Kuficha na kuhifadhi sukari nini tofauti yake??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,119
Kila nikisikia taarifa ya habari ni kwamba imekatwa sukari tani kadhaa ya mfanya biashara mkubwa wa sukari!! sijaona sukari ikikamatwa kwa wakulima au wafugaji , maana yangu hawa ndio biashara yao na wana vibari!!
Iweje wawe wameficha??

Nani aliye waendea kuomba kuuziwa sukari akakataliwa?? Hili la kufichwa je hatujakalilishwa na serikali huku hii sukari ikiwa imehifadhiwa sehem husika!!

Yale maeneo iliko patikana sukari ni maeneo husika na sio sehem ya mabanda ya ng'ombe ili tuingie shaka iweje sukari kuwekwa mabanda ya kuku??
Swali mfanya biashara mkubwa yukoje ??
Anatakiwa awe na vigezo gani??

Majibu kirahisi awe na mtaji mkubwa na stoo za kuhifadhia bidhaa husika pasi na vibali!!

Je hawa wafanya biashara walificha sukari au iko sehemu husika inapohifadhiwa sikuzote??

Na je ? Muda gani kisheria mtu anakua anahesabika ameficha sukari??

Je tani zaid ya 30 elfu zilizo kamatwa zimezalishwa ndani ya mwezi mmoja na nusu na viwanda vyetu vya ndani?? Maana tangazo la kusitisha kuingiza sukari limetolewa na raisi wetu mwez much mwaka huu tarehe 8 je viwanda vyetu vimezalisha na kuuuza zaid ya tani 70 elfu kwa mwez mmoja na nusu zingatia nyingine imeendelea kutumika nakuwa mikonon mwa watumiaji! Kama ndio hivo hakuna haja ya kusema viwanda vyetu haviwez kuzalisha tani lak 6 maana kwa kwa hesabu hiz wanaweza

Je hawa wafanya biashara ikiwa sukari wamenunua muda mrefu kabla hata ya tangazo la raisi iweje wawe wahujumu uchumu?? Siamini mwezi mmoja na nusu unatosha kumwita mtu ameficha huku serikali ilikua na shehena yake iliosema ipo na hawatwambii iko wap!!
Hoja yangu serikali inawaonea wauza sukari sana tena sana!! Hii athari zake zitayumbisha wa wafanya biashara na nchi yetu maana hawatahifadhi sukar gharan zaid ya wachuuzi kuwa ndio wateja wa viwanda !!
Hii itakua athari kwa viwanda pind vitakapo anzisha uzarishaji kwa kuhofia kununua sukar na kuja kunyang'anywa.

Je ikiisha hii tunayowanyang'anya nini kifuatacho maana sukari itakua hamna na uzalishaji umesimama.

Chonde chonde tutafute suruhu ya kudumu kuliko njia hiz za kutafuta sifa kwa kuwaumiza hawa wafanya biashara, na tunawaumiza kwa muda maana nina uhakika tutawalipa hawa mpaka akili itatukaa sawa !!
Viongozi wakili wao ndio walikosea kwa kuzuia uagizaji, huku viwanda havifanyi kazi na hawakua na uhakika na stoko yoyote. Dawa ni kuagiza kwa wingi ili bei ishuke yenyewe na si kwa amri ambayo haijawahi kutekelezwa (1800)

sema kwa vile viongoz wetu hawatakuja kutuambia tukikosea na sasa hela zenu tunawalipa tena wale tuliowaita waovu.

Mungu tuepushie haya mabalaa yasidi kuongezeka Tanzania yetu itafirisika!
 
kila nikitafakari hiki swala sijui viongozi wanatupeleka wapi? haiingii akilini KBS,
 
Mwenyewe kasababisha uhaba wa sukar sasa anaanza kuwavuruga wafanya biashara. Nani wakumwambia kuwa uamuzi wake ulikuwa wa kukurupuka. Naiona nchi yangu inaenda kuingia shimoni. Eti wanahujumu uchumi. Loh hili janga
 
Hivi kama mtu ana tani zote hizo na wanasema sukari haipo wana maana gani? Sukari imepotea kwa mpango. Halafu tuseme hakuna sukari. Nchi hii kwa fikra hizi itachelewa sana kuendelea
 
Kila nikisikia taarifa ya habari ni kwamba imekatwa sukari tani kadhaa ya mfanya biashara mkubwa wa sukari!! sijaona sukari ikikamatwa kwa wakulima au wafugaji , maana yangu hawa ndio biashara yao na wana vibari!!
Iweje wawe wameficha??

Nani aliye waendea kuomba kuuziwa sukari akakataliwa?? Hili la kufichwa je hatujakalilishwa na serikali huku hii sukari ikiwa imehifadhiwa sehem husika!!

Yale maeneo iliko patikana sukari ni maeneo husika na sio sehem ya mabanda ya ng'ombe ili tuingie shaka iweje sukari kuwekwa mabanda ya kuku??
Swali mfanya biashara mkubwa yukoje ??
Anatakiwa awe na vigezo gani??

Majibu kirahisi awe na mtaji mkubwa na stoo za kuhifadhia bidhaa husika pasi na vibali!!

Je hawa wafanya biashara walificha sukari au iko sehemu husika inapohifadhiwa sikuzote??

Na je ? Muda gani kisheria mtu anakua anahesabika ameficha sukari??

Je tani zaid ya 30 elfu zilizo kamatwa zimezalishwa ndani ya mwezi mmoja na nusu na viwanda vyetu vya ndani?? Maana tangazo la kusitisha kuingiza sukari limetolewa na raisi wetu mwez much mwaka huu tarehe 8 je viwanda vyetu vimezalisha na kuuuza zaid ya tani 70 elfu kwa mwez mmoja na nusu zingatia nyingine imeendelea kutumika nakuwa mikonon mwa watumiaji! Kama ndio hivo hakuna haja ya kusema viwanda vyetu haviwez kuzalisha tani lak 6 maana kwa kwa hesabu hiz wanaweza

Je hawa wafanya biashara ikiwa sukari wamenunua muda mrefu kabla hata ya tangazo la raisi iweje wawe wahujumu uchumu?? Siamini mwezi mmoja na nusu unatosha kumwita mtu ameficha huku serikali ilikua na shehena yake iliosema ipo na hawatwambii iko wap!!
Hoja yangu serikali inawaonea wauza sukari sana tena sana!! Hii athari zake zitayumbisha wa wafanya biashara na nchi yetu maana hawatahifadhi sukar gharan zaid ya wachuuzi kuwa ndio wateja wa viwanda !!
Hii itakua athari kwa viwanda pind vitakapo anzisha uzarishaji kwa kuhofia kununua sukar na kuja kunyang'anywa.

Je ikiisha hii tunayowanyang'anya nini kifuatacho maana sukari itakua hamna na uzalishaji umesimama.

Chonde chonde tutafute suruhu ya kudumu kuliko njia hiz za kutafuta sifa kwa kuwaumiza hawa wafanya biashara, na tunawaumiza kwa muda maana nina uhakika tutawalipa hawa mpaka akili itatukaa sawa !!
Viongozi wakili wao ndio walikosea kwa kuzuia uagizaji, huku viwanda havifanyi kazi na hawakua na uhakika na stoko yoyote. Dawa ni kuagiza kwa wingi ili bei ishuke yenyewe na si kwa amri ambayo haijawahi kutekelezwa (1800)

sema kwa vile viongoz wetu hawatakuja kutuambia tukikosea na sasa hela zenu tunawalipa tena wale tuliowaita waovu.

Mungu tuepushie haya mabalaa yasidi kuongezeka Tanzania yetu itafirisika!

Huu ni mtihani tu...watu wamekosea katika mkakati lakini wanataka kuaminisha kuwa tatizo ni la wafanya biashara.Sukari haipo viwandani na hiyo 'ilofichwa'ikitolewa yote basi kama haikuingia nyengine wiki hii kutakua hakuna sukari.
tuje katika mada yako...naweza kuijibi sasa hivi ukienda katika maghala ya hawa hawa wa sukari basi utakuta Mchele kwa wingi , utakuta sabuni kwa wingi, utakuta mafuta ya kupikia kwa wingi, utakuta dawa za maeno, na bidha nyengine zimejaa maghalani kwao..hio ndio biashara ya distributor/Msambazaji .
wazambazaji hawezi kuwa na gunia mbili za sukari au mchele..hata wenye viwanda wanataka watu wenye muscles kununua kwa wingi na siku zote hawafichi ila wanahifadhi...
 
Kumekuwa na ukanganyiko kwa walio kutwa na stock kubwa ya sukari katika kipindi cha uhaba.Kuna tofauti yoyote kisheria yawalio kamatwa na sukari wameficha au wamehifadhi?

Nani vipi tunaweza kutofautisha nani kaficha na nani kahifadhi?

Kwa mtazamo wangu: Mfano, familia mbili zinaishi nyumba moja wakakubaliana siku ya sherehe wote wagawe soda kwa watoto. Familia moja ikagawa soda zao zote lakini familia ya pili ikabakiza soda kwenye fridge yao na baadhi ya watoto hawakupa soda na wakaambiwa hakuna soda. Hii familia ya pili ni IMEFICHA soda hata kama ziko kwenye fridge.

In that sense, haijalishi kama magodauni yako yanajulikana ni UMEFICHA.
 
Tunaambiwa imefichwa kwa kuwa haionekani inapotakiwa kuonekana, lakini ingekuwa inaonekana madukani isingefuatwa huko kwenye maghala na hapo ndio kwenye utata wa neno kuficha, ingekuwa inapatikana kwa wingi mjini ungeambiwa umehifadhi.
 
Sasa wakati kutumia ASALI kama mbadala wa SUKARI umefika. Asali ina dorola masokoni
 
Kumekuwa na ukanganyiko kwa walio kutwa na stock kubwa ya sukari katika kipindi cha uhaba.Kuna tofauti yoyote kisheria yawalio kamatwa na sukari wameficha au wamehifadhi?

Nani vipi tunaweza kutofautisha nani kaficha na nani kahifadhi?

Kwa mtazamo wangu: Mfano, familia mbili zinaishi nyumba moja wakakubaliana siku ya sherehe wote wagawe soda kwa watoto. Familia moja ikagawa soda zao zote lakini familia ya pili ikabakiza soda kwenye fridge yao na baadhi ya watoto hawakupa soda na wakaambiwa hakuna soda. Hii familia ya pili ni IMEFICHA soda hata kama ziko kwenye fridge.

In that sense, haijalishi kama magodauni yako yanajulikana ni UMEFICHA.

babu M,
Mfano uliotoa ni mzuri sana, ili utumike hapa tunahitaji kuthibitisha;
1. Kwamba hawa wafanyabiashara hawakuwa wanauza sukari kwa wateja wao (siyo kwamba walikuwa wanauza kidogo kidogo)
2. Kwamba kuna mteja (mmoja au wengi) aliyeambiwa kuwa sukari hakuna.
 
Mwenyewe kasababisha uhaba wa sukar sasa anaanza kuwavuruga wafanya biashara. Nani wakumwambia kuwa uamuzi wake ulikuwa wa kukurupuka. Naiona nchi yangu inaenda kuingia shimoni. Eti wanahujumu uchumi. Loh hili janga
Lazima mtumie mpaka Asali ,kudadadeki . Wodi za wagonjwa wa kisukari zitapungua mwaka huu
 
Hapa wala haiitajiki science yoyote ile, sasa hivi kuna uhaba wa sukari na bei imepanda, ila locha ya kuwa na huo uhaba wa sukari, bado kuna watu ambao walipewa kibali cha kuuza sugari "wanahifadhi" hiyo sukari!
 
Mwenyewe kasababisha uhaba wa sukar sasa anaanza kuwavuruga wafanya biashara. Nani wakumwambia kuwa uamuzi wake ulikuwa wa kukurupuka. Naiona nchi yangu inaenda kuingia shimoni. Eti wanahujumu uchumi. Loh hili janga

huna nchi hii, watanzania hakuna wajinga kama wewe
 
Suala La Sukari Ni Uhujumu Uchumi na Kuitest Mamlaka ya Mungu Tanzania. Sukari ilikuwapo. Rais alipotangaza kuagiza mwenyewe basi ikapote na hata iliyopo bei ikapanda. Sasa hivi hata retailer wanaogopa kununua Sukari maana ni Ghali huko kwa wholesaler.

Sukari Ipo Maghalani Sema Imepandishwa bei makusudi kumkomoa Rais. Waache wacheze na Maisha yao. Ila wakumbuke Mamlaka hiii imewekwa na Mungu.
 
Heading ilipasa iwe kuhodhi na si kuficha. Kuhodhi ni kuzuia kuuza bidhaa fulani ilhali kuna uhaba wa bidhaa hiyo sokoni. Kuhodhi ni kosa la uhujumu uchumi. Jamani, Kiswahili ni lugha yetu, nashangaa tunapopungukiwa msamiati kiasi hiki halafu tunapoteza muda kulumbana. Kuficha- to hide; kuhodhi- hoarding. Ok?
 
Back
Top Bottom