Kuelekea 2020 upinzani hatuna namna, twendeni na Zitto Kabwe

Jef Kirhiku

Member
Dec 10, 2016
39
76
Nimefanya tathmini na kuwatizama wanasiasa wote waliopo upinzani na kugundua hakuna anayeweza kuuzika na kufanya vizuri uchaguzi ujao zaidi ya Zito Kabwe . Ana uwezo mkubwa wa uongozi ,ana maarifa ya kutosha ,hekima ,busara na ukomavu wa kiwango cha juu .

Anaweza kuvutia makundi mengi zaidi na kuakisi mahitaji ya uongozi ya kizazi cha sasa kuliko mwanasiasa yeyote mwingine ndani ya upinzani .
Vyama vyote vya upinzani wekeni tofauti zenu pembeni anzeni kumjenga na kumuandaa zito kabwe kuelekea 2020 . Lowasa hata akigombea hatoweza hata kufikia rekodi yake ya uchaguzi wa 2015.

Ni vyema akapumzika na kubaki kusaidia upande wa ushauri na mikakati .
Ukichanganya kura za upinzani ,wasio na vyama ,ccm waliochoshwa na masimango na kufokewa ,kura za chuki na hasira toka kwa watumishi wa umma Zito kabwe anaweza kushinda uchaguzi 2020.
 
Ndio kazi ya chadema siku hizi kuombea kila aina ya maovu yatokee Tanzania.

Tume inakuwa nzuri na huru inapowatangaza washindi Mbowe, Lisu, Lema, Mdee etc

Lakini tume hiyo hiyo inakuwa siyo huru inapowatangaza Magufuli, Zungu, majaliwa, Nchemba etc
 
Naona unataka yule mzee afe kwa pressure. Huoni anavyozunguka kukamilisha watu kuwa yeye ndo right person 2020? Mkuu kuwa na huruma basi.
 
Kutoka upinzani tunapaswa kutizama uwezo wa mtu zaidi kuliko uimara wa taasisi kwa sababu vyama vyote vya upinzani ni dhaifu mno .
Hatuwezi kwenda na ukawa hii ya sasa iliyosambaratika lazma tubuni ukawa mpya itakayojumuisha wanasiasa vijana wenye uwezo na vipaji kama zito kabwe .
Kwa sasa ukawa ni chadema tuu cuf na Nccr zimeshakufa watu washagawana mbao .
 
Ujana nao ni sifa? Hoja ya ujana ilipingwa kumbo uchaguzi uliopita. Bado mnaibeba.
 
Zitto alikuwa ni yule wa CHADEMA,Zitto wa ACT wazalendo ana kimbiwa hadi na afande Sele.

Weka Akiba ya Maneno, 2020 sio mbali wenzie tukichimbuwa Thread walizokuwa wanamshambulia Lowassa wanatamani Ardhi ipasuke wafiche nyuso zao. Unajua Yule aliekuwa anaitwa Sisimizi Leo hii ni Kamanda ? Unajua Mwenyekt Mwenza wa UKAWA alipewa kishafanya Mapenzi yasiyofaa?

Kuna Mkakati wa Siri sana wa kujaribu kuwakutanaisha Mbowe na Zitto maana .... for now!
 
Hatutaki one man show aka mungu wao..nashindwa kuelewa masifa mengi mnayo kesha kumpa sisi tunamuona wakawaida tu..yaan toothless dog..hutamfananisha na shujaa Kafulila?
Jaman sio yule zito wa chadema..we don't want snitch..MTU akiondoka hatubembelezi wazuri wengi wataungana nasi na mapambano yataendelea..we need really changes..sio misifa ya bila mimi"..
 
Nimefanya tathmini na kuwatizama wanasiasa wote waliopo upinzani na kugundua hakuna anayeweza kuuzika na kufanya vizuri uchaguzi ujao zaidi ya Zito Kabwe .
Ana uwezo mkubwa wa uongozi ,ana maarifa ya kutosha ,hekima ,busara na ukomavu wa kiwango cha juu .
Anaweza kuvutia makundi mengi zaidi na kuakisi mahitaji ya uongozi ya kizazi cha sasa kuliko mwanasiasa yeyote mwingine ndani ya upinzani .
Vyama vyote vya upinzani wekeni tofauti zenu pembeni anzeni kumjenga na kumuandaa zito kabwe kuelekea 2020 .
Lowasa hata akigombea hatoweza hata kufikia rekodi yake ya uchaguzi wa 2015.
Ni vyema akapumzika na kubaki kusaidia upande wa ushauri na mikakati .
Ukichanganya kura za upinzani ,wasio na vyama ,ccm waliochoshwa na masimango na kufokewa ,kura za chuki na hasira toka kwa watumishi wa umma Zito kabwe anaweza kushinda uchaguzi 2020.
Nitawaona CDM hawana akili kama wanafikiria kumsimamisha Lowassa. Maana kilichompa kura 6m siyo kupendwa kwa upinzani ni mtafaruku ndani ya CCM ambao unaweza kudhibitiwa miaka hii Mitano kwa 60% na kupunguza kura za Lowassa huku za Za JPM zikiongeze kwa 3.6 na kuwa 11.9 wakati Lowassa akiambulia 2.4 tu!! Hawatakuja waamini lakini ndio itakavyotokea hivyo!!
 
Naamini itafanyika coalitions ya maana kwenye upinzani kabla ya 2020.

BTW bila tume huru upinzani kushinda uchaguzi ni ndoto.
 
Kutoka upinzani tunapaswa kutizama uwezo wa mtu zaidi kuliko uimara wa taasisi kwa sababu vyama vyote vya upinzani ni dhaifu mno .
Hatuwezi kwenda na ukawa hii ya sasa iliyosambaratika lazma tubuni ukawa mpya itakayojumuisha wanasiasa vijana wenye uwezo na vipaji kama zito kabwe .
Kwa sasa ukawa ni chadema tuu cuf na Nccr zimeshakufa watu washagawana mbao .
Zitto hana uwezo wa kiwango unachotaka kutuaminisha, hana pumzi ya kuhimili changamoto, na kwa kiwango fulani hana tofauti sana na aliyepo sasa katika baadhi ya mambo!
 
Tatizo la zito ni mtu asiyeaminika, watawala wakimsogelea ana side nao kisiri, usaliti mwingi sasa hivi anaonekana mkali kwa kuwa system haimuitaji. Cku wakiweka dau mezani utashangaa zito anataka kuwa juu ya wenzake. Kiufupi antumia kipaji chake kujifaidisha na siyo kupigania maslahi ya kundi
 
Back
Top Bottom