Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,743
- 2,601
Mjadala wa raia wa kigeni hususani Wachina kufurika katika maeneo ya kibiashara hasa jijini Dar es Salaam, umechukua sura mpya, baada ya Serikali kuanza kuchukua hatua za kuwafuatilia kama wanafuata taratibu za kisheria.
Hatua za Serikali zimekuja wakati kukiwa na malalamiko ya kufurika kwa Wachina nchini wakishindana na wazawa katika biashara ndogo na kandarasi za ujenzi.
Wafanyabiashara walalamika
Baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la Kariakoo Dar es Salaam wameonyesha wasiwasi wa wafanyabiashara hao wakisema wanaua biashara katika eneo hilo.
“Kwa mfano ukiagiza kontena moja ya miavuli, Mchina yeye anafungasha kontena 10 za miavuli zinakufuata nyuma,” alisema Frank Nduta anayefanya biashara katika eneo la Kariakoo alipozungumza na Mwananchi Desemba 2024.
Alisema baadhi ya wafanyabiashara wa China wamefungua maghala na wanashindana na wazawa kuuza bidhaa za rejareja.
“Ukienda China kufungasha vipuri vya baiskeli, Mchina naye anakuja nyuma yako na kontena 10 za vipuri kama hivyo unaposhusha na yeye anashusha, tena unaweza kukuta yeye akatangulia kushusha, kwa sababu wewe si utakuwa unatafuta fedha za kulipia kontena lako,” alisema.
Alisema wafanyabiashara hao hawaishii Dar es Salaam, bali wameshaanza kutafuta masoko mikoani, wakitumia pia wamachinga ambao hawalipi kodi.
“Wanawapa wamachinga, kwa mfano ukifika Mtaa wa Narung’ombe, kuna wamachinga wengi, hivi unafikiri mtu mwenye duka anayelipa kodi anaweza kushindana nao?
“Kwa hiyo wakati wewe unapambana kulipa kodi mwenzako halipi, hivyo anauza bidhaa bei ya chini.
“Pili wanachukua ajira za wazawa na wanalifanya soko liwe gumu, kwa sababu wewe unafungasha kulingana na mahitaji ya soko, mwenzako analeta kontena 10, maana yake soko linafurika bidhaa na likifurika, yeye anauza hata bei ya chini ili amalize,” amesema.
Malalamiko hayo pia yameungwa mkono na aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Martin Mbwana akisema walishapeleka malalamiko hayo kwa viongozi wa Serikali, lakini hayajafanyiwa kazi. (Alisema lini?)
“Kuna vitu ambavyo mgeni hastahili kufanya ambavyo havihitaji teknolojia na tunaweza kufanya wenyewe.
“Kwa mfano unakuta mgeni amejiajiri kwenye bodaboda au taxi, ambayo sisi tunaweza kufanya. Sisi tunanunua mzigo kwao na wao wanakuja kwetu, halafu tunakwenda kuwauzia ndugu zetu na wao wanakwenda huko huko kuwauzia ndugu zetu, hiyo haiwezekani,” alisema.
Ameongeza jitihada za kuwabana wafanyabiashara hao zinakuwa ngumu kwa kuwa wanashirikiana na wazawa.
“Wachina wanawatumia Watanzania kwenye biashara, hivyo hata ukimkamata, utakuta mwenye leseni na namba ya TIN ni Mtanzania, ila utagundua Mchina yuko nyuma na ndiyo mwenye akaunti za benki.
Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo, Severine Mushi alikiri kuwepo kwa malalamiko hayo Desemba 2024 alipozungumza na gazeti la Mwananchi, akisema ni miongoni mwa mambo aliyopanga kuyashughulikia.
“Malalamiko yaliyopo ni kwamba Wachina wakishaingiza mzigo wanafungua maduka ya rejareja kama sisi wazawa wakati hawaruhusiwi.
“Kwa kuwa sasa nimekuwa ni kiongozi, nitayashughulikia haya kwa kuzungumza na mamlaka zinazohusika ili kuhakikisha tunaangalia sheria zilizopo na jinsi ya kuondokana na kero hii,” amesema.
Mbali na masokoni, mdau aliyeandika kwenye mtandao wa Jamii Forums akisema raia wa China wamefurika katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam.
Takwimu zinaonyesha kuwa China ndiyo mbia namba moja wa biashara na uwekezaji nchini, kumekuwa na mchanganyiko wa mawazo juu ya wingi wa raia Taifa hilo namba mbili kwa uchumi duniani.
Wapo wanaoona wingi wa Wachina nchini ni fursa ya maendeleo kwa kuongeza shughuli za kiuchumi na wengine wakihofu kuibuka kwa unyonyaji mpya wa uchumi na nguvu kazi.
Kwa mujibu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), hadi Februari 2024, China imeshasajili miradi 1,274 yenye thamani ya Dola 11.4 bilioni ikilenga kuzalisha ajira 149,759 ikiwa ni matunda ya ushirikiano wake na Tanzania.
Kandarasi za ujenzi
Akisoma makadirio ya mapato na matumzi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2024/25 Mei 2024 bungeni Dodoma, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi (sasa Waziri wa Mambo ya Ndani), Innocent Bashungwa alirejea takwimu za Bodi ya Usajili wa Makandarasi akisema katika jumla ya miradi 36,839, wazawa walitekeleza miradi 35,351 sawa na asilimia 95.9 ya miradi hiyo.
Hata hivyo, alisema miradi iliyotekelezwa na wazawa ni midogomidogo yenye thamani ya Sh23.74 trilioni, sawa na asilimia 38.5 ya miradi yote iliyosajiliwa na kutekelezwa katika kipindi hicho, ambayo ni Sh61.638 trilioni.
“Hivyo, makandarasi wa nje ambao ni takriban asilimia 4.1 walitekeleza miradi michache yenye thamani kubwa (asilimia 61.5 ya thamani ya miradi yote).
“Sababu kubwa inayochangia hali hii ni uwezo mdogo wa makandarasi wa ndani wa kifedha, mitambo na wataalam hivyo inakuwa vigumu kwao kushindana kwenye zabuni za kazi na makandarasi kutoka nje hasa kampuni za Kichina,” alisema.
Miongoni mwa kampuni zinazotajwa kutawala kandarasi za ujenzi wa barabara na majengo nchini ni pamoja na China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), Sinohydro Construction Corporation, China Railways 15 Bureau Group Corporation (CR15BGC).
Nyingine ni China Wu Yi Co. Ltd, STECOL Corporation, JIANGXI, China Railway Seventh Group, China Henan International Cooperation (CHICO), China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na China Geo- Engineering Corporation.
Ujio wa East Africa Commercial and Logistics
Baadhi ya wafanyabiashara pia wameonyesha hofu ya ujio wa kituo cha biashara cha The East Africa Commercial and Logistics kinachoendelea kujengwa Ubungo Dar es Salaam, wakisema kinaweza kufifisha biashara eneo la Kariakoo.
Kituo hicho kinatarajia kuanza kazi mwaka huu 2025.
Kituo hicho kitakachokuwa na jengo lenye ghorofa nne, kitakuwa na maduka zaidi ya 2,000 na uwanja wa kuegesha magari zaidi ya 1,000.
Meneja wa kituo hicho, Cathy Wang aliyezungumza na Mwananchi Desemba 2024 aliwatoa hofu wafanyabiashara na wadau wenye hofu akisema, kituo hicho mbali na kuwa na maduka, kitawaunganisha wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa nchini China na kuepusha usumbufu kilojistiki.
“Mradi huu utakuwa ndio lango kuu la bidhaa zinazotoka China kuingia nchini na kusafirisha bidhaa kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki.
“Wafanyabiashara hawatalazimika kuagiza bidhaa nje ya nchi na kusubiri miezi mitatu minne, badala yake watachukua hapa Tanzania,” alisema Wang.
Akizungumzia hofu ya kuzorota kwa biashara katika eneo la Kariakoo, Wang amesema, “Sidhani kwamba mradi huu utazorotesha biashara katika eneo la Kariakoo, kwa sababu hilo ni eneo kubwa lililoanzishwa tangu miaka 1940, hivyo watu hawataacha kwenda.
“Halafu kama tunataka nchi iendelee, hatuwezi kulazimisha kila mtu aende Kariakoo na ujifungie hapo ukisema tusipanue biashara kama tulivyojenga hapa Ubungo,” amesema.
Amesema katika kukuza biashara, wanakusudia kuongeza vituo katika maeneo mengine kama stendi ya Magufuli na soko kubwa wilayani Temeke.
Alisema eneo hilo litakuwa kituo cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na nchi za Jumuiya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
“Hebu fikiria miaka ijayo, nchi za Afrika Mashariki hazitalazimika kwenda China kufungasha mizigo, watakuja hapa Dar es Salaam, kwa hiyo wafanyabiashara wa ndani waje hapa kuchukua bidhaa na tutawaunganisha na wazalishaji wa bidhaa,” alisema.
Akieleza manufaa ya mradi huo kwa uchumi wa Tanzania, Wang amesema ni pamoja na kuzalisha ajira.
“Mpaka sasa ambapo mradi bado haujakamilika, kuna ajira za watu 5,000 zimezalishwa katika ujenzi na tutakapoanza mradi, angalau ajira 15,000 zitazalishwa na ajira zisizo rasmi zitakuwa 50,000.
Serikali yaja na mkakati
Baada ya malalamiko kuifikia Serikali, Februari 2, 2025, Waziri wa Viwanda na Biashara aliunda kamati ya watu 15 iliyoongozwa na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Edda Tandi Lwoga.
Waziri wa Biashara Selemani Jafo aunda kamati kwa ajili ya kuchunguza utitiri wa wafanyabiashara wa kigeni Kariakoo
Hata hivyo, baada ya kutimiza kazi yake, kamati hiyo haijaweka wazi waliyopata, bali wamekabidhi ripoti kwa Waziri wa Viwanda, Dk Selemani Jafo Machi 17, 2025.
www.jamiiforums.com
Pamoja na kuweka siri taarifa walizopata, Waziri Jafo ameeleza baadhi ya mambo yaliyomo kwenye taarifa hizo, akisema tayari kuna wafanyabiashara 31 wageni (hakutaja utaifa wao) waliochukuliwa hatua.
“Tumesikia takribani watu 31 waliobainina lakini watu 24 watu hao wote waliitolewa hapa nchini. hongereni sana wajumbe wote, hamkutaka kusubiri ndio maana timu hii ilikuwa imekamilika vizuri.
“Wale wote waliobainika na ikaonekana hawafai…takribani watu 24 wameondolewa hapa nchini,” amesema.
Dk Jafo aliendelea kueleza kuwa, kamati hiyo ilipotembelea magodauni ilibainika kuwepo kwa wageni wakifanya biashara kinyume cha utaratibu.
“Mlitembelea maduka mlibaini wafanyakazi wengi ambao waonafanya kazi kinyume cha utaratibu.
“Nishukuru maeneo mliyobainisha na hasa mlipotembelea wafanyabiashara, ikabinika biashara nyingine japo zinaonekana ni za wageni, lakini usajili wake umefanyika na Watanzania, credentials (nyaraka) zao wamezitoa, vitambulisho vya vile vya Nida (vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulishi vya Taifa) na vitu vingine, kuwawezesha wale kufanya biashara kinyume cha utaratibu.
“Hii ni changamoto ya uzalendo kwetu Watanzania. Kijana wa Kitanzania unatumika kuihujumu nchi yako. Hii ni ishara mbaya, kwamba unaweza kubebesha dawa za kulevya kwa masilahi ya mtu mwingine. Unatoa uhai wako, thamani yako na utu wako kwa mtu mwingine,” alisema Waziri Jafo.
Alisema ripoti hiyo imeweka mahali pa kuanzia lakini akasema changamoto itakuwepo katika majiji mengine ambayo ni Arusha, Mbeya, Mwanza, Tanga na Dodoma.
Amewataka watendaji wa Serikali zikiwemo Idara ya Uhamiaji na Idara ya Kazi kufanyia kazi mapendekezo hayo hususani katika Soko la Kariakoo.
“Idara ya Uhamiaji na Idara ya kazi, mtaanza kazi mara moja ya soko Kariakoo tukifanya kazi kama timu, mtafanya operesheni Kariakoo ikibainisha watu wote ambao wanafanya biashara kinyume na taratibu hizi.”
Awali akisoma mapendekezo ya kamati kwa Waziri Jafo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Lwoga alisema kamati imeshauri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Ajira na watu wenye Ulemavu, iandae sera ya maendeleo ya sekta binafsi.
“Uandaaji wa sera hii utasaidia kuratibu wa konfani za sekta binafsi na kukuza ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta ya umma, kutasaidia wanachama wanajiunga uanachama wa pamoja na itasaidia upatikanaji wa biashara na masoko elimu na ushauri wa kibiashara,” amesema.
Pia ameshauri kuwanizishwa kwa mfumo kwa ajili ya kuwapa wafanyaniashata mikopo ya muda mrefu na yenye riba nafuu.
Ameshauri pia Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) kuanzisha mfumo ulioanishwa katika Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kitaifa namba 16 ya 2004 kwa ajili ya kukopeshja wafanyabiashara wazawa kwa muda mrefu na riba nafuu.
Pia Benki Kuu ya Tanzaina inashauriwa ifanyie kazi suala la mikopo ya muda mrefu na kwa riba nafuu ili kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wazawa kushindana sokoni.

Soma: Ni kama masihara hivi lakini polepole Mikocheni na Masaki zinaenda kutawaliwa na Wachina
TakwimuTakwimu zinaonyesha kuwa China ndiyo mbia namba moja wa biashara na uwekezaji nchini, kumekuwa na mchanganyiko wa mawazo juu ya wingi wa raia Taifa hilo namba mbili kwa uchumi duniani.

Waziri Suleiman Jafo aiagiza idara ya uhamiaji kuanza mara moja operesheni maalum ya kuwaondoa wafanyabiashara haramu wa kigeni Kariakoo
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Suleiman Jafo, ameagiza kuanza mara moja kwa operesheni maalum ya kuwaondoa wageni wanaofanya biashara kinyume na taratibu katika soko la Kariakoo, jijini Dar es Salaam. Soma pia: Waziri wa Biashara Selemani Jafo aunda kamati kwa ajili ya kuchunguza utitiri wa...