ENANTIOMER
JF-Expert Member
- Sep 22, 2014
- 1,419
- 804
nimeangia huku nikajua kuna mambo ya msingi, kumbe mtoa mada haharisha barabarani. yaani unaongea swala la kuwawajibisha wakuu wa shule, huku unaacha kuongea swala la kuiwajibisha serikali kwa kugoma kuajiri walimu waliomaliza elimu yao tangu mwaka juzi. kwanini usinyumbue akili na ukaona kama serikali yetu mbovu nayo inasababisha shule zetu za umma kuendelea kufanya vibaya kutokana na kuendelea na msimamo wao mchafu wa kuwasomesha namba watoto wa wanyonge kwa kutowapatia walimu wa kuwafundisha!!!Matokeo mabaya kwa shule za serikali angalieni wakuu wa shule wengi ni wabovu na sio wabunifu wanashindwa kuwasimamia walimu wao hivyo serikali m-deal na hawa wakuu pia ikiwezekana muwachague walimu wa sayansi wawe wakuu wa shule.
enzi hizo shule za umma zilikua poa kulinganisha na za binafsi kwasababuShule za serikali enzi zetu zilikuwa best
hii kauli ni mbaya sana na ndiyo inayotumika kuwatesa walimu. halamshauri nzetu na serikali yetu, Mungu anawaona jinsi kwa jinsi wanavyowatesa walimu wetu, hali inayopelekea kuwashusha moyo wa kutufundishia watoto wetu, na hatimae watoto wetu wanarudi na sifuri wakati tuliuza ngimbe wakasome. usirudii tena kuongea kauli mbaya kama hiiWaalim ni wito sio kaz
Mkuu;
Natofautiana nawe kwa mengi tu. Huwezi niambia kuwa kwa sababu wanafunzi wengi huingia kidato cha kwanza kwa kufaulu kwao wengi ndio kunawafanya wafeli. Unataka kusema hakuna hata mmoja tu mwenye kuelewa?? Nadhani sema kuwa waalim wengi hawana wito. Wengi wamekuja kufanya kazi zao na wale wenye wito wa hiyo kazi ndo hao hukimbilia private kwa sababu wanasikika sifa zao hivyo hutwaliwa private chap chap.
Waalim ni wito sio kazi. Mwenye wito anacho kipaji cha kufundisha. Kama umeenda kufanya kazi hutakaa ueleweke. Kwa sababu unaangalia saa ukutani 45 min zako ziishe utoke. Unakopi skim ili kuwafurahisha wakaguzi.
Mkaguzi mwenyewe hana usafiri wa kufika huko uliko mara kwa mara.
Serekali; Badala ya kuwatumbua waalim wakuu, tafuteni waalim wenye wito sio wasaka ajira. Haiwezekani mwalim ufundishe mwaka mzima halaf wasikuelewe na mwakani uendelee. Huna wito.
Hivi unajua mwalimu wa Serikali wanavyonyanyaswa kupata haki zake,? Hivi unategemea darasani atafundisha akiwa na saikolojikale nzuri? Nyumbani kuko hivyo,Anaidai serikali haitaki kumlipa, Madaraja haimpandishi kwa wakati na wakati mwingine yanapandishwa kwa upendeleo, Mfano ninao ushahidi wa waalimu watatu shule ya kijijini waliajiliwa 2011 Hadi sasa hawajawahi kupanda daraja, Hawana kesi yoyote na wanafanya kazi izuri lakini hawathaminiwi,Sasa unamtaka Mkuu wa shule awasimamie nini? Waliopo halmashauri kutwa nzima wapo kwenye vikao visivyoisha tena vyenye kulipana posho, Je ni lini waalimu wamefanya vikao shuleni kwao wakajilipa posho? Polisi kila tarehe 15 Anapewa Ration ya chakula, 400000, Mwalimu kila tar 15 Anapewa nini? Acha kuropoka, Funga mdomo kama hujui chanzo cha tatizo
Police hawahawa tunaonunua wote michicha na tembele mtaani ndo wapewe miposho hiyo acha utani wwHivi unajua mwalimu wa Serikali wanavyonyanyaswa kupata haki zake,? Hivi unategemea darasani atafundisha akiwa na saikolojikale nzuri? Nyumbani kuko hivyo,Anaidai serikali haitaki kumlipa, Madaraja haimpandishi kwa wakati na wakati mwingine yanapandishwa kwa upendeleo, Mfano ninao ushahidi wa waalimu watatu shule ya kijijini waliajiliwa 2011 Hadi sasa hawajawahi kupanda daraja, Hawana kesi yoyote na wanafanya kazi izuri lakini hawathaminiwi,Sasa unamtaka Mkuu wa shule awasimamie nini? Waliopo halmashauri kutwa nzima wapo kwenye vikao visivyoisha tena vyenye kulipana posho, Je ni lini waalimu wamefanya vikao shuleni kwao wakajilipa posho? Polisi kila tarehe 15 Anapewa Ration ya chakula, 400000, Mwalimu kila tar 15 Anapewa nini? Acha kuropoka, Funga mdomo kama hujui chanzo cha tatizo
kama hujui na hilo kwasasa, basi ukale malimao. kwa taarifa yako polisi kwasasa wako vizuri. stori ulizohadithiwa hapo zamani, ambazo ndizo umekuja kutuhadithia leo, sio za kweli kwasasa. polisi wako poa kwasasa huku walimu wakiwa na njaa kali.Police hawahawa tunaonunua wote michicha na tembele mtaani ndo wapewe miposho hiyo acha utani ww
Enzi zenu hizi shule 10 bora zilikuepo?Shule za serikali enzi zetu zilikuwa best
Mmmmmh, ndugu. Unaongelea wito dunia ya leo? Yaani mtu apoteze miaka akisaka elimu, atumie resources za wazazi, alipie mkopo wa heslb indefinitely halafu unasema akafundishe kwa wito? Hapana ndugu hizo zama zimepita. Hawa hawa waalimu wasaka ajira(kama unavyowaita) wapewe incentives za kutosha , na mazingira ya elimu yaboreshwe kwa ujumla wake utaona matokea.
Umeongelea pia kuhusu suala la angalau hata wachache wangeonekana wamefaulu katika darasa husika. Ndugu yangu kama umesoma unajua hali inakuwaje unapokuwa kwenye darasa lenye ushindani wa watu wengi wenye uwezo. Automatically hautazembea, ni wazi nawe utajitahidi tu. Lakini kama waliodahiliwa ni wa ufaulu wa chini kama ilivyo siku hizi , hata wakiwemo wawili wanojitahidi watafeli tu kwa kuwa wapo kwenye wingi wa wenzao wasio na uwezo, hivyo kukosa ushindani na kurelax. Mfano enzi zetu sisi kufaulu darasa la saba haikuwa mchezo. Unakuta kata nzima au tarafa anafaulu mmoja tu na mwenye uwezo kweli. Sasa huyo anaenda kukutana na wenye uwezo wenzake, sikilizia moto wake hapo. Wala walimu hawakuwa na kazi sana. Lakini kwa ufaulu wa leo wa darasa la saba kumlaumu mwalimu ni kumuonea. Na pia kulinganisha matokeo ya sasa na ya hapo nyuma ni statistically insignificant.
kwahyo wew unaona ni sawKwani kuna siku shule za serikali ziliwahi kufaulisha kuliko shule za private..!?