Kufungwa kwa uwanja wa uhuru msimu wa ligi

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,269
4,569
Tokea ligi ya Vodacom ya mwaka jana kumalizika hadi kuanza ligi ya 2010/11 kulikuwepo na muda wa kutosha kukarabati viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya ligi ya Vodacom. Uongozi wa uwanja wa Uhuru haukufanya hivyo badala yake msimu wa kuanza ligi (msimu wa mavuno) ndipo wanafunga uwanja kwa ukarabati. Kwa mwenye akili timamu huwezi kupanga kufanya ukarabati msimu wa mavuno. Ingekuwa busara mara ligi ya mwaka jana ilipomalizika wangefunga kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayofuata. Vile vile hainiingii akilini timu za Dar kutafuta viwanja vingine wakati kuna Uwanja wa Taifa. Jee uwanja wa Taifa ukikaa bila kutumika unapanda thamani? au gharama za uendeshaji hazitakuwepo?
 
Back
Top Bottom