Kuelekea Tanzania ya viwanda

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,721
515
To Whom It May Concern.

Kwanza nimpongeze Rais wetu MH. JPM kwa style ya utawala wake na kwa hatua mbalimbali anazochukua ktk kusimamia mapato ya serikali, kuboresha huduma za jamii na kushajihisha uwekezaji ktk viwanda . Nimeguswa kushauri yafuatayo.

1. Kufanya juhudi za makusudi ktk kufufua kiwanda cha matairi cha General Tyre kilichopo Arusha. Hapa kuna swala la ajira, kodi na kupunguza gharama kwa serikali walau kwa kupata huduma ya tairi kwa namna ambayo serikali inaweza dhibiti matumizi (swala la manunuzi).

2. Pale inapogundulika kuwa serikali ilifanya makosa/uzembe mfano ktk ukusanyaji wa kodi kupitia ushuru wa magari basi weledi na busara zitumike ktk ukusanyaji ikizingatiwa kuwa wananchi ni wateja kwa serikali. Vinginevyo itakuwa ni kama serikali inawakomoa wananchi. Hivi karibuni serikali ilitoka usingizini na kubaini kuna ushuru wa magari ambao haujakusanywa kwa zaidi miaka 3,4,7 na hata 10. Kwa upande wa walipa kodi kumekuwa na sababu nyingi kama magari husika kutotembea kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubovu/ajali au kuuzwa kama chuma chakavu na ukosefu wa ufahamu mzuri wa taratibu za kodi na utoaji taarifa. Badala ya kutoa elimu zaidi na kuweka mipango mizuri ya kupata mapato yaliokuwa " yamepotea" kumekuwa T TRA na wapiga deal wenzao (Auctioneers) wamekuwa na mlipuko wa kukamata magari kwa kushtukiza na kudai kodi za papo kwa papo. Unategemea vipi kulipwa milioni kadhaa kwa mtindo huu wa kushtukiza. Kibaya zaidi zoezi limekuwa na udhalilishaji kwa kiasi fulani. Tuache unafiki kama ni kodi TRA ina anuani za wahusika ni vyema wakawasiliana badala ya kufanya mambo kienyeji ktk zama hizi za ICT.

3. Nimependa sana dhana ya viwanda. Sina uhakika kama serikali ya JPM inazungumza lugha moja ktk hili. Tumeshuhudia vituko vya TANESCO. Niseme tu sina hakika ktk ngazi ya wizara kama kuna mawasiliano. Kilimo, Viwanda, Nishati, fedha, OWN nk ni lini wamekaa kuweka mikakati ya pamoja? Au ni mikakati ipi ya pamoja tulionayo kwa sasa? Haingii akilini kodi ya kununua machine ndogo tu ya kuchakata jusi au unga unaishia kulipia kodi mara tatu ya gharama halisi...hii ni deterrence kwa uwekezaji hususani kwa wawekezaji wa ndani.

4. Mwisho nimalizie swala la kodi. Kwa kweli MH. JPM yuko sahihi ktk leadership hasa pale anatoa maamuzi na kusemekana anaingilia mamlaka zingine. Ukiwa na Bunge useless kama hili linalopitisha miswaada kwa kujitazama lenye ni lazima JPM afanye kazi ya ziada. HAINGII AKILINI MTU ANUNUE GARI KWA SAY USD 2000 TRA waamue value wanayotaka wao say USD 4500 . No wonder kuna watu wanatelekeza magari yao kwa sababu regime kandamizi ya kodi. Magari mengi maana yake kodi kupitia mafuta nk.

Tunahitaji kubadilika
 
Safiii.. how viwanda bila mazingira rafiki kwa entrepreneur haitofanikiwa,
.Mazingira rafiki

1.miundombinu bora na wezeshi

2.kupunguza mlundiko wa kodi za mapato

3.ushirikwishwaji wa wananchi katika kutunga sera stahiki za ukuzaji viwanda.
 
Yote anayajua mh.hakna ushirkishwaj awamu hii! Mpiga ngoma yy, mchezaji yy! Patamu hapoooo! Amekua na nia njema lakn kidole kimoja hakivunji chawa!

MACHOZI ya watu ndo yanampa faraja mkuu! Mfalme Juha!
 
Mada za hovyo hovyo bora mfungue shule muende peleka huu upuuzi wako kwenye vi group vyenu vya wasap vya Uvccm.
 
Back
Top Bottom