezi kwenda na njaa tuache kujilisha upepo. Let say Patrobas analia njaa then same time anamuangalia mwenzake Juliana Shonza huko ccm hivi unadhani anajisikiaje? Je wakija watu na fungu hatafika bei?

Tunajua mwenyekiti Mbowe hapokei mshahara ni kweli lakini yule ni Tajiri hana njaa je vipi kwa hawa wengine?

Wenyeviti wa mikoa na wilaya wanalipwa? Angalau ile ya kujikimu tu maisha ya kila siku? Kama hapana je wanawezeshwa vipi basi? Mana achana kabisa na kitu njaa siku wakiuza majimbo huko tusisikie makelele na Ccm inatumia udhaifu huo kufanya inachotaka.

Ipo sheria kwamba mtumishi wa umma haruhusiwi kuwa kiongozi wa kisiasa sheria hiyo ni kama mtengo kuvibana vyama vya upinzani visipate watu wasomi wenye ushawishi na uzoefu serikalini.

Hivi kweli kijana anaweza kucha kazi na mshahara serikalini akaenda kugombea nafasi kutumikia chama halafu huko asilipwe sasa ataishi vipi?

Chadema inapaswa kuruka mtego huo kwa kuweka mishahara kwa viongozi wake ili kuvuta hata watumishi wawe tayari kuacha kazi zao waingie chamani wasukume harakati mbele otherwise tuseme tumeamua kusubiria wastaafu waliochoka au wafanya biashara ambao wengi wanakuja kwa maslahi yao.

KAULI YA PATROBAS
"Kijana ukiwa chadema unatumika kama karai la ujenzi wa nyumba na nyumba ikishaisha na kupigwa rangi unatupwa"

Ipo haja ya chama kitathmini kauli hiyo kwa undani zaidi lakini kama wenye mamlaka watapuuzia nakuona ni kauli ya mtu msaliti basi ni wazi tutakua tunafanya makosa makubwa sana. Ni wakati mchango wa vijana uthaminiwe, ni wakati sasa wa maoni na mawazo ya vijana wasomi yaheshimiwe.

Waliohama wamehama ila wametuachia mafunzo, turekebishe tusonge mbele.
 
Sipingi maelezo ya mleta post hata kama sijui yana ukweli kiasi gani lakini lazima kuna ukweli fulani katika uliyoyaandika.

Mimi ni shabiki wa CHADEMA na nimeshasema sasa iwe ndio mwisho wa Mbowe kuwa mwenyekiti kwani mchango wake unatosha. Hao Lowassa na Sumaye wabaki wanachama tu wa kawaida kwani nao sio aina ya wanachama wa CHADEMA tunaowajua.

Ni kawaida mtu akikaa madarakani muda mrefu kuanza kuongoza nje ya misingi na ubunifu kupungua. Demokrasia ya kweli ni pamoja na kupisha wengine. Kuna viongozi wazuri tu.

Mengine ni propaganda za kawaida za wanasiasa.
 
Shida ni kuwa watu ni wabinafsi sana.

Vijana wengi wanaoingia siasa za upinzani wanakuja na malengo yao binafsi na sio malengo ya chama na nchi. Ndiyo maana akina Patrobas wanajifananisha na makarai. Chama kinemuiñua, kikampa fursa ya kugombea ubunge sema tu alishondwa.

Najiuliza kama kweli angeshinda ubunge angefanya kile alichofanya leo? Mimi nasema Mbowe songa mbele, siasa za upinzani ni lazima ziwe za kujitolea, mwenyekiti wa Bavicha alitakiwa awe na means nyingine ya kuishi sio kusubiri posho.

Ukweli ulio wazi ni kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya Bavicha ya Heche na ya Patrobas. Patrobas ameonyesha kupwaya sana na Bavicha imepoteza nguvu, hata hivyo hatumlaumu sana kwani siasa kwenye awamu ya 5 zimebadilika sana. Hata hivyo ni aibu kwa kiongozi kuanza kulalamika na kukimbia chama.

Napendekeza kuwa watu wa aina ya Patrobas, Masha waondoke mapema CDM kwani kazi ya ukombozi wa Taifa letu inaelekea kukamilika.

Mark my words. Mungu anakwenda kutufurahisha watanzania kwa hiyo wala wote waondoke mapema.
 
Mimi ambalo huwa linanishangaza hivi mashabiki wa CHADEMA wanatumia akili gani kuendelea kuwa mashabiki wa chama hiki? Am sorry, it may look annoying, lakini huwa sielewi kwa kweli.

Nilikuwa shabiki mkubwa wa CHADEMA hadi pale kilipobadili gia angani. Sababu kiligeuza misingi iliyokikuza chama. Ukweli ni kwamba CHADEMA hakikuwa chama kinachopendwa na watu wengi, mpaka pale kilipoaminika kupiga vita ufisadi kwa nguvu zote, na ni wazi watu wengi walimwamini sana Dr Slaa. Ndio ulikuwa muhimili wa chama.

Sasa hivi CHADEMA kimekaribisha na kukumbatia mafisadi waliolaumiwa na chama hicho hicho kwa miaka mingi ya nyuma. Pili wamekuwa wapingaji wakubwa wa hata mambo makubwa ya kuleta maendeleo kwa wananchi yanayofanywa na utawala uliopo.

Najua wamewekeza sana kwenye propaganda hasa kwenye mitandao ya kijamii. Ili linasaidia kuteka akili za baadhi ya vijana. Lakini si mbinu sustainable, hasa kama serikali wanayoipinga inajitahidi sana kutatua matatizo ya wananchi wengi na kuleta maendeleo.
 
Patrobas hakuwa treated in the way he deserved. Hakuheshimiwa alivyostahili na kwa hadhi yake. Sio yeye tu. Namna Mbowe anavyoiendesha Chadema ni kimtandao kama nilivyowahi kusema awali.

Kama mfalme siyo?
Vijana wa siku hizi mnapenda kulelewa! Vipi wewe umepata mlezi???.
Umnenunuliwa kwa kiasi gani kuja na pumba hizi??
 
Kama mfalme siyo?
Vijana wa siku hizi mnapenda kulelewa! Vipi wewe umepata mlezi???.
Umnenunuliwa kwa kiasi gani kuja na pumba hizi??

Kila anayesema ukweli u against hao watajwa anatfuta mlezi? Au INA maana amenunuliwa? Amesema anatafuta mlezi?

Jamani lini watanzania tutajifunza kukabili hoja kwa hoja badala ya kutoa mapovu Maneno yasiyo lenga kujibu hoja mezani ?

Ndo maana nasikia utafiti Fulani uliwahi kufanywa tukawa miongoni mwa watu wa mwisho kuwa na IQ kubwa. Inawezekana ni kweli
 
Kwasasa kikundi hiki cha watu wanne kinafanya kazi Maalum ya kumdhibiti Lissu na Lowassa na wenzake kutoka CCM wasipate fursa yoyote ndani ya Chama kwasababu kuu mbili:- 1. Mbowe bado anataka kuwa Mwenyekiti wa Chama 2. Mbowe anataka kugombea Urais 2020
huu mstari si uamini mpaka ifikie hiyo 2020,Mungu atupe uzima tuu.
 
Nawapongeza sana vijana wawili very very smart ambao wamejiunga na chama cha mapinduzi leo. Naninatoa wito kwa vijana ambao ni makarai wasomi wasingojee mpaka makarai yatoboke . Karibuni sana CCM.

Chama cha mapinduzi nakifananisha na nyumba isiyokwisha. Kila siku CCM inajengwa na nondo ngumu sana zenye kuhimili matetemeko aina yote.

Sasa kama wewe ni karai njoo tukuyeyushe uwe nondo na utumike kuijenge ccm mpya. Na mwisho wa maisha yako Jina lako itaandikwa kwa wino wa dhahabu kwa mchango wako wa kuijenga hii nchi!
Msioogope Karibuni CCM.
 
Back
Top Bottom