Bado Siku 32, kufikia siku ya Uchaguzi Mkuu 2020 tarehe 28 oktoba, 2020.
Ibara ya 5(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977
Inasema;
Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.
Ili uweze kutimiza Haki hii ya Kikatiba ya kuchagua yani kupiga kura ni vyema uwe umejiandaa na mambo kadhaa kama vile
> Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura,
> Kuwa na Kadi ya Mpiga Kura
> Kuhakiki Taarifa zako kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
> Kushiriki kwenye Kampeni za Wagombea kwa kusikiliza na kuelewa Ilani na Sera za Vyama vyao vya Siasa ili uweze kufanya maamuzi sahihi
Pia ni vyema kushiriki au kupata Elimu ya Mpiga Kura kutoka kwa Tume ya taifa ya Uchaguzi pamoja na wadau wa Uchaguzi waliopewa vibali na Tume kutoa Elimu ya Mpiga Kura kamavile Asasi za kiraia pamoja na vyombo vya Habari.
Elimu hiyo itakuwezesha kufahamu mambo kadhaa kama vile
> Hatua za upigaji kura
> Tofauti kati ya Karatasi ya Kura ya nafasi ya Rais, Mbunge na Diwani
> Masanduku ya kura na tofauti zake
> Sehemu ya faragha ya kupigia kura yani Kituturi
Baada ya kufahamu hayo utakuwa umejiandaa vyema kwajili ya Kupiga Kura siku ya Jumatano tarehe 28 Oktoba, 2020.