Tumekuwa na utaratibu wa sisi wananchi kuwaachia wanasiasa hatma ya maisha yetu katika jamii zetu tunazoishi.
Nashauri tuanze utamaduni mpya wa kabla ya chaguzi zozote zile na hasa za mitaa tunayoishi, tuwe na mikutano huru ya wananchi katika eneo husika bila kuingiliwa wala kupenyeza itikadi za vyama, tuainishe mambo ya msingi na kutengeneza dira ya miaka 5.
Dira hii tuwape wale wote wanaohitaji kutuongoza waje na mipango au sera za namna gani wataweza kuyafikia yale tuliyowapa.
Pia hii itatusaidia kuwa kipimo cha utendaji wake. Tusiwaachie wao kuwa watengeneza sera na irani za vyama, kwani haya ndio yametufikisha tulipo.
Natumaini mtaa utakao weza kutumia ushauri huu tunaweza kushuhudia ukipiga hatua kubwa ya maendeleo.
Nakaribisha mawazo ya kuboresha kwa lengo la kujenga.