Kufungwa kwa uwanja wa uhuru

kichenchele

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
539
176
Inaniwia vigumu sana kuelewa dhana nzima ya hawa wahusika wanaoendelea na mchakato wa kuufunga uwanja wa uhuru eti usitumike tena kwani utafanyiwa marekebisho, hivi walikuwa wapi kipindi ligi imeisha? Kama wanania ya dhati ya kufanya marekebisho ya viwanja takwimu zao kweli zinaonyesha ni uwanja wa uhuru tu wenye hali mbaya? Acheni usumbufu
 
Walikuwa wapiga mahesabu ya mapato na matumizi yao kwa msimu ulioisha sasa ndio wamemaliza wanataka kufanya ukarabati ili waweze kuutumia tena msimu ukifika kati :glasses-nerdy::glasses-nerdy:
 
Ni ishara kuwa kila timu iwe na uwanja wake mzuri unaofaa kwa mechi za ndani na za kimataifa. Sio kukalia majungu na ufisadi tu!
 
Ni ishara kuwa kila timu iwe na uwanja wake mzuri unaofaa kwa mechi za ndani na za kimataifa. Sio kukalia majungu na ufisadi tu!
Japo lengo huenda lisiwe kama tunavyodhania lakini hizi timu zinazotumia huo uwanja zinatia aibu,uwanja haujaanza kufungwa leo,na wangekuwa ni watu wa kufikiri sasa wangeshakuwa na viwanja siku nyingi kwa mfano Simba na Yanga wanaweza kuweka tofauti zao pembeni wakashirikiana kutafuta wabia wengine wakakodi uwanja (e.g Tanganyika parkers) hata kwa miaka 10 wakaukarabati ili wautumie kwa mechi za ligi tu,hatua kwa hatua wanaweza kujikwamua na kuondokana na adha hii. Hata Ulaya kuna timu hazina viwanja ila zimeingia mikataba ya kuvimiliki na kuvitumia ktk mechi zao.
 
Back
Top Bottom