Kuelekea 2015, USHAURI wa Bure kwa Mhe LOWASSA

Kuelekea 2015, USHAURI wa Bure kwa Mhe LOWASSA

Mhe. AJAYE

Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
32
Reaction score
6
Mhe LOWASA! inafahamika​ ww ni mmoja kati ya watu wachache waliojipambanua wazi kuwa wana nia ya kugombea URAIS 2015, na ni ww ndiyo kati ya watu wenye nguvu kubwa ya kupata cheo hicho 2015, kwanza nikupongeze kwa harakati yako ya kuisaka nafasi hiyo ya juu ya uongozi Tanzania. Yapo mambo kazaa ambayo napenda uyafahamu na napenda nikushauri, ningepata nafasi ya kukaa na wewe nafikri ningeweza kukushauri kirefu zaidi, lkn kutokana na ugumu wa kuonana na ww, Yafautayo napenda uyafahamu;

1) Watanzania zaidi ya 50% wanaojitambua na ambao siyo wanaCCM wanapenda uwe rais wa Nchi kuanzia 2015...
ni kwa kuwa wanafahamu mchango wako ktk maendeleo ya nchi yetu kipindi cha uongozi wako.

2) Watanzania wanajua kilichofanyika mpaka ikapelekea UJIUZULU nafasi yako kama waziri mkuu.

3) Pia, watanzania zaidi ya 60% kwa sasa hawaitaki ccm

4) Na zaidi ya 70% ya watanzania huchagua chama na siyo uwezo wa kiongozi AS INDIVIDUAL

5) Kingne, ufahamu kuwa kwa sasa CCM haishindi kihalali bali wanatumia ubabe wa vyombo vya Usalama na nguvu ya fedha.

Mhe; Kutokana na hayo yote napenda nikushauri yafuatayo kama njia mbadala za kuweza kutimiza ndoto zako za kuwa Rais wa nchi na kuleta maisha bora na maendeleo kwa nchi yetu

a) Kutokana na chama chako kutokubalika kwa Watanzania wengi kwa sasa ( sababu ziko wazi kwa kila mtu) na kwakuwa kuna zaidi ya 50% ya wataz wasio wanaCCM wanaopenda uwe Rais wa nchi, Mhe, LOWASA ili upate kushinda kwa urais itakuwa vyema kama/endapo utajiengua CCM (ama ugombee kama mgombea binafsi au tafuta chama kingne, kama ACT au ADC), hii itakusaidia kuchukua ile 60% ya watu ambao hawaitaki CCM kwa sasa, itakusaidia pia kuwa na uhakika wa kuipata ile 50% ya wapiga kura wanaojitambua.

b) Tafuta wafuasi wengne nje ya ccm watakao Ku-support ktk harakati zako, hii ni kwa sababu kwa kuendelea kutumia makada walewale wa CCM (Kina kigwangala, Serukamba n.k) wananchi hawatakuwa na IMANI na ww na wanakuwa na mashaka ya kumwingiza Shekhe yuleyule mwenye kanzu tofauti

c) Kwa kuwa % kubwa ya watanzania wanajua kilichokufanya ujiudhulu, wanajua kuwa ulitolewa kafara ili kuficha makubwa yaliyokuwa nyuma ya pazia, plz waelezo watz A-Z ya kilichotokea kwenye sakata la Richimondi hadi kupelekea ww kuwa MBUZI wa KAFARA,na itakuwa vizuri endapo kama utatutajia majina ya wahusika waliokuwa nyuma ya PAZIA, hii itakuongezea idadi ya wapiga kura na itaondoa utata kwa wale ambao wanaIMANI ya kwamba et ww ndo ulikuwa mhusika wa Richimond.

Mhe...! Chukua hayo machache.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom