manyoda
Member
- Dec 16, 2010
- 64
- 23
Habari ndugu zangu!
Katika mambo ambayo watu wa kisasa tumekosa, hasahasa wakazi wa jiji la Dar, jiji la foleni ni kukosekana kwa muda wa kutafakari. Hii pia inaendana na kujengeka kwa tabia ya kufanya mambo bila kufikiria kwa umakini na undani juu ya jambo hilo....manufaa na madhara yake!
Hali hii inazidishwa sana na maendeleo ya kisayansi na teknolojia tuliyokuwa nayo kwa sasa, hasa mitandao na simu za mkononi zinazoruhusu mitandao "smartphones". Mambo haya yametushughulisha sana kiasi cha wengi wetu kukosa walau dakika ishirini ndani ya masaa 24 kutafakari, hasa masuala mbalimbali muhimu yanayomzunguka yeye binafsi na hata jamaa zake wa karibu, wakiwepo wazazi na ndugu kwa mfano.
Kwa muktadha huu niwakumbushe wana JF walio/tulio katika mkumbo huu kurudi nyuma kidogo na kujitathmini na kujirekebisha na kwa wale wenye tabia chanya ya kutafakari na kufanya maamuzi muhimu na mazuri kuendelea na utamaduni huu mzuri na wa kuigwa.
Nawasilisha