Kufukuza wafanyakazi hewa si kazi ya Mkuu wa Mkoa

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Salaam wanajamvi,

Nimekuwa nikifuatilia habari ya sasa ya mjini kuhusu utumbuaji wafanyakazi hewa.Si rahisi kwa Mkuu wa Mkoa kujua idadi na aina ya wafanyakazi wa serikali.Kazi hiyo ni mahsusi kwa Maafisa Rasilimali watu ambao kimsingi ndio walitakiwa kutumbuliwa.

Wanawajua wafanyakazi wote waliostaafu na waliokufa au kufukuzwa.wengine wanaotakiwa kuwajibishwa ni watunza Hazina wa Halmashauri na wahasibu kwa kuwa ndio walipaji.

Kuwabana Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni kuwaonea.Kuhakiki wafanyakazi walio active ni majukumu ya kila siku ya watu niliowataja.
 
Wewe utakuwa mtumishi hewa,jisalimishe.
Ni vema kuelewa kwanza kabla ya kurukia mambo , ni hivi , kumfukuza kazi Dc au Rc na kuwaacha mameneja wa rasilimali watu na wahasibu ambao ni walipaji ni kujitafutia sifa za uongo , next time usikurupuke .
 
Binafsi nilisikitika sana kwa mama Kilango kutimuliwa kazi, japo sijawahi kuwa mshabiki wake wala wa chama chake ila niliona kama ilibidi yeye kufukuzwa ili magazeti yasikose cha kuandika juu ya utendaji kazi wa awamu hii, nasema hivyo kwanini, ni lipi kosa kubwa kati ya yeye kutokujua kuwa kuna watumishi hewa katika mkoa wake, tena mkoa ambao amefika hata mwezi haujaisha na kosa la yule waziri aliyetuma msg kwa yule mtumishi wa bandari akimuambia afungue bomba la kitu gani sijui (mtanisaidia) wakati waziri Mkuu alipotembelea huko bandarini, binafsi niliona hili la msg lilikuwa na udanganyifu mkubwa zaidi.........
 
mkuu ni valve za mabomba za kuhakiki kiasi cha mafuta kutoka kwenye meli.lile jipu limekaa sehemu nyeti.mhusika aliwahi kusema bungeni kuwa akitoboa yote anayoyajua kuhusu ESCROW nchi itatikisika.hii ndim Tanzania yetu!
 
Binafsi nilisikitika sana kwa mama Kilango kutimuliwa kazi, japo sijawahi kuwa mshabiki wake wala wa chama chake ila niliona kama ilibidi yeye kufukuzwa ili magazeti yasikose cha kuandika juu ya utendaji kazi wa awamu hii, nasema hivyo kwanini, ni lipi kosa kubwa kati ya yeye kutokujua kuwa kuna watumishi hewa katika mkoa wake, tena mkoa ambao amefika hata mwezi haujaisha na kosa la yule waziri aliyetuma msg kwa yule mtumishi wa bandari akimuambia afungue bomba la kitu gani sijui (mtanisaidia) wakati waziri Mkuu alipotembelea huko bandarini, binafsi niliona hili la msg lilikuwa na udanganyifu mkubwa zaidi.........
Mimi mwenyewe ni adui wa kila mwanaccm lakini namna yule mama alivyodhalilishwa nimeona aibu sana .
 
Back
Top Bottom