Kugombea ubunge kwa sababu tu ya umaarufu

Kariongo

Senior Member
Apr 5, 2012
112
5
Hii tabia ya watu kugombea ubungu kutokana na umaarufu labda alikuwa mganga wa kienyeji maarufu, muigizaji, muimbaji, mcheza shoo za twanga n.k itatuletea watunga sheria mbumbumbu. Jaman tuwen macho. Hata kule bungen kwenye mambo ya msingi utawaona tu kina lisu, Mnyika, chenge, Zito na sio kima Maji marefu, Vick kamata and the like
 
Mkuu, kwa bahati mbaya sana huwezi kuchaguliwa bila kujulikana.
Inapokuja swala la kujulikana ndipo hapo wanapoibuka akina John Komba, Vicky Kamata n.k.
Nasikia Hadija Kopa yupo njiani kuingia mjengoni, sasa hivi ni mjumbe wa Nec ya CCM.
 
Kujulikana kwanza nenda kwenu kakonko ukagombee ubunge kama ujapata kura mbili yako na ya demu wako tu.
 
Lakin"i anachosema aliyeanzisha mjadala ni kweli kabisa. Mfano mzuri jana jioni wakati wanapitisha sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii kifungu kwa kifungu. Wapo waliopitia na kufanya marekebisho, (wengi toka CDM, siwataji majina). Lakini pia kulikuwa na kundi kubwa lililokuwa linasubiri kusikia "kifungu hiki kinaafikiwa?" Halafu wajibu "Ndiyooooooo!". Yaani kama vile ushabiki fulani. Sijui hata kama walivisoma kwa makini.
 
lakin"i anachosema aliyeanzisha mjadala ni kweli kabisa. Mfano mzuri jana jioni wakati wanapitisha sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii kifungu kwa kifungu. Wapo waliopitia na kufanya marekebisho, (wengi toka cdm, siwataji majina). Lakini pia kulikuwa na kundi kubwa lililokuwa linasubiri kusikia "kifungu hiki kinaafikiwa?" halafu wajibu "ndiyooooooo!". Yaani kama vile ushabiki fulani. Sijui hata kama walivisoma kwa makini.

mfano: Lusinde.
 
Hii tabia ya watu kugombea ubungu kutokana na umaarufu labda alikuwa mganga wa kienyeji maarufu, muigizaji, muimbaji, mcheza shoo za twanga n.k itatuletea watunga sheria mbumbumbu. Jaman tuwen macho. Hata kule bungen kwenye mambo ya msingi utawaona tu kina lisu, Mnyika, chenge, Zito na sio kima Maji marefu, Vick kamata and the like

Mkuu, Sasa huyu chenge unamtaja wa nini, ungempotezea tu hata kama huchangi.
 
Ama kweli bunge la tanzania,hata mie nimejiuliza sijapata picha kabisa.inakuwaje watunga sera jamani? sheria nyingi huwa zinapitishwa na wabunge wasiozidi 5 hivi kweli ni haki? kweli elimu kwa wabunge inatakiwa
 
Mkuu, kwa bahati mbaya sana huwezi kuchaguliwa bila kujulikana.
Inapokuja swala la kujulikana ndipo hapo wanapoibuka akina John Komba, Vicky Kamata n.k.
Nasikia Hadija Kopa yupo njiani kuingia mjengoni, sasa hivi ni mjumbe wa Nec ya CCM.

Unachokisema kwa upande fulani lakini ni Katiba yetu inasema hivi:

67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wamiaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe yaUchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

My Take

1. Wananchi ndiyo tuwe makini na watu wanaokuja hata kama ni wanasheria waliobobea lazima tuwabane.
2. Hawa wanasimamia mambo yetu tunayotaka kama hawafanyi inabidi katiba mpya itoe mwanya wa namna ya kuwaengua.
 
Mimi kwa maoni yangu ni afadhali Hilo bunge waachiwe wakina mnyika na wenzake wafanyie kazi ya kutunga sheria nyumbani kwao badala ya kukusanyika halafu wengine hawachangii. LakIni kwenye suala la posho kila mtu anasimama kutetea lakini kwenye masuala ambayo ni core ya bunge wanaishia kusema ndiyooooooo
 
Back
Top Bottom