figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Sasa kumekucha, Edward Lowassa ameanza kufyeka Vichaka upya ikiwa ni maandalizi ya urais 2020. Nahisi kuna madhaifu ameyaona kwa rais aliyepo. Kila la heri.
Lowassa akisalimiana na viongozi wa kikundi cha walemavu mto wa mbu katika mkutano wa kuimarisha chama Wilayani Monduli leo. Aliambatana na Salum Mwalimu
Aliyekuwa mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya UKAWA kupitia CHADEMA na mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA Edward Lowasa amewataka watanzania kutambua kuwa CHADEMA bado kipo imara kitaendelea kuwatumikia na kwamba chama hicho hivi sasa kinajengwa kitalam zaidi.
Mh.Edward Lowasa ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na umati wa wapenzi wanachama mashabiki wa CHADEMA na watanzania wengine katika mjiji mdogo wa Mto wa Mbu wilaya ya Monduli ambapo pia amewataka watanzania kudumisha amani na kuwa na subira kwakuwa wakati wa utawala wa ukombozi wa CHADEMA unakaribia.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Salum Mwalimu amesema watanzania wanakila sababu ya kumshukuru Mh.Lowasa kwa utulivu aliyo uonesha baada ya uchaguzi na kuwa Lowasa anajali utu zaidi kuliko maslahi yake na mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Isack joseph akiahidi kutenda haki katika utawala wa CHADEMA kwenye Halshauri hiyo.
Katika mkutano huo pia watu wenye ulemavu walipata nafasi ya kutoa shukrani zao kwa wanasiasa baada ya uchaguzi mkuu wakidai panapo tokea machafuko wao ndiyo maathirika wakubwa.