Kufahamu mambo yako hapa: Ramli ya kutizama mambo unayotaka

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
5,001
4,551
Katika makala hii kama unataka nikutizamie mambo yako:

1091790

hii ni kwa wale wanaohitaji kutazama mambo yao ikiwemo,
Haoa tutaweza kutizama:
  • Nyota yako,
  • Bahati yako,
  • Kipato chako,
  • Nyumba yako na mizimu yako,
  • Kizazi chako na mali yako na ushindi wa kamari
  • Maradhi na afya yako,
  • Mahusiano na ndoa yako,
  • Kama umefanyiwa madawa aina ya kifo(sikushauri)
  • Safari yako ya maisha na mafanikio yako(ndoto zako)
  • Kazi yako na biashara yako au ulezi wako
  • Marafiki zako na msaada wako
  • Adui wa kisiri kuangalia uchawi,mikosi,nuksi,gundu n.k
Kupitia milango yako yote 12 kwa karata,shikeli,kikombe cha kahawa,kiganja cha mkono, na aina yoyote pia kwa usulil hikmat na ramli ya milango 12/nyumba 12 pamoja na kufahamu yote yanayohusiana na malengo ya maisha pamoja na betting na kujua kama wewe upo sahihi katika fani ya kubet na siku maalum na muda maalum wa kufanya betting, au kutafuta kazi,pesa na mapenzi na kuangalia ni zipi nguvu zako za miujiza.

au kufanikisha mambo unayoyataka kwa muda sahihi na kwa mtu sahihi au sehemu sahihi au kufahamu jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokusumbua katika kaisha kulingana na milango hii,kwa wanaohitaji pia kupata jambo linachelewa kujua ufanye nini karibuni na mengineyo mengi yanayohusu miujiza yako karibuni.

Katika kipindi kilichopita nyuma yaani maisha ya nyuma huko kwenye nyakati za kibabiloni wasoma nyota walichanganua haya mambo mengi katika miongozo ya watu wao. wao walijaliwa na kupewa uwezo na Mwenyezi Mungu na kufundishwa elimu pana ya ulimwengu na wengi wao wakakufuru na pia walifundishwa yanayosibu watu na kuyafahamu kuwa katika safari ya mwanadamu kuna mgawanyiko wa milango 12 tu ambayo ukiitanua humo utapata kila hatua ya maisha ya mwanadamu kama vile mihemko ya kazi,tamaa,matumaini,ndoto na mahusiano uwezo n.k

Basi watu hao wasoma nyota wa kibabiloni waliamua kugawanya maisha ya mwanadamu baada ya kuyasoma kwa kipindi kirefu ndipo wakagawanya matukio ya maisha ya mwanadamu katika milango 12 tu na hakuna mganga,tabibu au mchawi anaeweza kukusomea chochote kile kwenye rada zake bila kutumia milango hii 12 wote wanatokea hapa kwa elimu zinazozidiana lakini wengi wao ni waongo.

Katika magawanyo hayo 12 ndio wakaamua kuita milango ya nyota/nyumba za nyota au ramli n.k, basi humu yamegawanyika na kuna mlango wa mtu nyumba yake au nyumbani, mlango wa utajiri binafsi,mlango wa ndoa, mlango wa kazi n.k

Hapa ili niweze kukutizamia nitahitaji kufahamu nyota yako iliyochomoza wakati unazaliwa achilia mbali hizi nyota za magazetini mnavyosemewa viseversa unakuta mtu unaambiwa leo siku mbaya kwako halafu unakuta hakuna siku nzuri mfano wake lazima utaona nyota ni utapeli tu wa watu na sanaa tungo.

nyota zote 12 zinaweza kuwa na sifa zinazofanana kwako kiasi kwamba kila nyota ukisoma unakuta kuna kitabia cha nyota hiyo unacho kulingana na siku na saa,

Baada ya kuifahamu nyota yako iliyochomoza wakati unazaliwa ndio nitaiunganisha na nyota hizo za magazetini pamoja na jina lako na la mama ndio kuweza kupata nyota tatu ambazo zitakuwa katika tabia moja yaani kama moto,maji,upepo na udongo baada ya kuipanga vema na kuijua basi ndio tunapata nyota yako sahihi na kujua tukio unalotaka kujua lipo wapi na vipi unaweza kuliweka unavyotaka.

Hii ndio milango 12 nitakayo zungumzia hapa na ukihitaji nitakutizamia na kuangalizia kati ya machaguo yako au kama utahitaji kujua yote basi pia naweza kukutizamia ni wewe na jinsi utakavyohitaji:

1: MLANGO WA KWANZA: Binafsi
1091941

huu ni mlango binafsi ambao unakuzungumzia wewe binafsi ni mlango wenye nguvu zaidi katika milango yote kwenye chart yako ambayo nitakusomea kwa sababu huu unakuwakilisha wewe na tabia zako,mitindo yako,akili yako,ujasiri na uwezo wako,

Huu mlango pia utazungumzia tabia yako ya nje kwa watu wewe ni wa aina gani,kipi unapenda kipi, hupendi kipi ufanye kipi usifanye,na watu wanakuchukuliaje,muonekano wa sura yako, muda mwingine mlango huu huitwa mlango wa ubinafsi wako.

Unachotaka katika maisha yako na vipi unaweza kuja kukipata na njia gani upite ili kupata, kujua mlango huu wa kwanza vema utajua vipi ulianza ungepatia wapi na vipi umekosea au umekosea wapi na vipi unaweza kurekebisha.

Wengine huita mlango huu kuwa ni mlango wa Mwanzo wa muongozo mzima wa maisha ambapo mwanzo wa mtu kitu cha kwanza ni kujitambua na pia ni mlango unaoweza kumuelezea mtoto mchanga anaeanza kuijua dunia, mambo yote yanayokuhusu wewe binafsi tutayaona hapo. na pia matatizo ya kichwa ni katika mlango huu tu.

2: MLANGO WA PILI: Pesa na Umiliki
1091942

Huu unahusika na kile unachokipata kwenye maisha yako na vipi unaweza kupata zaidi au kutafuta na kipi utakachopata yaani kipato chako mtiririko wako wa pesa utapitia wapi,uhamaji wa umiliki wako vipi pesa au unachomiliki kitakuwa kikihama mambo utakayo kuwa unayafanya kwa kipato na jinsi unavyojihisi kipesa ukiwa nayo au hauna na vitu ambavyo unahitaji vikuzunguke karibu yako, pia utaona hapa nguvu yako ya kipato na uwezo ulionao wa kumiliki kipato chako, huu mlango unakuonyesha ni vipi unaweza kupata mafanikio katika maisha yako,na pia matatizo ya shingo ni hapo tu

3: MLANGO WA TATU: Mawasliano
1091943

Huu ni mlango wa mawasiliano ambapo huu tutatizama maeneo yanayokuzunguka kwa karibu katika sehemu tatu wewe binafsi,familia au ukoo wako na safari zako za kila siku huu utazungumzia jinsi unavyofikiria,kuandika,kumbukumbu,nguvu au kipaji ulichonacho elimu yako ya mapema uliyoipokea,kama unaweza kumudu siasa na mambo yote ya siasa kimaongezi uwezo wako wa kujifunza na kuelewa mahusiano yako na ndugu zako kama kaka na dada au binamu shangazi mjomba,jirani na wanaoishi jirani au ndanni kwako au kwenu safari fupi na gari ya kusafiria au kutembelea maelezo yake utayapata hapo, hasa safari za kazi au mambo ya kielimu, safari za kiserikali n.k
pia matatizo ya mikono ni hapo tu.

4: MLANGO WA NNE: Nyumba
1091945

Huu utazungumzia nyumbani kwenu kipindi cha maisha yako yaliyopita nyuma kwenu, pia mambo yaliyopita,yaliyopo na yajayo, inaonyesha aina ya maisha ya nyumbani kwenu uliyokuwa ukiishi na wazazi wako, unaweza kukileta nini katika maisha haya au kutumia nini katika maisha haya ambacho ulichukua kwa wazazi na kitakufanikishia vipi na pia unawezaje kumiliki ardhi au kiwanja au utapata vipi kumiliki ardhi, pia mlango huu utazungumzia miaka ya karibuni inayokuijia mbele, pia kinga unayotakiwa kutumia kutoka katika mambo ya kiroho, huu ndio mlango wa ajabu sana katika milango yote unawezaje kujiokoa na maisha haya kimwili na kiroho. pia matatizo ya kifua au maziwa ni hapo tu

5: MLANGO WA TANO: Mbinu na Sex
1091946

Ikiwa unataka kuangalia mlango huu basi utapata kujua jinsi gani unaweza kuonekana mwenye mbinu au unaweza kutumia mbinu zipi katika mafanikio ya kupata mali,kizazi au watoto utakao zaa na pia asili yako ya ufanyaji au mtindo wa ufanyaji sex, watoto wataishi vipi na wewe na vipi uwaweke katika hali nzuri vipi upate utajiri ambao hautahusu kuwazuru wao,kujifurahisha,sanaa,mambo ya kufurahisha roho sex mambo mapya ya kufanya kimaisha, ushindi wa kamali na michezo ya ushindani,betting n.k
Hapa tutatizama yote yanayohusiana na wewe mali zako zinatoka wapi na kwa nani au nini, na pia kizazi chako kinatatizo gani na jinsi ya kurekebisha n.k
matatizo ya moyo pia.

6: MLANGO WA SITA: Afya na Huduma
1091947

Hapa tutaangalia maradhi yako ni yapi au nini kinachokutokea mwilini usichokifahamu na njia za kujiponya ni zipi, kama umerogwa pia matatizo ya tumboni na pia utaangalia uliyemuajili au aliyekuajili ana heri kwako kama hana heri vipi unaweza kumuepuka pia nani anaweza kukuhudumia wakati unahitaji msaada ikiwemo mikopo,tiba kujengewa nyumba au kununuliwa gari,kusomeshwa n.k
hata matatizo ya tumbo,

7: MLANGO WA SABA: MAPENZI NA NDOA
1091948

Huu ni mlango pekee unaohusiana na mwenza uliyenaye au unaemchagua kama mke au mume na habari zake zipo hapo na aina ya ndoa utakayokuwa nayo either utaachika au kuacha na kuowa au kuolewa pengine na pia wenza au wapenzi utakaoshiliki nao ni yupi atakuletea manufaa na yupi atakuletea matatizo, hapa pia kutakuwa kunazungumzia mikataba mbalimbali baina yako na watu au partnership katika kazi biashara na mambo ya kisheria yote ni hapo, uwezo wako wa kufanya kazi na wengine kwa upendo na maadui wa wazi basi utawajua hapo kwa majina na vitendo vyao huu mlango upo kinyume na mlango wa kwanza huu unazungumzia watu wengine waliokitofauti au kinyume na wewe
Hapa tutaangalia pia mambo yote ya ndoa,mchumba,hawara,na mzinifu mwenzio kuna habari gani kuhusu yeye na anaweza kukunufaisha vipi,

8:MLANGO WA NANE: Kifo na Ufufuo
1091949

Huu ni mmoja kati ya milango ya ajabu (ambapo mingine ni wa nne na wa kumi na mbili) na nimilango migumu zaidi kuielewa maana inakwambia vitu ambavyo ni vigumu na hatari kuvijua na wengine milango hii huita milango ya kuhama mtu kiroho yaani inasimama kwenye nguvu ya maisha ambayo ni ngono,kuzaa,kufa na maisha baada ya kufa na pia itaonyesha kutatokea nini baada ya wewe kufa na vipi unaweza kurekebisha kwa hawa utakao waacha vyote viwili mwili na roho yako pia pesa za mwenzi wako auurithi wa aliyekufa madeni na majanga yote yapo hapa mikosi ya kuzulumu marehemu na mizuka ya watu waliokufa kutokutulia au kutolewa kafara na ndugu au kuuliwa na jamaa au kufanyiwa ufisadi na watu yote hayo yapo hapa pia ni mlango unaozungumzia kifo ingawaje siku zilizosalia ni mipango yake Mwenyezi Mungu katika kutizama na mlango huu ni pia hapa utaweza kuona katika safari yako ya maisha tunatizama kama wewe unatatizo gani ambalo ni hatari zaidi na baya sana na giza lililopo kwako na hatari uliyo nayo hatutizami siku ya kufa maana anaijua Mwenyezi Mungu pekee lakini aina ya kifo pia sita tizama japo nayo inawezekana kwa watu wengine wenye maamuzi binafsi, Pia magonjwa ya ngono na zinaa yapo hapa na maradhi ya sehemu za siri

9: MLANGO WA TISA: Safari ya Maisha
1091950

kwenye malango huu wa tisa huu ni mlango unaohusu akili ya mtu na na safari ndefu huu tofauti yake na mlango wa tatu ni kwamba mlango huu unazungumzia safari ndefu za mbali hata nchi za nje vipi utaenda na sababu nini na pia mlango huu unazungumzia elimu za kiroho na ndoto na pia elimu au ualimu na mengineyo yanayohusu humo pia wana falsafa na nguvu za ubongo kutanua uwezo wako wa kifikra na safari za nchi tofauti yote hayo unaweza kuyaona kupitia mlango huu wa tisa ambao pia unazungumzia waganga na mbinu za kuwa mganga wa kwenye na visions yote yapo hapo ukitaka kuyajua
mapaja maradhi yake ni hapo

10: MLANGO WA KUMI: kazi na mambo ya jamii
1091951

Mlango huu unazungumzia maswala yako yote ya kazini na aina ya kazi zenye mafanikio kwako pia katika kujituma kwako unafaa kufanya kazi zipi zipi usifanye ipi ujihusishe nayo ipi uache, nguvu yako ni ipi na uwezo wako ni upi kazini wenzio wanakutizama vipi na vipi uende nao sawa wafanya kazi wananjama gani na wewe na wewe upo katika hali gani kwenye taswira zao uwajibikaji wako ni upi na unamsaada kiasi gani kwa watu. pia maradhi ya maungo yapo hapo

11: MLANGO WA KUMI NA MOJA: Jamii na msaada
1091952

Huu ni mlango unaohusiana na marafiki,tumaini na mafanikio ya kimsaada, huu upo kinyume na mlango wa tano ambao unahusu starehe za haraka lakini huu unahusu matakwa ya mtu ya muda mrefu kama ndoto zake na ushindi wa muda mrefu, pia huusiana na mambo ya anasa kama club,tamasha,matukio ya starehe,pombe,ofisi za zinaa,pia ni mlango unaokufanya au kukuonyesha jinsi ya kustarehe na wengine na njia za kuwaingia na pia mlango wa mawazo na utendaji wa kijamii na mengineyo

12: MLANGO WA KUMI NA MBILI: Siri na majini
1091953

Hapa kama ni mchawi,una jini au una una siri ya mtu unataka kuijua tunaitizamia hapo,pia ni mlango unaohusisha majuto kunyanyapaa, kufedheheka kushindwa kujisaidia na kupoteza matumaini, na ndio moja kat ya milango ya ajabu pia ambao una uhusiano na vita za kisirisiri na kulogana yote yapo hapo na kila ubaya wa kificho yote yanapatikana kwenye mlango huo kufungwa,kutoloka na pia ndio mlango unaohusiana na nguvu za miujiza au majaaliwa wengi huuita mlango wa Karma na ndio mlango pekee wa kujua nguvu za mtu za miujiza ni zipi na kama anafit kwenye elimu ya kiroho.

Fahamu ya kwamba chochote unachotaka kutizama au kumtizamia mtu au unachotaka kufanya basi muongozo mzima upo humo kwenye hiyo milango na majibu na jinsi ya kufanya yapo humo,

Tukikusanya yote hayo tunapata maada nne yaani;-
  1. udongo
  2. maji
  3. moto
  4. upepo
Na ndiyo zinazozungusha kila kitu na kila kiumbe hai.
kama una swali ambalo ni personal na upo nje ya Jamii forums:

Wasiliana nami kupitia:
Email: rakimsspiritual@gmail.com
Whatsapp no: +255 783 930 601

Kwa haya na mengineyo:
Tembelea:

Rakims

Rakims
 
Habari wakuu,
Natumai nyote ni wazima lengo la thread hii ni kwa wale wanaohitaji kutazama milango yao yote 12 kwa karata pia kwa usulil hikmat na divination ya milango 12 pamoja na kufahamu yote yanayohusiana na target pamoja na betting na kujua kama wewe upo ok katika fani ya kubet na siku maalum na muda maalum Wa kufanya betting..

Kwa wanaohitaji pia kupata jambo linachelewa kujua ufanye nini karibuni na mengineyo mengi yanayohusu maajabu na miujiza karibuni...
Milango 12 ni hii:

1: Mlango wako binafsi
2: Mlango Wa pesa na nafasi
3:mawasiliano
4: mizunguko na asili
5: mbinu jinsia,na ngono
6: afya na Huduma
7: ndoa na mwenza
8: aina ya kifo na ufufuo
9: Akili na safari ndefu
10: kazi
11: marafiki na jamii
12: Siri na Majini

Kwa wale ambao ni wataalam pia nawakaribiasha
Natumia Ifreet Wa karata,ifrit Wa kitabu na ifrit Wa Geomancy
@mzizi_mkavu
Rakims /spiritual man
Niangalizie hyo namba 7
 
Habari wakuu,
Natumai nyote ni wazima lengo la thread hii ni kwa wale wanaohitaji kutazama milango yao yote 12 kwa karata pia kwa usulil hikmat na divination ya milango 12 pamoja na kufahamu yote yanayohusiana na target pamoja na betting na kujua kama wewe upo ok katika fani ya kubet na siku maalum na muda maalum Wa kufanya betting..

Kwa wanaohitaji pia kupata jambo linachelewa kujua ufanye nini karibuni na mengineyo mengi yanayohusu maajabu na miujiza karibuni...
Milango 12 ni hii:

1: Mlango wako binafsi
2: Mlango Wa pesa na nafasi
3:mawasiliano
4: mizunguko na asili
5: mbinu jinsia,na ngono
6: afya na Huduma
7: ndoa na mwenza
8: aina ya kifo na ufufuo
9: Akili na safari ndefu
10: kazi
11: marafiki na jamii
12: Siri na Majini

Kwa wale ambao ni wataalam pia nawakaribiasha
Natumia Ifreet Wa karata,ifrit Wa kitabu na ifrit Wa Geomancy
@mzizi_mkavu
Rakims /spiritual man
shirku billah
 
Back
Top Bottom