Kuelekea 2020 ubunge CCM kinaweza kushindwa vibaya sana.Anaweza kubaki Magufuli peke yake

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Wadau nikionacho kwa sasa kwa jinsi ambavyo wananchi wanawananga wabunge wa CCM ni dalili kua hali si shwari, wamepoteza imani kabisa na wabunge wa CCM! Imani yao kwa sasa imebaki kwa Magufili tu ambaye nao bado wengi wanasema hawawezi kumwamini 100% maana hali ya maisha inazidi kua mbaya siku hadi siku tofauti na walivyoahidiwa wakati wa kampeni.


Kitu ambacho wengi wa wabunge wa CCM wanasubiri ili kushinda ubunge katika majimbo yao ni kushikwa mkono na raisi Magufuli kuwaombea kura, Kwa bahati mbaya sana wananchi wa sasa ni waelewa sana wameshagundua ni nani anawasemea matatizo yao, kinachoonekana ni kua wananchi hawataangalia jina la chama ispokua ni aina ya mbunge watakayempenda kwa uwajibikaji wake na sio uwajibikaji wa Magufuli kumbeba mtu.


Ninachokiona kwa sasa ni kwamba wapinzani wameshawagundua madhaifu yaliyoonekana katika uchaguzi uliopita ikiwa ni pamoja na kulazimisha kurudia kuhesabu kura upya badala ya kutumia forms za matokeo ya kwenye vituo zilizokwishasainiwa na mawakala wa vyama,kiingine ni umakini wa TAKUKURU ya sasa kuwakamata watakaogawa rushwa kitu ambacho hua ni Kama daraja kwa wengi wasiojiweza, kiingine ni kutumia polisi kuwakamata wagombea wa upinzani ili kupenyesha kura feki.


Kinyume na mataranio ya wengi ni kwamba ikitokea Maguguli akashinda uchaguzi anaweza kujikuta na wabunge wachwanawanangaCM hali itakayomuwia ngumu kuendesha serikali atakavyotaka.
 
Tatizo wananchi hawajielewi ccm ni ileile hata wamuweke nani hakutakuwa na mabadiliko. Wananchi wanahitaji elimu ya kujua haki zao hapo ndio ccm itaondoka bila ya hivyo labda 2090 tusubiri. Manake sijawahi kusikia Punda akageuka Farasi
 
ndoto za alinacha, ccm itatawala milele! bavicha mlishafeli kitambo, sasa ivi nenden monduli mkanywe maziwa ya bure!
 
Tatizo kubwa hao wabunge wa upinzani hawana tofauti na wabunge wa CCM .
 
hadi miaka 5 ipite wataelewa maana halisi ya mfumo, pia watapata majibu ya swali hili kwa nini wanye akili waliona ccm ni ileile?
 
Back
Top Bottom