Kuelekea siku ya valentine

Kuelekea siku ya valentine

DanbyHR

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
286
Reaction score
395
Hello!! Habari??

Hivi watu wanaotumia platform hii kutafuta wapenzi waume/wake hasa wale wanaotaka kufikia kabisa kwenye malengo ya juu kimaisha Ndoa?? Wanakuwa wako serious kweli?? Mbona siwaelewagi hata kidogo. Au kuna creteria zingine wanakuwa nazo??

Katika pita pita zangu huwa nakutana na nyuzi za watu wanatafuta wapenzi especially wale wa kiume, kwa kuwa mi niko zangu single mpaka sasa, huwa naona kwanini nisiungane na huyu mwanamke tuwe couple... Siwaelewi yani kaweka kabandika tangazo lake, af huko PM akifuatwa ananuna, hatoi ushirikiano. Mi wananikera si bora angekausha tu.

Kuna wanawake kadhaa, mi nilienda nao vizuri PM mpaka tukahamia kwenye mawasiliano ya simu namba. Sasa wakaanza leta vidude vyao hata sivielewi mfano mmoja akaanza kusema we muda wote uko online unafanya kazi sa ngapi?? Siwezi fanya kazi zangu bila Internet, so najikuta tu nakuwa online muda wote. Akanitosa.

Mwingine nae, tumeongea, tukaanza pendana wee!! Penzi limekolea akagundua mi kadogo, nina 26 years ye ana 31 na mtoto juu. Akanibwaga. Nkala za mbavu. Sasa visababu vinavyofanya mnipige chaga sivielewi kabisa. Online?? Miaka?? Wa miaka nilimwambia kabisa sijui hakuzingatia. Akanibadilishia habari mi nshaanza kukolea kaa moto wa kifuu.

Sasa hawa ambao hawajibu huko PM mbona wanaleta ukuda, unamwambia mtu njoo PM kama una nia ya kweli, afu akija unamkaushia. Mnanikera kwa kweli. Maoni yangu kama application pool imejaa ndo unafanya selection we sema tu, sio kukaa kimya. Asantee.

Location : Hawaii Bar, Baruti.
IMG_20200210_144739_400.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Geofrey Daniel,

Pole mdau...ndo watu walivyo...most of ladies are very selective sometimes ndo maana hata wanakosa wenza...wengine wanaangalia kipato wengine wapo kwa ajili ya kudanga tu...kaza buti wewe bado ni kijana mdogo utapata mwenza tu..

Hao mabint wenye 30s ndo wenye stress wewe hata sion sababu ya kuhangaika kutafuta patner kwenye mitandao...
 
Kuelekea siku ya Wapendanao, iwapo mpenzi wako atataka vitu vitamu *(chocolate, cakes sijui maua)* siku hiyo, mwambie hata Biblia inakataza akasome[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541]

*Hesabu 9:11*, "Jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Ataiadhimisha kwa kula mikate isiyotiwa chachu na mboga chungu".

ASANTE
 
Kumbe ma single boy tuko wengi. Masingle wote nipende kukuambieni kuwa siku ya valentine kwetu itakuwa ni tar. 14 mwezi wa pili tu, itakuwa siku ya kawaida kama ilivyo leo tu.
 
Back
Top Bottom