KUDURO from Angola / Tchiriri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KUDURO from Angola / Tchiriri

Discussion in 'Entertainment' started by Sikonge, Jun 20, 2009.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Katika pitapita nimekumbana na hii dance kutoka Angola ambayo nasikia imeifunika kabisa Kizomba. Kuduro ni dance ambayo ilianza kuchezwa mara baada ya vita na walikuwa wakicheza pamoja. Kwa wale wazee watakuwa wanakumbuka jinsi mashuleni zilikuwa zikipigwa Soca dance, mnapanga mstari na kuanza kucheza pamoja na hii iko kwenye form hiyo.

  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=uA6pPWGWnHw&feature=related"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

  Na ukiisikia haileti tofauti kubwa na mdundiko wetu wa Dar wa akina Mzee Mbegu " Kilakshare kilakshare, Pugu Kariakoo...". Ila baadaye ikaja Kuduro ya vijana ambayo wanaicheza kama Breakdance. Ukiisikiliza na kuangalia utaona kuwa imechanganya na kitu kama techno music/House???

  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=wAZqqZiVxkg"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

  Hapa mwisho, jamaa katengeneza MCHANYATO wa hizo KUDURO zote yaani kwa Wazee na Vijana na kwa mataifa yote wapenzi wa KUDURO.

  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=cmLlHrWM0PE"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

  Ukiangalia sana utagundua kuwa wimbo uliotamba zaidi unaitwa TCHIRIRI, na ukitaka kuuangalia basi waweza nao kuuona kwenye YOUTUBE.
  Kwa ujumla ni dance nzuri sana hasa ile ya Wazee na ukiwaangalia hawa jamaa hadi unapata hamu ya kudumbukiaMO kwenye screen na kuanza kucheza hiyo Kuduro yao. Nawatakieni weekend njema.

  NB: Kuna Film tayari juu ya hii dance "LUANDA, A FABRICA DE MUSICA" au Luanda, kiwanda cha Wanamusiki. Mwandishi na Director ni Kiluande Liberdade, Inzs Gonealves. Ni Documentally film na imebase kwenye nchi za Angola na Portugal.
   
 2. I

  Ipole JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu sikonge mambo makubwa haya lini ulikuwa huko
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nguguye Ipole,

  Mie na Angola wapi na wapi? Pita pita yangu kwenye MITANDAO tu na sikuwa nimeshafika huko. Niseme ukweli kuwa huwa naona aibu kuwa hata Zanzibar sijafika. Ila ntajitahidi nikifika Dar basi lazima nende hadi Zenji nikaonane na Kibunago tupate bia baridi siku ya kwanza na siku ya pili tumalizie Juice ya Mtende.....

  Yes Ipole, hilo ndilo Kuduro, limewapagaisha hasa Wazungu. Sijui sisi mwanamuziki gani atakuja wapagaisha hadi Wazungu kwa miziki yake? Tatizo naona tunaiga sana badala ya kuchukua chetu na kukibadilisha kiwe cha Kisasa.

  Ningelikuwa mwanamuziki, basi ningelijaribu kutengeneza miziki ya Mwinamila au Makongoro au hata Manywele (wa Chabutwa, wamkumbuka??) na kuifanya iwe ya kisasa. Tena kwa Tabora kuna hadi akina Mwana Lwelwe wa Migabo (hehee, wanacheza kama Sikinde, ngoma ya UKAE)....."kuimba sana mwisho wake utakufa lofaa......"
   
 4. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  its very big in mozambique aswell!
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kapinga,

  Unafahamu hawa jamaa Angola na Mozambique ni kama sisi na Kenya ila sema tu hawa common Border. Ila kama sikosei, wao na Angola na ukamalizia na Sao Tome and Principe, walitawaliwa na Waportugal. Hata yule mwana muziki Afric Simon, alitoka Brazil na kuanza kutesa na miziki Mozambique, kabla hajaibuliwa na ma promotor na kupelekwa Ulaya.

  Angola na Mozambique hufanya sana fujo kwenye michezo mbalimbali na watu huwa hawaamini inakuwaje? Kumbe jibu ni kuwa hawa jamaa wamejaa Portugal kibao na huko huwa ni kiasi cha kuamua kuchezea Portugal au kwenda makwao (Angola na Mozambique) na the biggest star katika mpira wa miguu ni huyu bwana Eusébio da Silva Ferreira ambaye nafikiri hadi leo wana mpa heshima kama PELE wa Portugal. Mhhh, hadi sanamu wamemuwekea Eusébio - Wikipedia, the free encyclopedia
   
Loading...