Kuelekea Dar Derby VPL Simba SC dhidi ya Yanga SC, One Touch Operation 3 Points

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Hello Hello!

Kuelekea Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL Jumamosi January 4, 2020 utapigwa mchezo wa watani wa jadi (Dar Derby), ambapo mabingwa wa nchi Simba SC mnyama mkali, wanawakaribisha Yanga SC kwenye Uwanja wa Taifa.

Mchezo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote hasa ukizingatia ni mchezo wa kwanza kwa watani wa jadi kukutana kwa msimu huu wa Vodacom Premier League VPL 2019/2020.

Simba SC, inaongoza ligi kwa alama 34, dhidi ya Yanga SC yenye alama 24 wanataka kuwahakikishia Wanasimba na Wadau wa soka kwamba hawaongozi ligi kwa bahati mbaya bali kutokana na uwezo wa kikosi chao ambacho kimesheheni nyota wengi wenye uwezo mkubwa wa kupata ushindi pamoja na kutoa burudani uwanjani.

Yanga SC, kutaka ushindi mchezo huu, wana kikosi cha kawaida sana pia wana shida nyingi ndani na nje ingawa kwa sasa wanajitahidi kupunguza shida hizo, lakini kila mmoja anajua kwamba kuna matatizo ya wachezaji kudai mishahara pamoja wengine kuvunja mikataba yao.

Watu wanaofuatilia kandanda wanajua kwamba kwa sasa ukitaja timu bora hapa nchini Tanzania ni Simba SC, yenye uwazo mkubwa wa kiuchumi hivyo basi kupelekea kuwasajili wachezaji mahiri wenye kuamua matokeo ya ushindi uwanjani.

Wanasimba jongea hiyo January 4 2020 kushuhudia kandanda safi lililothibitishwa na shirikisho la soka Afrika CAF kutoka kwa Simba SC, One Touch Operation 3 Points, Kulitaka Mwana, Kulipewa Mwana

SimbaNguvuMoja Next Level
IMG_20200103_081625_641.jpeg
IMG_20200103_083310_328.jpeg
IMG_20200103_083250_233.jpeg
 
Hii ni Derby ambayo SIMBA ananafasi kubwa ya kupata point tatu kutokana ubora wa kikosi chake lakini kwa mpira lolote linaweza kutokea kwasababu kwenye derby timu zinakamia sana
 
Watu mnaishi kwa Historia eti hujui.....derby zinavyokuwa.....
Kila kitu kipo wazi kuwa yanga ni mbovu.
Mchezaji ametua juzi kesho anacheza afu unatarajia matokeo.
Walahi umemaliza hapo, unajua kuna watu akili zao za kizamani na hawajui lolote.

Hao ndo wale Mwekezaji ni Wananchi
 
Walahi umemaliza hapo, unajua kuna watu akili zao za kizamani na hawajui lolote.

Hao ndo wale Mwekezaji ni Wananchi
Wakubali tu saiv wanaokotana.....kama ndondo.
Haya naskia mcheza karate lamine hatokuwepo......
Mchezaji waliyemuokota mwingine sijui tariq naye.....hayupo.....
Kifo kinawahusu hawa kesho.
 
Wakubali tu saiv wanaokotana.....kama ndondo.
Haya naskia mcheza karate lamine hatokuwepo......
Mchezaji waliyemuokota mwingine sijui tariq naye.....hayupo.....
Kifo kinawahusu hawa kesho.
Haraka zote zile ili awahi game na Simba, hatakuwepo?
 
Back
Top Bottom