Mpambanaji K
Member
- Dec 29, 2008
- 84
- 6
Watanzania wenzangu,
ninaandika hoja yangu huku nikiwa na majonzi tele kuhusu hatima ya elimu yetu Tanzania.
Inaonekana wazi kuwa viongozi wa chuo na serikali imeamua kwa makusudi watoto wa masikini wasisome Tanzania?nyie mwaonaje?
Naomba kuuliza wandungu wangu, hivi hatima ya Tanzania inaelekea wapi? ninamaanisha? serikali kutelekeza jukumu lake la kutoa elimu kwa wanannchi wake ni nini?
Naomba kuuliza wandungu wangu, hivi hatima ya Tanzania inaelekea wapi? ninamaanisha? serikali kutelekeza jukumu lake la kutoa elimu kwa wanannchi wake ni nini?
Ndiyo haya tulikuwa tunaongelea kule kwenye polygamy; wazazi wengi nchi hii wanajua kuzaa na serikali itunze; ni kweli kuwa serikali ni wazembe kiasi kikubwa; lakini wazazi wa Tanzania hata wale wanafunzi (walengwa) hutegemea serikali mno! This issue must be managed otherwise sioni kama tutaendelea hivi kuwa na serikali ambayo inashindwa kusaidia wanafunzi wake; na wazazi wengi ambao hupenda kuzaa na kuto-invest kwa watoto wao.na pia tujiulize, ni nini jukumu la wazazi/walezi kuwapatia watoto wao elimu?
Interested Observer umekosea kidogo unapo sema wazazi wengine kazi yao ni kuzaa tu wakingojea serikali iwasomeshee. Serikali ni nani?? Inasomeshea pesa za nani??? Ni kodi zetu sote watanzania (direct taxes and inderect taxes). Wao wamepewa jukumu la kukusanya na kupanga matumizi na kusimamia utekelezaji wa matumizi hayo.
It's our monies full stop.
Je, serikali isomeshe watoto wa walala hoi, so ifanyie nini hizo pesa???? Iwalipe akina Wakili mkono??? inunulie magari ya kifahari??? Watanulie mawaziri na maofisa wengine wa serikali??? Watajirikie viongozi na maofisa wengine wa serikali ambao baada ya miaka michache ya kazi ya kiutumishi au kisiasa wawe matajiri wa majumba mengi ya kifahari, magari mengi ya kifahari, na mipesa mingi wakaifije akaunti za kigeni kama akina Chenge????
Pesa yote iliyokwenda Meremeta, Deep green, n.k. isinge wezesha kusomesha watoto kwa kiasi kikubwa????
Ni kweli kuzaa bila mpango haitatusaidia. Lakini pia hata nchi nyingi zilizo endelea hawajawaachia wazazi tu suala la elimu. Fanya utafiti na utaelewa.
Hivi Nyerere wakati anawasomesha watanzania bure wakati ule zile pesa alikuwa anazitoa wapi?
Nsololi umeeleza vizuri kabisa na nakubaliana nawe.Kama elimu ingekuwa priority ya serikali yetu basi hakuna mwanafunzi angeachwa.Pesa ipo isipokuwa inatumika katika vipaumbele hasi.
Mtarajiwa ;
Ifuatayo ni jibu la swali lako!
1. Inawezekana sana kusomesha watu hadi University bure... ingawa bure yenyewe inategemea unaangalia kutoka engo gani?
*Vijana waliovijiweni wakifanya kazi wote au at least 75% na kuzalishia taifa, alafu wakajisikia wazalendo na wakalipa kodi*Wenye majumba ya kukodisha wakilipa kodi*Wenye biashara wakalipa kodi kwa kiwango kile kile ambacho mfanyakazi analipa*Wafanyakazi wa serikalini wakaondoa marurupu yasiokatwa kodi, badala yake yawekwe kwenye mishahara na kukatwa kodi*Kwa ujumla wetu tukibalika tukaona fahari kulipa kodi sio sasa asiyelipa kodi ndiye shujaaTutaweza kufanya mengi.
2. Namna ya pili kodi zisilipwe kama ilivyo sasa na kila mtu abebe mzigowake mwenyewe. rejea msemo wa . C.D. Msuya. yaani mkusanye kodi kidogo, hivyo hamuwezi kutoa huduma za kijamii... ati ukipiga mkwara record za ukusanyaji zinapanda... ukitulia ukasanyaji kodi unakuwa wa chini... taifa gani hili?
Nyerere alitumia ya njia ya 1.... kumbuka kulikuwa na kodi ya maendeleo pia na wananchi walikuwa wakilipa... Mashirika na viwanda vilikuwa vikilipa kodi
Siku hizi kuna mtu hajui kodi ni nini? ati kuna wanasamehewa 100%..kisa mishahara yao ni chini ya 100,000/-. that is wrong! kodi inatakiwa akatwe kila mtu hata kama itakuwa kama token tu... inabidi aelewe kwamba kuna kitu kinaitwa kodi.
Sisi tunatumia hiyo njia ya 2.
Nilichokiona juu ya wanafunzi hao 2000 ni wenyewe kuamua ama kwa kutaka au kwa bahati mbaya kutoendelea na chuo.Walitangaza mtu ambaye hatajaza form atakuwa amejiondolea haki ya kusoma pale. hawa hawakujaza so wameamua kutoendelea na chuo. Waliopewa musa mpaka alhamisi ni waliojaza lakini hawakulipa ada yote wanayodaiwa. still inaonyesha nchi yetu elimu ni kwa walionacho.