Leo kajeruhiwa Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chadema,
Mh.Mbilinyi. Wengi wanamjua kama Sugu.kufuatia vurugu zilizotokea Bungeni leo mchana baada ya nAibu Spika wa Bunge Mh.Jobu Ndugai, kuamuru maaskari wamtoe nje Kiongozi wa kambi ya upinzani mh.Freeman Mbowe,kufuatia kukaidi amri ya nAibu spika wakati alipo ambiwa akae chini,Akagoma kutii kauli hiyo.
Katika purukushani za kumtoa nje mh.Mbowe ndipo alipo jeruhiwa kiasi na damu zikamtoka.
Sasa je? kufuatia Vurugu hizo,kuna haja ya vikosi kama Red Brigade,Green Guard,Blue Guard,kuwepo nje ya Geti la Bunge ili kuwalinda Viongozi wao wa Vyama?